Podcasts by Category

Changu Chako, Chako Changu

Changu Chako, Chako Changu

RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.

220 - Maoni ya washiriki katika kongamano la idhaa za kiswahili duniani sehemu ya mwisho
0:00 / 0:00
1x
  • 220 - Maoni ya washiriki katika kongamano la idhaa za kiswahili duniani sehemu ya mwisho

    Ni jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni, le parler francophone na Muziki, na leo tunahitimisha mlolongo wa Makala kuhusu kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika huko Mbeya, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni kutoka Alliance Francaise ya Arusha na Nairobi, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki King Kaka kutoka nchini Kenya.

    Sun, 21 Apr 2024
  • 219 - Sehemu ya tatu ya Makala kuhusu kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani

    Ni Jumapili nyingine tunakutana katika Makala Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, Utamaduni, le parler francophone na Muziki, leo ninakuletea mazungumzo kuhusu ubidhaishaji wa lugha ya kiswahili, ikiwa ni kauli mbiu ya kongamano la nne za idhaa za Kiswahili Duniani lililofanyika mkoani Mbeya Mwezi Machi. Na kwenye le parler francophone nitakuletea mradi wa Creation Afrika unaonadaliwa na Allliance francaise ya Nairobi

    Sun, 14 Apr 2024
  • 218 - Kongamano la idhaa za kiswahili duniani, umuhimu wa kujifunza lugha ya Kiswahili

    Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Msimamizi wa kituo cha radio China Kimataifa ambaye ni raia wa China kufahamu zaidi kwanini alivutiwa na swala la kujifunza lugha ya kiswahili, ni katika muktada wa kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika Mbeya nchini Tanzania. Kwenye Muziki utasikiliza wimbo wa mwanamuziki Lupman mwenye asili ya Burundi anaefanya kazi yake huko Sweeden.

    https://www.youtube.com/watch%3Fv%3DdsIZZ0MmadE

    Tue, 09 Apr 2024
  • 217 - Kongamano la nne la idhaa za kiswahili duniani "Tasnia ya habari na ubidhaishaji Kiswahili duniani"

    Karibu kuungana nami katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, Makala ambyo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sehemu ya kwanza ya mazungumzo kuhusu Kongomano la nne la idhaa za Kiswahili duniani. Kwenye le Parler francophone nitakueleza ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Idd Aziz kutoka nchini Kenya.

    Sun, 31 Mar 2024
  • 216 - Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya kifaransa sehemu ya pili

    Makala haya yameandaliwa na Florence Kiwuwa kwa ushirikiano na Ruben Lukumbuka.

    Mon, 25 Mar 2024
Show More Episodes