Filtrer par genre

Bongo Bila Borders

Bongo Bila Borders

Sabai na Alexa

Karibu kwenye Bongo Bila Borders — podcast inayozungumzia mambo yanayogusa tamaduni, imani, afya, mtindo wa maisha, mahusiano ya kimataifa, na kadhalika! 💥 Tunavunja stereotypes, tunajenga madaraja ya tamaduni, na tunashiriki hadithi halisi! 🎧 Kipindi kipya kila wiki (Alhamisi) Follow, share na ujiunge🔉 Tunapeleka Bongo duniani kote!💫 #BongoBilaBorders 🌍 #Kiswahilikitukuzwe #Kiswahilikienee

14 - LUGHA NA UTAMBULISHO
0:00 / 0:00
1x
  • 14 - LUGHA NA UTAMBULISHO

    Je, lugha unayozungumza ndiyo kitambulisho chako? 🎙️


    Katika Bongo Bila Borders Episode 13 tunaizungumzia lugha kama pumzi ya utambulisho, kama mwanga unaoangaza njia mpya, na kama mlango unaoweza kufunguka unapozungumza zaidi ya lugha moja. Tunagusia namna maneno yanavyoweza kukuinua, kukutambulisha na kukupa nafasi ambazo wengine hawazifikii kwa urahisi. Lugha ni nguo tunazovaa, ni muziki tunaoubeba, na ni pasipoti ya roho katika safari yetu ya dunia.

    Tunalisheheni pia penzi la Kiswahili, lugha inayokua kwa kasi na kuufikia ulimwengu kwa sauti ya ujasiri. Leo linasikika kwenye utafiti, kesho kwenye biashara, keshokutwa kwenye sanaa na diplomasia. Wimbi lake linapanuka na kuunganisha tamaduni nyingi kama mkondo wa maji unaokutana na bahari. Huu ni wakati wa kuikumbatia lugha yetu kwa fahari, kuiendeleza kwa bidii na kuiruhusu iitupe mbali kadiri upepo wa dunia unavyovuma. ✨

    Karibu usikilize, ujisikie na utafakari nasi, kwani lugha hasa Kiswahili lina uwezo wa kutuunganisha, kututia nguvu na kutupa nafasi ya kuona dunia kwa macho mapya na moyo ulio wazi.

    Thu, 27 Nov 2025 - 26min
  • 13 - SAFARI

    🌍Kwa wengi huko Magharibi, “Safari” ni adventure; picha za simba, tembo na milima mikubwa.

    Lakini kwetu Waafrika, ‘Safari’ ni zaidi ya hili. Bongo Bila Borders inavunja mipaka ya tafsiri, tukizungumza maana halisi ya Safari kutoka mtazamo wa Kiafrika.

    🎙️ Sikiliza sasa Safari ipo hewani!


    #BongoBilaBorders #Safari #AfricanPerspective #HadithiZaKwetu

    Thu, 30 Oct 2025 - 36min
  • 12 - FOOD/CHAKULA

    🇹🇿🍲 Bongo Bila Borders inakuletea ladha halisi za Afrika Mashariki! Kutoka kwa mitaa yenye pilipili kali ya Dar es Salaam hadi vibanda vya chakula vinavyochemka usiku kucha, tunachunguza chakula, tamaduni, na watu wanaofanya jiji hili kuwa kitovu cha ladha barani Africa. 🌍🔥

    #BongoBilaBorders #DarEats #ChakulaChaBongo #EastAfricanFlavors #TanzaniaVibes

    Thu, 23 Oct 2025 - 40min
  • 11 - MUONEKANO | VIWANGO VYA UREMBO

    Katika kipindi hiki, tunachambua tofauti na kufanana kwa viwango vya urembo kati ya Marekani na Tanzania/Mashariki ya Afrika. Ni nani anayeamua nini ni "urembo"? Je, mitazamo ya kijamii, historia na utamaduni vina athari gani kwenye mwonekano? Usikose!

    #BongoBilaBorders #Urembo #Mwonekano #PodcastYaKiswahili #EastAfricaMeetsUSA

    #SwahiliPodcast

    Thu, 16 Oct 2025 - 31min
  • 10 - Transportation/Usafiri

    🚆✈️ Episode 9 imewasili! Leo kwenye #BongoBilaBorders tunajadili usafiri — kutoka 🇹🇿 SGR na TRC hadi 🇺🇸 Amtrak, Greyhound Bus, na American Airlines! 🚍✈️

    Je, unadhani mfumo wa usafiri wa Marekani ni bora zaidi kuliko wa Tanzania? Au tunapaswa kujivunia maendeleo ya reli mpya na huduma za #AirTanzania? 🇹🇿✨


    🎙️ Sikiliza mjadala wetu kuhusu changamoto, teknolojia, na tofauti za kitamaduni katika kusafiri — kutoka mabasi ya moshi hadi ndege za kisasa!

    👇 Tuambie kwenye maoni: Wewe unapendelea kusafiri kwa treni, basi, au ndege? Kwa nini?

    @Amtrak @GreyhoundBus @AmericanAir @sgr_tanzania @tzrailways @AirTanzania

    #BongoBilaBorders #Transportation #SwahiliPodcast #Usafiri #Travel #ExploreTanzania #SGR #TRC #AirTanzania #Amtrak #GreyhoundBus #AmericanAirlines #SafariZaBongo #TanzaniaToTheWorld #CultureTalks #PodcastYaKiswahili #TravelAfrica #CrossCulturalConversations

    Thu, 09 Oct 2025 - 31min
Afficher plus d'épisodes