Filtrer par genre

Wimbi la Siasa

Wimbi la Siasa

RFI Kiswahili

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

248 - Kenya: Kwanini rais Ruto na mtangulizi wake wanatupiana maneno ?
0:00 / 0:00
1x
  • 248 - Kenya: Kwanini rais Ruto na mtangulizi wake wanatupiana maneno ?

    Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2027, vita vya maneno kati ya rais William Ruto na mtangulizi wake, Uhuru Kenya zimeshika kasi. Nini chanzo cha majibizano haya ? Victor Abuso anachambua hili kwa kina na Edwin Kegoli, mchambuzi wa siasa na masuala ya sera nchini Kenya.

    Wed, 23 Sep 2026
  • 247 - Hatima ya serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar

    Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, amezindua Kamati ya pamoja ya majadiliano kati ya chama chake CCM na kile cha upinzani ACT Wazalendo, katika kile kinachoashiria hatua mpya katika mchakato wa maridhiano ya kisiasa katika visiwa hivyo. Hatua hii inakuja baada ya vyama hivyo kusaini tamko la pamoja la makubaliano Julai tarehe 9 mwaka huu, ili kupata maridhiano ya kisiasa. Kwanini imechukua muda mrefu kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ? Tunachambua.

    Wed, 16 Sep 2026
  • 246 - Kenya yatoa siku 90 kwa wageni wasio na vibali halali kuvitafuta

    Serikali ya Kenya, imewatangazia raia wa kigeni wanaoishi nchini humo bila vibali vya kuishi au kufanya biashara, kuvitafuta ndani ya siku tisini.Hii inafuatia kauli ya rais William Ruto, wiki iliyopita, kuagiza operesheni dhidi ya wachuuzi wanaofanya biashara ndogo ndogo nchini humo. Je, hatua hii ya serikali ya Kenya inamaanisha nini na tishio ya utengamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ?

    Wed, 09 Sep 2026
  • 245 - Mpango wa rais Tshisekedi kuhusu mazungumzo yatafanikiwa ?

    Mwishoni mwa mwezi wa Agosti, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, alitangaza mpango wa namna mazungumzo ya kitaifa yatakavyofanyika, kusaidia kuleta utulivu wa kisiasa nchini humo. Mazungumzo hayo yataanzia katika mikoa yote 26, kabla ya yale ya kitaifa kufanyika jijini Kinshasa. Makundi yenye silaha na waasi wa M23/AFC hawatoshiriki kwenye mazungumzo hayo. Je, mpango huu utafanikiwa ?

    Wed, 02 Sep 2026
  • 244 - DR Congo: Mvutano waendelea kuhusu mpango wa kuifanyia marekebisho katiba

    Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi Julai, iliidhinisha sheria tata ya kufanyika kwa kura ya maoni, ili kuifanyia  katiba mabadiliko baada ya kupitishwa na wabunge mwezi Juni. Hatua hii imewakera wapinzani wa rais Felix Tshisekedi, kutoka muungano wa C64 ambao wameitisha maandamano Septemba 15, baada ya kuchelewa kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa. 

    Tunachambua na mbunge Willy Mishiki kutoka upande wa rais Tshisekedi na Emery Damien Kalwira kutoka muungano wa upinzani wa  C64.

    Wed, 19 Aug 2026
Afficher plus d'épisodes

Autres podcasts de Actualités et Politique