Filtrar por género

Jua Haki Zako

Jua Haki Zako

RFI Kiswahili

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

268 - Je haki za mtoto wa kiume unazifahamu, na je unafikiri zimekiukwa?
0:00 / 0:00
1x
  • 268 - Je haki za mtoto wa kiume unazifahamu, na je unafikiri zimekiukwa?

    Katika makala haya mtetezi wa haki za mtoto wa kiume Faith Maina Wanjiku, anasisitiza kwamba kampeini  za kumpa uwezo mtoto wa kike ndizo zimechangia kudidimia kwa hadhi ya mtoto wa kiume.

    Wajiku Maina raia kutoka nchini Kenya, anasema katika jamii ya leo hakuna anayeshughulikia haki na majukumu ya mtoto wa kiume, hali ambayo imechangia kizazi kizembe cha mtoto wa kiume.

     

    Skiza makala haya kufahamu suluhu kwa baadhi ya changamoto za mtoto wa kiume.

    Thu, 09 May 2024
  • 267 - Kenya : Polisi watuhumiwa kuwaua raia kiholela zaidi ya raia 118 wakiuawa mwaka 2023

     Makala haya tunaangazia ripoti ya mashirika ya kiraia nchini kenya kuhusu vifo vya kiholela vinavyodaiwa kutekelezwa na polisi.

    Ripoti hiyo inakaria kwa mwaka uliopita wa 2023, polisi waliwaua zaidi ya raia 118, masharika hayo yakisema licha ya mauwaji hayo ya raia hakuna hatua ambazo zimechukuliwa na serikali waathibu wahusika.

    Hata hivyo masharika hayo yanasema idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha  na mwaka 2022 ambapo zaidi ya watu 130, wanadaiwa kuuawa na polisi nchini Kenya.

    Mauwaji haya ya raia kwa mjibu wa masharika haya yanayojumuisha, shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International , tume ya haki za binadamu nchini Kenya , na masahrika mengine, ni kwamba yalitekelezwa wakati wa operesheni ya uhalifu.

     

    Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

    Thu, 02 May 2024
  • 266 - Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu

     Unamkumbuka  kiongozi wa wa dini Paul Mackenzi anayetuhumiwa kwa kushiwishi waumini wake kususia chakula hadi kufa, ili kukutana na yesu nchini Kenya.

    Baada ya takriban  mwaka moja na mwezi mmoja wa serikali ya Kenya kufukua miili ya waumini   waliofariki na kuzikwa katika msiku wa Shakahola na kuzifanyia uchuguzi wa vina saba yaani DNA, serikali sasa imeanza kutoa miili hiyo kwa familia za jamaa waliofariki.

    Serikali ya Kenya kupitia kwa mwanapatholijia wake mkuu daktari Johason Odour, imesema ilichukuwa muda mrefu kutoa miili kwa family zilizoathirika kutokana na kuharibika kupita kiasi.

    Soma piaWazee wauliwa pwani ya Kenya kwa tuhuma za kwamba ni wachawi

    Katika haya  mwanahabari Diana Wanyonyi kutoka pwani ya Kenya  alihudhuria mazishi ya baadhi ya waathiriwa wa mafunzo ya itikadi kali Paul Mackenzie na anasimulia hali ilivyokuwa 

    Thu, 25 Apr 2024
  • 265 - Haki ya watoto chotara shirika la African Futures Lab linataka Ubelgiji kuwatambua

    Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za binadamu la African Futures Lab, lenye makao yake jijini Brussels nchini Ubelgiji, lilizindua ripoti kushinikiza watoto chotara na mama zao kutoka nchini DRC, Rwanda na Burundi, kulipwa fidia, kutambuliwa kuwa raia wa Ubelgiji na kupata haki nyingine za msingi.

    Wakati wa ukoloni wa nchi ya Ubelgiji kwa nchi hizo za maziwa makuu, wakoloni, wanaume wazungu kutoka nchini Ubelgiji, waliwachukua kwa nguvu wanawake kutoka DRC, Rwanda na Burundi na kuwapeleka Ubelgiji na kuwazalisha, huku wengine wakifanyiwa hivyo wakiwa kwenye nchi zao.

    Makala haya yameandiliwa na Benson Wakoli

    Soma piaHaki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)

    Wed, 17 Apr 2024
  • 264 - Madaktari nchini Kenya wagoma kuishinikiza serikali kuzingatia haki zao

    Muungano wa madaktari, wauza dawa na madakrati wa meno, KMPDU, ambao unawakilisha zaidi ya wanachama 7,000 uliitisha mgomo Machi 15, ili kudai mishahara iliyocheleweshwa, pamoja na kupewa ajira mara moja kwa madaktari wanafunzi.Mgomo ambao umesababisha hali ya sintofahamu kwa wagonjwa kwa takribani wiki tatu sasa.

    Tue, 16 Apr 2024
Mostrar más episodios

Otros podcasts de Gobierno y Organizaciones