Podcasts by Category

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

RFI Kiswahili

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

289 - Mkuu wa majeshi ya Kenya Francis Ogolla aaga dunia, ziara ya wajumbe wa EU DRC
0:00 / 0:00
1x
  • 289 - Mkuu wa majeshi ya Kenya Francis Ogolla aaga dunia, ziara ya wajumbe wa EU DRC

    Makala hii inaangazia yaliyojiri nchini Kenya na kifo cha mkuu wa majeshi ya nchi hiyo KDF aliyepoteza maisha na maafdisa wengine tisa wa jeshi katika ajali ya helikopta Alhamisi Aprili 18, rais William Ruto alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, mgomo wa wafanyabiashara huko Kampala Uganda, ziara ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa na EU huko Goma kutathmini hali ya kibinadamu kwa waliokimbia mapigano ya M23, Senegal, pia Togo kuhusu ziara ya ujumbe wa ECOWAS, lakini pia mashambulio kati ya Iran na Israel.

    Sat, 20 Apr 2024
  • 288 - Miaka 30 ya mauaji ya kimbari Rwanda, UN yaondoa jeshi lake DRC na mengineyo duniani

    Makala yameangazia mambo mengi ikiwemo maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yanaendelea wiki hii, MONUSCO kuanza kuwaondoa wanajeshi wake eneo la mashariki mwa DRC, mgomo wa madaktari nchini Kenya, mwaka mmoja wa mzozo wa Sudani kutimia jumatatu ya aprili 15 na mengineyo duniani. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi

    Sat, 13 Apr 2024
  • 287 - Maadhimisho ya miaka 30 mauaji ya kimbari nchini Rwanda, uteuzi wa waziri mkuu mpya DRC

    Ni makala maalum, kuhusu kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, tunahoji mchakato wa maridhiano umefikia wapi miaka 30 baadaye..... hali iko vipi kwa sasa. na dunia imepata  somo gani? Pia kuhusu mauaji hayo, tutarejelea kauli ya Rais Emanuel Macron iliyoonekana kuwa inalenga kutuliza hisia za waathiriwa.
    Huko DRC uteuzi wa Judith Tuluka Suminwa, mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu. Mahakama nchini Uganda ilitoa uamuzi wake kuhusu sheria dhidi ya ushoga. Kabla ya kwenda Kenya, Sudani..pamoja na Senegal ambako Bassirou DF aliapishwa kuwa rais mpya, tutakwenda Israeli na maeneo mengine duniani.

    Sat, 06 Apr 2024
  • 286 - Diomaye Faye kuapishwa jumanne kama rais wa Senegal, ziara ya rais wa DRC Mauretania

    Rais mteule wa senegal akutana na rais anayemaliza muhula wake Macky Sall, chama kipya cha aliyekuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma chazuwiwa kushiriki uchaguzi wa mwezi mei,kamati ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa, yaitaka Uingereza kuachana na mpango wake wa kuwahamisha wahamiaji kwenda nchini Rwanda, na rais wa DRC Félix Tshisekedi ahitimisha ziara yake huko Mauretania, tutaangazia siasa za Kenya, Tanzania, yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani.

    Sat, 30 Mar 2024
  • 285 - Rais Museveni amteua mwanae kuwa mkuu wa majeshi, kifo cha okende kilipangwa

    Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Uganda Yoweri Museveni ya kumteua mwanawe kuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo, mazishi ya mwanasiasa Cherubin Okende, yaliyojiri nchini Rwanda, lakini pia Sudan huko ambako wiki hii Marekani ilisema kuwa ina matumaini mazungumzo ya kumaliza mzozo wa nchi hiyo yatarejea hivi karibuni baada ya mfungo wa Ramadan, uchaguzi wa urais huko Senegal jumapili ya Marchi 24 tumeangazia yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani. Ungana nami Reuben Lukumbuka

    Sat, 23 Mar 2024
Show More Episodes