Filtrar por gênero
- 248 - Kenya: Kwanini rais Ruto na mtangulizi wake wanatupiana maneno ?Wed, 23 Sep 2026
- 247 - Hatima ya serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar
Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, amezindua Kamati ya pamoja ya majadiliano kati ya chama chake CCM na kile cha upinzani ACT Wazalendo, katika kile kinachoashiria hatua mpya katika mchakato wa maridhiano ya kisiasa katika visiwa hivyo. Hatua hii inakuja baada ya vyama hivyo kusaini tamko la pamoja la makubaliano Julai tarehe 9 mwaka huu, ili kupata maridhiano ya kisiasa. Kwanini imechukua muda mrefu kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ? Tunachambua.
Wed, 16 Sep 2026 - 246 - Kenya yatoa siku 90 kwa wageni wasio na vibali halali kuvitafuta
Serikali ya Kenya, imewatangazia raia wa kigeni wanaoishi nchini humo bila vibali vya kuishi au kufanya biashara, kuvitafuta ndani ya siku tisini.Hii inafuatia kauli ya rais William Ruto, wiki iliyopita, kuagiza operesheni dhidi ya wachuuzi wanaofanya biashara ndogo ndogo nchini humo. Je, hatua hii ya serikali ya Kenya inamaanisha nini na tishio ya utengamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ?
Wed, 09 Sep 2026 - 245 - Mpango wa rais Tshisekedi kuhusu mazungumzo yatafanikiwa ?
Mwishoni mwa mwezi wa Agosti, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, alitangaza mpango wa namna mazungumzo ya kitaifa yatakavyofanyika, kusaidia kuleta utulivu wa kisiasa nchini humo. Mazungumzo hayo yataanzia katika mikoa yote 26, kabla ya yale ya kitaifa kufanyika jijini Kinshasa. Makundi yenye silaha na waasi wa M23/AFC hawatoshiriki kwenye mazungumzo hayo. Je, mpango huu utafanikiwa ?
Wed, 02 Sep 2026 - 244 - DR Congo: Mvutano waendelea kuhusu mpango wa kuifanyia marekebisho katiba
Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi Julai, iliidhinisha sheria tata ya kufanyika kwa kura ya maoni, ili kuifanyia katiba mabadiliko baada ya kupitishwa na wabunge mwezi Juni. Hatua hii imewakera wapinzani wa rais Felix Tshisekedi, kutoka muungano wa C64 ambao wameitisha maandamano Septemba 15, baada ya kuchelewa kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa.
Tunachambua na mbunge Willy Mishiki kutoka upande wa rais Tshisekedi na Emery Damien Kalwira kutoka muungano wa upinzani wa C64.
Wed, 19 Aug 2026 - 243 - Kwanini kampeni za mapema zimeanza nchini Kenya, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ?
Ni mwaka mmoja, kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya. Uchaguzi huo utafanyika tarehe 10 mwezi Agosti mwaka 2027. Wakenya watamchagua rais, Magavana, Maseneta, wabunge, wawakilishi wa kike na viongozi wa Wadi mbalimbali. Hata hivyo, joto la kampeni ya mapema, imeshaanza kushuhudiwa, hasa kwenye kinyanganyiro cha urais. Nini kimesababisha joto na kampeni za uchaguzi mkuu kuanza mapema nchini Kenya ? Tunachambua.
Wed, 12 Aug 2026 - 242 - Maridhiano ya kisiasa nchini Tanzania yatafanikiwa ?
Nchini Tanzania, maneno maridhiano na Katiba mpya, yameendelea kutawala vinywa vya wanasiasa na wananchi wa taifa hilo baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na vurugu wa Oktoba mwaka 2025. Hivi karibuni, rais Samia Suluhu Hassan alikutana nna viongozi wa vyama vya siasa na kutangaza mpango wa maridhiano na mchakato wa katiba mpya. Je, haya yanawezekana bila ushiriki wa chama cha upinzani CHADEMA, ambacho kiongozi wake Tundu Lissu, amezuiwa jela kwa sababu ya kesi ya uhaini ?
Wed, 05 Aug 2026 - 241 - Kenya: Je, Seneta Edwin Sifuna anataka kuwania urais 2027 ?
Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya 2027, nyota ya kisiasa ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna inaonekana kuanza kung'aa. Sifuna aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha ODM, sasa anaongoza vuguvugu linaloitwa Linda Mwananchi. Je, Sifuna ameanza kutembea kwenye viatu vya aliyekuwa kiongozi shupavu wa kisiasa, Marehemu Raila Odinga. Tunachambua.
Wed, 29 Jul 2026 - 240 - Je, mazungumzo ya kitaifa nchini DRC yatafanyika ?
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amekubali kuanzisha mazungumzo ya kitaifa kujadili mivutano ya kisiasa likiwemo suala la kuibadilisha katiba na changamoto za kiusalama mashariki mwa nchi hiyo. Tayari muungano wa maaskofu wa kanisa katoliki CENCO na ule wa makanisa ya Kiprotestanti, wameanza mashauriano na wadau mbalimbali kuhusu mchakato wa mazungumzo ya kitaifa. Je, mazungumzo hayo yatafanyika? Tunachambua na wanasiasa wa DRC.
Wed, 22 Jul 2026 - 239 - Kwanini vita vya Marekani na Iran vimeanza tena ?
Marekani na Iran zimeanza tena kushambuliana, na kuzua wasiwasi wa kuendelea kwa vita vilivyoanza mwezi Februari 2026. Mashambulizi haya yamelenga kudhibiti eneo la Bahari ya Hormuz, njia muhimu inayotumiwa na meli zinazosafirisha mafuta na gesi kuelekea katika maeneo mbalimbali ya dunia. Kwanini Marekani na Iran zimeanza tena kushamuliana na hii inamanisha nini ?
Wed, 15 Jul 2026 - 238 - Rais Ndayishimiye ataweza kuleta maridhiano kati ya upinzani na serikali nchini DRC ?
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, wiki hii amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani kutoka muungano wa C64 na viongozi wa Kanisa Katoliki na Kiprotestanti nchini DRC, wanaopinga mchakato wa marekebisho ya katiba unaoungwa mkono na rais Felix Tshisekedi. Je, rais Ndayishimiye, atafanikiwa kuleta maridhiano ?
Wed, 08 Jul 2026 - 237 - Kwanini vita vinaendelea mwaka mmoja baada ya DRC na Rwanda kutia saini ya mkataba wa amani ?
Vita vimeendelea kushuhudiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kati ya wanajeshi na waasi wa M23/AFC wanaotuhumiwa kuungwa mkono na Rwanda licha ya Kigali na Kinshasa, kutia saini mkataba wa kusitisha vita mwaka mmoja uliopita. Kwanini vita vinaendelea licha ya kuwepo kwa mkataba huu ? Tunachambua.
Wed, 01 Jul 2026 - 236 - Serikali nchini Uganda inatumia Mahakama kuwanyanyasa wapinzani ?
Nchini Uganda, mwanasiasa wa upinzani na Meya wa zamani wa jiji la Kampala Erias Lukwago anakabiliwa na mashtaka ya uhaini. Alikamatwa nyumbani kwake na wanajeshi kwa agizo la Mkuu wa Majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba na kuzuiwa kabla ya kufikishwa Mahakamani. Wiki hii, mwanasiasa mashuhuri na wakili wa Besigye Martha Karua kutoka nchini Kenya, alizuiwa kuingia nchini Uganda na kufukuzwa nchini humo, na sasa serikali ya Uganda imempiga marufuku kurejea nchini humo. Tunachambua.
Wed, 24 Jun 2026 - 235 - Kenya kuwalipa fidia waathiriwa wa maandamano ya kisiasa
Serikali ya Kenya, itaanza kuwalipa fidia watu karibu Elfu Mbili, walioathiriwa na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo kuuawa, kubakwa, kutoweka na kujeruhiwa wakati wa maandamano ya kisiasa yaliyotokea nchini humo kati ya mwaka 2017 hadi 2025. Tume ya taifa ya haki za binadamu nchini Kenya, katika ripoti yake, inasema imewatambua waathiriwa wote wanaopaswa kupokea fidia hiyo, ambayo itaigharimu serikali nchini humo, Dola za Marekani Milioni 15. Tunachambua.
Wed, 17 Jun 2026 - 234 - Vijana nchini Kenya wanavyotumia teknolijia kuhamasisha elimu ya kisiasa
Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2027, vijana nchini humo, wanakumbatia teknolojia kuwafikia vijana wengi hasa wale wa rika la Gen Z, kujiandikisha kama wapiga kura na kuwania nyadhifa mbalimbali za uongozi. Je, hatua hii inaweza kuleta mwamko mpya wa kisiasa nchini Kenya ? Mwanahabari wetu Benson Wakoli alikutana na kuzungumza na vijana hao.
Wed, 10 Jun 2026 - 233 - DR Congo: Wanasiasa wachuana kuhusu mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kumeundwa miungano miwili ya kisiasa. Kundi la kwanza linaitwa "C4" linalounga mkono mabadiliko ya katiba, chini ya rais Felix Tshisekedi. Nao vigogo wa upinzani wakiongozwa na Martin Fayulu, Moïse Katumbi na wengine, wao wameunda C64" vuguvugu linalopinga marekebisho yoyote na kuilinda katiba ya sasa. Nini hatima ya makundi haya ? Tunachambua.
Wed, 03 Jun 2026 - 232 - Kwanini kampeni za mapema zimeanza nchini Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027?
Siasa za kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, zimeanza kupamba moto nchini Kenya, mwaka mmoja kabla ya wananchi kupiga kura. Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amejitokeza waziwazi na kumkosoa mrithi wake William Ruto kwa namna anavyoongoza serikali. Ruto na washirika wake, wanamtaka Uhuru kuachana na siasa. Tunachambua kauli za viongozi hao wa kisiasa.
Thu, 28 May 2026 - 231 - Sheria mpya nchini Uganda yalenga vyama vya siasa vya upinzani
Nchini Uganda, rais Yoweri Museveni ambaye aliapishwa Mei tarehe 12 kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano baada ya kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40, ametia saini mswada tata unaolenga kudhibiti ushawishi wa kigeni nchini humo kuwa sheria. Ukiukwaji wa sheria hii mpya, adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 10 jela, kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuendeleza maslahi ya kigeni dhidi ya taifa la Uganda.
Wed, 20 May 2026 - 230 - Kwanini suala la siasa na usalama, halikupewa nafasi kubwa kwenye mkutano wa Afrika na Ufaransa ?
Mkutano wa siku mbili kati ya Ufaransa na mataifa ya Afrika, uliofanyika jijini Nairobi nchini Kenya kati ya Mei 11 hadi 12, haukutoa kipaumbele suala la siasa na usalama katika mataifa ya Afrika, wakati huu nchi kama DRC, Sudan na yale ya ukanda wa Sahel kama Mali, Niger na Burkina Faso yakishuhudia changamoto kubwa ya kiusalama. Tunachambua kwa kina.
Thu, 14 May 2026 - 229 - Mpango wa DRC kuwakubali wahamiaji waliofukuzwa Marekani kwazua mjadalaWed, 06 May 2026
- 228 - Tanzania: Ripoti ya Tume imejibu maswali magumu kuhusu ukweli wa Oktoba 29 ?
Nchini Tanzania Aprili tarehe 23, tume iliyoundwa kuchunguza matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka 2025, ilitoa ripoti yake. Kwa mujibu wa tume hiyo, watu zaidi ya 500 walipoteza maisha, maelfu walijeruhiwa huku uharibifu wa mali wenye zaidi ya thamani ya Shilingi za nchi hiyo Bilioni 125. Je, ripoti hii imejibu maswali magumu kuhusu ukweli wa kilichotokea nchini Tanzania ? Tunachambua.
Wed, 29 Apr 2026 - 227 - Kwanini Ruben Kigame, anataka kuwa rais wa Kenya 2027 ?
Uchaguzi Mkuu nchini Kenya ni mwezi Agosti mwaka 2027, lakini wanasiasa mbalimbali wameanza kuonesha nia ya kugombea kiti cha urais. Miongoni mwao ni Ruben Kigame, mwanasiasa, mwanaharakati, mhadhiri, mwandishi wa Habari na mwanamuziki maarufu wa nyimbo za Injili. Yeye ni mlemavu wa Macho, ameamua kujitosa uwanjani, kutafuta uongozi wa nchi ya Kenya. Nini kimemsukuma ? Wiki hii anazungumza na mwenzangu, Benson Wakoli.
Wed, 22 Apr 2026 - 226 - Mazungumzo mapya kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya DRC nchini Uswizi
Awamu ya tisa ya mazungumzo ya amani kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yalianza siku ya Jumatatu Aprili 13 nchini Uswizi. Ujumbe wa Qatar ambao ni wasuluhishi, akiwemo mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika Massad Boulos, wanashiriki. Nini Ajenda ya mazungumzo haya ? Raia wa DRC wategeme nini ? Tunachambua.
Wed, 15 Apr 2026 - 225 - Harakati za watetezi wa haki za binadamu Mashariki mwa DRC
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yakiongozwa na Amnesty International, katika ripoti zao, yamekuwa yakionya kuwa maisha ya wanaharakati wa haki za binadamu, wana habari na viongozi wa mashirika ya kiraia yapo hatarini katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23, Mashariki mwa DRC. Wiki hii Ruben Lukumbuka, anazungumza na Jack Sinzaera, mwanaharakati maarufu kutoka Kivu Kaskazini.
Wed, 08 Apr 2026
Podcasts semelhantes a Wimbi la Siasa
El Partidazo de COPE COPE
Herrera en COPE COPE
La Linterna COPE
Es la Mañana de Federico esRadio
La noche de Cuesta esRadio
Hondelatte Raconte Europe 1
Au Coeur du Crime Europe1
Affaires sensibles France Inter
LEGEND Guillaume Pley
El colegio invisible OndaCero
La Rosa de los Vientos OndaCero
Les grands dossiers de l'Histoire par Franck Ferrand Radio Classique
Espacio en blanco Radio Nacional
Enquêtes criminelles RTL
Entrez dans l'Histoire RTL
Le grand récit RTL
Les Grosses Têtes RTL
L'Heure Du Crime RTL
Parlons-nous RTL
El Larguero SER Podcast
SER Historia SER Podcast
Todo Concostrina SER Podcast
Un Libro Una Hora SER Podcast
HISTORIAS DE LA HISTORIA VIVA RADIO
