Podcasts by Category

Jua Haki Zako

Jua Haki Zako

RFI Kiswahili

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

266 - Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu
0:00 / 0:00
1x
  • 266 - Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu

     Unamkumbuka  kiongozi wa wa dini Paul Mackenzi anayetuhumiwa kwa kushiwishi waumini wake kususia chakula hadi kufa, ili kukutana na yesu nchini Kenya.

    Baada ya takriban  mwaka moja na mwezi mmoja wa serikali ya Kenya kufukua miili ya waumini   waliofariki na kuzikwa katika msiku wa Shakahola na kuzifanyia uchuguzi wa vina saba yaani DNA, serikali sasa imeanza kutoa miili hiyo kwa familia za jamaa waliofariki.

    Serikali ya Kenya kupitia kwa mwanapatholijia wake mkuu daktari Johason Odour, imesema ilichukuwa muda mrefu kutoa miili kwa family zilizoathirika kutokana na kuharibika kupita kiasi.

    Soma piaWazee wauliwa pwani ya Kenya kwa tuhuma za kwamba ni wachawi

    Katika haya  mwanahabari Diana Wanyonyi kutoka pwani ya Kenya  alihudhuria mazishi ya baadhi ya waathiriwa wa mafunzo ya itikadi kali Paul Mackenzie na anasimulia hali ilivyokuwa 

    Thu, 25 Apr 2024
  • 265 - Haki ya watoto chotara shirika la African Futures Lab linataka Ubelgiji kuwatambua

    Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za binadamu la African Futures Lab, lenye makao yake jijini Brussels nchini Ubelgiji, lilizindua ripoti kushinikiza watoto chotara na mama zao kutoka nchini DRC, Rwanda na Burundi, kulipwa fidia, kutambuliwa kuwa raia wa Ubelgiji na kupata haki nyingine za msingi.

    Wakati wa ukoloni wa nchi ya Ubelgiji kwa nchi hizo za maziwa makuu, wakoloni, wanaume wazungu kutoka nchini Ubelgiji, waliwachukua kwa nguvu wanawake kutoka DRC, Rwanda na Burundi na kuwapeleka Ubelgiji na kuwazalisha, huku wengine wakifanyiwa hivyo wakiwa kwenye nchi zao.

    Makala haya yameandiliwa na Benson Wakoli

    Soma piaHaki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)

    Wed, 17 Apr 2024
  • 264 - Madaktari nchini Kenya wagoma kuishinikiza serikali kuzingatia haki zao

    Muungano wa madaktari, wauza dawa na madakrati wa meno, KMPDU, ambao unawakilisha zaidi ya wanachama 7,000 uliitisha mgomo Machi 15, ili kudai mishahara iliyocheleweshwa, pamoja na kupewa ajira mara moja kwa madaktari wanafunzi.Mgomo ambao umesababisha hali ya sintofahamu kwa wagonjwa kwa takribani wiki tatu sasa.

    Tue, 16 Apr 2024
  • 263 - DRC : Jamii ya mbilikimo yalilia serikali kuwapa nafasi kuhudumu serikalini

    Nchini DRC , mara kwa mara jamii ya mbilikimo ama wambute kama wanavyo julikana katika taifa hilo, wamekuwa kilalamikia kile wanachodai  kubaguliwa na raia kutoka jamii ya wabantu nchini DRC.

    Jamii hiyo imekuwa ikidai wameachwa nje kwenue nyadhifa kama vile viongozi wa nyumba 10 hadi cheo cha rais, wanadai hakuna raia kutoka jamii hiyo anashikilia wadhifa wowote serikali.

    Moja ya mashirika za haki za binadamu kwa jina  " Greats lakes Human Right Programme" katika ripoti ya hivi karibuni , imesema kwamba sheria nzuri zipo za kuwalinda na kutetea haki za mbilikimo , ila utekelezaji wake ndio umekuwa changamoto.

    Mwandishi wetu wa Beni nchini DRC Eriksson Luhumbwe amezungumza na raia hao kutoka jamii ya mbilikimo na kutuandalia ripoti hii, skiza.

    Wed, 10 Apr 2024
  • 262 - Haki za raia wa mataifa ya Afrika wanaofanya kazi katika mataifa ya ughaibuni.

    Raia wa mataifa tofauti tofauti ya Afrika ikiwemo Kenya na Uganda huelekea katika mataifa ya kiarabu kutafta ajira Kila mwaka . Changamoto nyingi zikiripotiwa.Kwenye makala haya Florence amezungumza nao wakina dada wanaofanya kazi huko .

    Thu, 04 Apr 2024
Show More Episodes