Filtrer par genre

MAISHA na Koleman Thompson

MAISHA na Koleman Thompson

Koleman Thompson

Karibu kwenye podcast yangu, MAISHA: Swahili Edition! Dhumuni la podcast hii ni kuzungumzia safari zetu za maisha na mambo ambayo tumepitia na kujifunza. Kwa majina naitwa Koleman Thompson. Nililelewa katika jingo la Utah, Marekani. Nilijifunza Kiswahili nilipotumikia kama Mmisionari kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Pia, nina podcast nyingine inayoitwa “MAISHA: English Edition”. Ukitaka kusikiliza kuhusu maisha ya watu waongeao Kiingereza, utafute hiyo podcast. Asante sana kwa kusikiliza!

8 - 7. Sean Olson na Mzungu Mswahili | Two Americans do a Podcast in Swahili
0:00 / 0:00
1x
  • 8 - 7. Sean Olson na Mzungu Mswahili | Two Americans do a Podcast in Swahili

    Jiunge nasi tunavyozungumzia kwa nini tunapenda Kiswahili na utamaduni wa Afrika. Mfuatilie Sean kwenye TikTok @seanolson0237 na unifuatilie mimi kwenye TikTok @mzungu_mswahili

    Sat, 07 Jun 2025 - 32min
  • 7 - 6. Lizbeth Leonard | Maisha ya Vijana wa Tanzania

    Lizbeth Leonard ni mtu mzuri sana ambaye anampenda Mungu na familia yake sana. Nilibarikiwa sana kuishi na yeye na familia yake wakati ambao nilikuwa Tanzania. Aliboresha maisha yangu sana kwa mfano na maneno yake. Kwenye kipindi hiki, tulizungumza sana kuhusu maisha ya vijana wa Tanzania (ikijumuisha umuhimu wao, changamoto zao, na utatuzi kwa changamoto zao). Natumaini kwamba wengine watafaidika kutokana na mazungumzo haya.

    Sun, 25 Aug 2024 - 53min
  • 6 - 5. Mwalimu Vinold John | Utamaduni na Lugha ya Waswahili

    Vinold John ni mwalimu bora kabisa na nimefurahi kujifunza kutoka kwake mara kwa mara kwenye progamu hii hapa Tanzania. Anapenda sana kufundisha kuhusu utamaduni na lugha ya Waswahili. Katika kipindi hiki, tulizungumza mawili matatu kuhusu mada hizo, pamoja na umuhimu wa subira katika maisha yetu. Furahie! Ukitamani kujifunza kutoka kwa mwalimu Vinold, unaweza kumkuta kwa njia zifuatazo: Email - vinoldjohn@gmail.com Whatsapp - +255 756 704 834 Podcast - Bonga Language School Instagram - bonga_language_school

    Thu, 15 Aug 2024 - 56min
  • 5 - 4. Erick Mwasha | Kuishi Maisha ya Furaha

    Jiunge na mimi na Rafiki yangu Erick tukizungumzia masuala makubwa ya maisha kama vile umuhimu wa kuwasaidia watu wengine, changamoto za maisha katika Tanzania, na kuishi vizuri na wengine!

    Thu, 08 Aug 2024 - 1h 22min
  • 4 - 3. Fredrick Charles | Maana ya Maisha na Umuhimu wa Amri za Mungu na Mpango Wake

    Katika kipindi hiki, Fredi na mimi tulizungumzia maana ya maisha kidini na kijamii. Fredi ni rafiki yangu mpya hapa Tanzania. Yeye ni mtu mwema sana na ana mawazo mazuri mengi kushiriki. Anapenda Mungu sana na pia anafuatilia mambo ya siasa na mpira. Tuliongea kuhusu mpango wa Mungu na umuhimu wa kupenda wengine katika maisha yetu. Alisimulia matokeo machache ya maisha yake pia. Mfurahie!

    Fri, 19 Jul 2024 - 1h 18min
Afficher plus d'épisodes