Podcasts by Category

Afrika Ya Mashariki

Afrika Ya Mashariki

RFI Kiswahili

Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.

124 - Ujumbe unaoandikwa kwenye vyombo vya usafiri katika mataifa ya Afrika
0:00 / 0:00
1x
  • 124 - Ujumbe unaoandikwa kwenye vyombo vya usafiri katika mataifa ya Afrika

    Je ujumbe unaoandikwa unahalisia na vitu vilivyowatokea makonda na madereva wa vyombo hivyo.

    Wed, 01 May 2024
  • 123 - Tanzania:Juhudi za wabunifu katika kupunguza hewa ya ukaa kutunza mazingira

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Masuala na Utalii, katika taarifa ya misitu na ufugaji nyuki inabainisha kuwa mkaa ni chanzo kikubwa cha nishati ya kaya katika maeneo ya mijini kwa kupikia na kupasha joto, kwa kuwa inachukuliwa kuwa ya bei nafuu na inapatikanakwaurahisi.

    Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya watu wote wa Tanzania kutegemea nishati ya majani. Nishati ya kupikia ndiyo inayoongoza kwa matumizi ya biomasi katika kaya ikilinganishwa na sekta nyingine kama vile ujenzi na kilimo sekta ya msingi.

    Thu, 18 Apr 2024
  • 122 - Fursa za uchumi wa buluu zilizopo katika  Ziwa Victoria

    Uchumi wa Buluu ni dhana pana yenye kubeba maana nzima ya kutumia kila rasilimali itokanayo na rasilimali maji kama Bahari, mito na maziwa.

    Dhana hii ubeba shuguli mbalimbli ikiwemo utalii, uvuvi, kilimo cha mwani, bandari pamoja na mafuta na gesi zilizomo baharini au katika maziwa.

    Kwa wakazi wa Jumuiya ya Afrika mashariki hasa katika mikoa inayo zunguka Ziwa.

    Victoria kwa siku za usoni wanachangamkua fursa za uchumi wa buluu uliopo katika maeneo yao.

    Dhana hii inatafsiriwa kwa kasi kwa siku za usoni na imekuwa ikitajwa kama ndio mharobaini wakuwanusua wananchi walio wengi kutoa katika mnyonyoro wa umasikini uliotopea.

    Sat, 13 Apr 2024
  • 121 - Magonjwa ya figo Afrika Mashariki

    Wagonjwa wengi barani Afrika wanahisi kuwa gharama ya matibabu ya figo ipo juu zaidi.

    Wed, 03 Apr 2024
  • 120 - Sehemu ya pili: Mradi wa kilimo unaofadhiliwa na AFD mjini Arusha

    Mradi wa kilimo endelevu unatanua mbawa zake sio tu katika kilimo bali pia kuwajengea uwezo wakulima kufanya shuguli za ufugaji.

    Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhiri wa shirika la maendeleo la Ufaransa AFD katika mkoa wa Arusha nchini Tanzania unakwenda mbali zaidi hadi kuwafikia wanamazingira.

    Mafuzo wanayopata wanasema yamekuwa chachu yakubadili Maisha yao kwani sasa wanamudu vyema kuwapatia Watoto wao elimu bora

    Sat, 30 Mar 2024
Show More Episodes