Podcasts by Category
TCRA Tanzania

Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) is a statutory regulatory body responsible for regulating the electronic and postal communication sector in Tanzania. It was established under the Tanzania Communications Regulatory Authority Act, No.12 of 2003, which merged the Tanzania Communications Commission (TCC) and the Tanzania Broadcasting Commission (TBC).
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni taasisi iliyoasisiwa kwa mujibu wa sheria yenye wajibu wa kudhibiti sekta ya mawasiliano ya Kielektroni na Posta Tanzania. Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) namba 12 ya mwaka 2003, ambayo iliunganisha zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).
- 10 - Mawasiliano ni Fursa: Gari la Mtambo (Mobile Monitoring Radio Frequency Station)
Ungana nasi kufahamu juu ya kazi ya gari la mtambo wa usimamizi wa masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Unaweza kufuatilia kipindi cha Mawasiliano ni Fursa kupitia chaneli ya YouTube ya TCRA ili kufahamu kwa kina kuhusu majukumu ya gari hilo katika usimamizi wa huduma za mawasiliano nchini. TCRA inaendelea kutumia teknolojia na mifumo mbalimbali kusimamia sekta ya mawasiliano katika kuhakikisha ubora , usalama na upatikanaji wa huduma za mawasiliano. Kwa maoni na mapendekez...
Thu, 17 Jul 2025 - 9 - Matumizi ya Akili Unde (Artificial Intelligence) Katika Zama za Kidijiti
Fahamu Matumizi ya Akili Unde (AI) Katika Zama za Kidijiti” kupitia ufafanuzi uliotolewa na Mtaalamu wa Masuala ya Akili Unde (Artificial Intelligence - AI) na Mwanzilishi Mkuu wa Mfumo wa AI wa Ghala Bw. Kalebu Gwalugano katika mahojiano aliyofanya na TCRA Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!
Mon, 30 Jun 2025 - 8 - Dondoo za Kutambua Taarifa Feki Mtandaoni
TCRA imepata nafasi ya kujadiliana na Nuzulack Dausen, ambaye ni mwandishi wa habari mwenye tuzo nyingi kutoka Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Nukta Africa na Nukta Habari, akibobea katika ripoti za biashara, takwimu, na teknolojia. Yeye pia ni Mwandishi wa Thomson Reuters nchini Tanzania na mhadhiri wa Uandishi wa Habari za Takwimu na Fedha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambapo alipata Shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Umma. Hapa tutafahamu namna ya kutambua ta...
Mon, 09 Jun 2025 - 7 - Usimamizi wa Huduma za Posta Tanzania (Sehemu ya Pili)
Katika sehemu ya pili ya kipindi hiki cha huduma za posta, TCRA inatoa elimu kuhusu haki na wajibu wa mtoa huduma na mtumiaji wa huduma za posta nchini. Kipindi hiki hujadili pia anuani makazi (post codes) zinatotumika kutambulisha maeneo mbalimbali nchini Tanzania pamoja na matumizi yake katika huduma za mawasiliano ya posta. Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!
Mon, 26 May 2025 - 6 - Usimamizi wa Huduma za Posta Tanzania (Sehemu ya Kwanza)
TCRA inahakikisha uwapo wa huduma za posta zenye kuaminika, usalama, ufanisi na bei nafuu ndani ya Jamhuri ya Tanzania. Ungana nasi katika kipindi hiki kufahamu utaratibu na kanuni za utoaji wa huduma katika sekta ndogo ya Posta nchini Tanzania. Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!
Mon, 26 May 2025 - 5 - Uidhinishwaji wa Vifaa vya Mawasiliano ya Kielektroniki
TCRA huidhinisha vifaa vya Mawasiliano ya Kielektroniki kwa mujibu wa Sheria Kifungu Na. 83 (1) na (2) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta ya Mwaka 2010. Uidhinishwaji huo ni utaratibu maalum wa kuhakikisha kwamba Vifaa vya Mawasiliano ya Kielektroniki vinakidhi matakwa, mahitaji na viwango vya kitaifa na kimataifa kabla ya kuruhusu vifaa hivyo kuingia sokoni. Ungana nasi kufahamu zaidi kuhusu utaratibu, umuhimu na mlengwa wa utaratibu huu wa kuidhinisha vifaa...
Mon, 26 May 2025 - 4 - TCRA Zanzibar: Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano, Ofisi ya Zanzibar
Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 iliyoianzisha TCRA inaipa Mamlaka wajibu katika majukumu mbalimbali ikiwemo; kukuza ushindani bora na uchumi wenye tija; kulinda maslahi ya watumiaji; kulinda mitaji ya Watoa Huduma wenye ufanisi; kukuza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa watumiaji wote wakiwamo wenye kipato kidogo, walioko vijijini na watumiaji walio na walioko katika mazingira magumu; pamoja na kuimarisha Elimu kwa Umma, uelewa na ufahamu wa huduma zinazosimamiwa na TCRA. Meneja wa ...
Mon, 05 May 2025 - 3 - Taarifa ya Sekta ya Mawasiliano: Januari - Machi, 2025
Karibu katika wasaa wa kusikiliza ripoti hii inayowasilisha takwimu za sekta ya mawasiliano za robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025. Kwa ujumla, ripoti inatoa takwimu za mawasiliano ya simu, pesa mtandao kupitia simu za mkononi, intaneti, utangazaji, posta na usafirishaji wa vifurushi na vipeto. Takwimu hizi zimeandaliwa kwa kuzingatia viwango vya Shirika la Umoja wa Mawasiliano Duniani (ITU) vya kukusanya na kuandaa takwimu za huduma ya mawasiliano/TEHAMA. Kwa maoni na mapendekezo,...
Fri, 02 May 2025 - 2 - Wasichana katika TEHAMA, 2025: Mageuzi Jumuishi ya Kidijiti
Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA (International Girls in ICT Day) huadhimishwa kila Alhamisi ya nne ya mwezi Aprili kila mwaka. Hii inafuatia makubaliano ya nchi wanachama wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU), kuhimiza wasichana kupenda kusoma masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, kwa kifupisho cha kiingereza –STEM, yaani Science, Technology, Engineering and Mathematics. Nchi wanachama wa ITU pia zilikubaliana kuhamasisha Wasichana na Wanawake kushiriki kwe...
Fri, 02 May 2025 - 1 - Jamii Yetu: Zanzibar - Mawasiliano na Maendeleo ya Kilimo
Mawasiliano huleta faida mbalimbali katika maisha ya kila siku. Kipindi hiki kinaelezea yaliyojiri katika kilimo cha karafuu na namna mawasiliano huchochea kilimo hiki katika kisiwa cha Zanzibar. Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!
Mon, 03 Mar 2025
Podcasts similar to TCRA Tanzania
El Partidazo de COPE COPE
Herrera en COPE COPE
La Linterna COPE
Es la Mañana de Federico esRadio
La noche de Cuesta esRadio
Hondelatte Raconte Europe 1
Au Coeur du Crime Europe1
Affaires sensibles France Inter
LEGEND Guillaume Pley
El colegio invisible OndaCero
La Rosa de los Vientos OndaCero
Les grands dossiers de l'Histoire par Franck Ferrand Radio Classique
Espacio en blanco Radio Nacional
Enquêtes criminelles RTL
Entrez dans l'Histoire RTL
Le grand récit RTL
Les Grosses Têtes RTL
L'Heure Du Crime RTL
Parlons-nous RTL
El Larguero SER Podcast
SER Historia SER Podcast
Todo Concostrina SER Podcast
Un Libro Una Hora SER Podcast
HISTORIAS DE LA HISTORIA VIVA RADIO
TCRA Tanzania TCRA Tanzania
El Orden Mundial OndaCero
Scurt buletin de știri Parlamentul European
The Ugandan Podcast The Ugandan Podcast
दिनभर: पूरा दिन,पूरी ख़बर (Dinbhar) BBC Hindi Radio
Der livet leves KS
Season of Hope TWR
BFM Politique BFMTV
The Langley Files: CIA's Podcast Central Intelligence Agency