Filtrer par genre
Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu
- 492 - Ni, Kwanini Wakatoliki tunapokea Mwili wa Kristo katika Umbo la Mkate tuu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Peter Mjwauzi, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kwanini sisi Wakatoliki tunapokea mwili wa Kristo katika umbo la Mkate tuu na wakati wa Sala ya Ekaristi Padre anasema twaeni mnywe wote?
Mon, 29 Apr 2024 - 28min - 491 - Je, wafahamu mambo gani ya kufanya unapoingia Kanisani ?
Karibu katika Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Frateri Elikana Nyagabona, anajibu swali lililoulizwa naomba kujua ninapoingia Kanisani ni mambo gani natakiwa kufanya hadi inapoisha Misa Takatifu?
Mon, 29 Apr 2024 - 27min - 490 - Je, Wafahamu Mashirika yanayotumia neno Bruda?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Faxon Polycarp Mpili, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali linalojibiwa linasema neno Bruda lina maana gani? ni mashirika gani wanatumia neno bruda, na kazi zao ni zipi katika kanisa.
Mon, 29 Apr 2024 - 19min - 489 - Je, Wafahamu vipindi vya Litrujia katika Kanisa Katoliki?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateli Baltazar Bao, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Tunaomba kuelezwa kuhusu vipindi vya kilitrujia katika Kanisa Katoliki maana tumekuwa tukisikia wanasema sasa ni kipindi cha Krismas, mara Majilio mara Pasaka, kiukweli hatuelewi maana yake pia mpangilio […]
Mon, 29 Apr 2024 - 26min - 488 - Je, Wafahamu Siri ya Miaka 28 ya Radio Maria Tanzania kwa Wanautume wake?
Uinjilishaji ni wajibu wa kila Mkristo Mbazitwa, Radio Maria Tanzania inarahisisha kazi hiyo ya Uinjilishaji kupitia vipindi vyake Mbalimbali Katika miaka 28 ya Radio Maria Tanzania, karibu uwasikilize Wanautume wa Radio Maria Tanzania wakielezea Utume huu Miaka 28 iliyopita kupitia Makala hii iliyotayarishwa na Agatha Kisimba.
Fri, 26 Apr 2024 - 54min - 487 - Miaka 28 ya Utume wa Radio Maria nchini Tanzania
Karibu usikilize Makala maalumu ya Miaka 28 ya Uinjilishaji wa Radio Maria Tanzania Katika makala hii , Rais wa Radio Maria Tanzania Ndugu Humphrey Julius Kira, amezungumzia Miaka 28 ya Radio Maria Tanzania tangu kuanzishwa kwake Aprili 26,1996 na pia ameelezea kwa undani namna Taasisi hii ilivyokuwa na kuenea kwa wigo wa Matangazo hapa nchini […]
Fri, 26 Apr 2024 - 58min - 486 - Fahamu dalili za wito wa maisha ya wakfu.
Ungana na Fredy William katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, ambapo Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania, anazungumzia juu ya dalili za wito wa maisha ya wakfu.
Fri, 26 Apr 2024 - 53min - 485 - Fahamu dalili au cheche za wito.
Karibu Ungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania, Mada ni muendelezo wa dalili au cheche za wito.
Fri, 26 Apr 2024 - 56min - 484 - Je, ni kweli Makadinari wa Afrika hawachaguliwi kuwa Mapapa?
Karibu katika Kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu la Songea, Frateri Noah Mwamfupe anajibu swali lililoulizwa, Kwanini Makadinari wa Afrika hawachaguliwi kuwa Mapapa?
Wed, 24 Apr 2024 - 24min - 483 - Je, Wafahamu kwanini Wakristo husherekea Sikukuu ya Pasaka?
Karibu Uungane na Elizabeth Masanja katika Kipindi cha Utume wa Walei, Mada inayozungumziwa ni juu muendelezo kwanini tunasherekea Pasaka, Mwezeshaji Ndugu Luuteliko Ubelo kutoka kamati ya Uinjilishaji kutoka Utume wa Walei Jimbo kuu la Dar es salaam.
Wed, 24 Apr 2024 - 42min - 482 - Fahamu barua za kitume za Baba Mtakatifu Yohane Paulo II.
Ungana na Joyce Jonatus katika Kipindi cha Mtaguso Mkuu wa Vatcan, ambapo Padre Richard Matanda Tesha kutoka Jimbo Katoliki Moshi, anazungumzia juu ya Barua za kitume za Baba Mtakatifu Yohane Paulo II.
Wed, 24 Apr 2024 - 49min - 481 - Je, Wafahamu Utaratibu Wakusoma Masomo Kanisani?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateli Ezekieli Ngimba, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kwanini Masomo Kanisani katika maandiko matakatifu yanasomwa vipande vipande, Je yale yasiyosomwa hayafai?
Wed, 24 Apr 2024 - 24min - 480 - Ni, kwa namna gani Mapaji ya Roho Mtakatifu yanafanya kazi katika Utashi wetu? (Sehemu ya pili)
Karibu ungane nami Elizabeth Masanja, katika kipindi cha Roho Mtakatifu na Kanisa leo tupo Askofu Mkuu Mstaafu Josaphat Louis Lebulu wa Jimbo Katoliki Arusha ikiwa ni muendelezo wa kipindi cha Mapaji ya Roho Mtakatifu yanavyofanya kazi katika utashi wetu.
Wed, 24 Apr 2024 - 51min - 479 - Yafahamu mafundisho ya Kanisa juu ya vidhibiti mimba.
Karibu usikilize Kipindi cha Pro Life utetezi wa uhai, ambacho hukujia kila siku ya Jumanne Saa 8:00-8:55 mchana na kurudiwa Saa 4:00 usiku. Katika Kipindi hiki, Wakufunzi kutoka Pro Life Tanzania, wameendelea kudadavua mada ihusuyo “Maisha ya vijana na dunia ya leo, mada ndogo ya mafundisho ya Kanisa juu ya vidhibiti mimba”. Mtangazaji ni Agatha […]
Tue, 23 Apr 2024 - 57min - 478 - Je, Wafahamu Sadaka ya Melkisedeki?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateli Michael Mangazini, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Padre anapoadhimisha sadaka la Misa Takatifu katika Sala ya Ekaristi husali akisema uipokee Sadaka hii safi na Takatifu isiyo na doa aliyokutolea Melkisedeki kuhani wako mkuu ‘ Naomba […]
Mon, 22 Apr 2024 - 28min - 477 - Je, nini maana ya neno Parokia katika Kanisa katoliki?
Ungana na Mhashamu Method Kilaini, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba katika muendelezo wa kipindi cha Historia ya Kanisa Maswali na majibu kutokana na mada mbalimbali zilizowasilishwa katika vipindi vya nyuma.
Mon, 22 Apr 2024 - 49min - 476 - Je, Marehemu akifanyiwa maombi anaweza kusamehewa dhambi zake pasipo yeye kutubu kabla ya kifo chake?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateli Caspary Nyiihwil, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Ni halali kufanya ibada ya wafu na Je marehemu akifanyiwa maombi anaweza kusamehewa dhambi zake pasipo yeye kutubu kabla ya kifo chake?
Mon, 22 Apr 2024 - 23min - 475 - Je, wafahamu maana ya Usizitazame Dhambi zetu ila tu Imani ya Kanisa lako?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateli Michael Paul Magazini, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema baada ya kusali Baba yetu padre hutamka maneno haya usizitazame Dhambi zetu ila tu Imani ya Kanisa lako, Je Mungu anangalia Dhambi zetu?
Mon, 22 Apr 2024 - 21min - 474 - Je, wafahamu visababishi vya Uraibu?
Karibu Ungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Uraibu na Padri Richard Matanda Tesha kutoka Jimbo Katoliki Moshi, akizungumzia vyanzo vya Uraibu.
Fri, 19 Apr 2024 - 50min - 473 - Nini Maana ya Sifa anazopewa Bikira Maria kupitia Litania ya Bikira Maria?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateli Zakaria Simkonda, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema katika Litania ya Bikira Maria nini maana ya Sifa anazopewa Mama Bikira Maria Mfano nyumba ya dhahabu, Sanduku la agano, waridi lenye fumbo na Mnara wa Daudi.
Fri, 19 Apr 2024 - 27min - 472 - Fahamu Faida za Kuitikia Wito Mtakatifu.
Ungana nami Happiness Mlewa, katika Kipindi Katekisimu Katoliki Shirikishi, mada inayozungumziwa ni Faida za Kuitikia Wito Mtakatifu , Mwezeshaji Padre Deodatus Kagashe Katunzi, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja kut0ka Mkoa wa Kagera.
Fri, 19 Apr 2024 - 56min - 471 - Sikiliza ufafanuzi wa Padre Amigu kuhusu Daraja ya Upadre.
Karibu usikilize Kipindi cha Ujumbe wa Biblia na Padre Tutus Amigu Mtaalamu wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Jimbo Kuu la Mwanza, ambapo katika Kipindi hiki anaendelea kufafanua juu ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ya Upadre, katika mada Kuu ya “kukoseana na kusameheana”. Mtangazaji ni Agatha Kisimba.
Wed, 24 Apr 2024 - 51min - 470 - Fahamu namna ya kuzibiti Usalama wa Mitandao.
Ungana na Mtangazaji Erick Paschal katika Kipindi cha Elimu Jamii, Mada inayozungumziwa ni Muendelezo mwa mada ya Usalama Mtandaoni, Wawezeshaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, Robin Lukae Afisa wa Mawasiliano kutoka TCRA, Alfa Wawa Afisa Uhusiano kutoka TCRA pamoja na Bi. Consolata William Afisa Mawasiliano kutoka TCRA.
Wed, 17 Apr 2024 - 45min - 469 - Fahamu Maisha ya Vijana katika Dunia ya leo.
Ungana na Mtangazaji Eliza Masanja katika Kipindi cha Pro-Life, mada inayozungumzwa ni Maisha ya Vijana katika Dunia ya leo, Wawezeshaji Wakufuinzi kutoka Pro-Life.
Wed, 17 Apr 2024 - 50min - 468 - Je, Wafahamu Vikwanzo Katika kuitikia Wito?
Ungana na Mtangazaji Fredy William katika Kipindi Katekisimu Katoliki Shirikishi, mada inayozungumziwa ni juu ya vikwazo katika Wito, Mwezeshaji Padre Deodatus Kagashe Katunzi, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja kutoka Mkoa wa Kagera.
Wed, 17 Apr 2024 - 56min - 467 - Fahamu namna ya kupata Wito na Mang’amuzi yake.
Ungana na Mtangazaji Happiness Mlewa katika Kipindi Katekisimu Katoliki Shirikishi, mada inayozungumziwa ni juu ya mang’amuzi ya Wito, Mwezeshaji Padre Deodatus Kagashe Katunzi, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radaio Mabiu Sauti ya Faraja ktuoka Mkoa wa Kagera.
Wed, 17 Apr 2024 - 52min - 466 - Je, unafahamu vitu gani unatakiwa ule nyakati za Sherehe mbalimbali katika Jamii
Ungana na Mtangazji Agatha Kasimba katika kipindi cha Chakula na Lishe, Mwezeshaji Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka Tasisi ya Chakula na Lishe Tanzanzania TFS, Bi Adelini Mnuo, mada inayozungumziwa, Ulaji unao shauliwa nyakati za Sherehe .
Wed, 17 Apr 2024 - 52min - 465 - Fahamu Maana na Thamani ya Kufanya Nadhiri.
Ungana na Padre Dkt.Clement Kihiyo, Mkuu wa Idara ya Liturujia Baraza la Maaskofu Tanzania[TEC] akizungumzia Ibada ya Kuweka Nadhiri za Kitawa
Wed, 17 Apr 2024 - 49min - 464 - Nini Maana ya Sala ya Bwana?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Samson Mahinya, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema, Je Sala ya Baba yetu tunayoisali kila siku ipo kwenywe Bibilia Takatifu?
Wed, 17 Apr 2024 - 28min - 463 - Amka na Mama Dominika ya Pasaka[Sehemu ya kumi na Moja]
L'articolo Amka na Mama Dominika ya Pasaka[Sehemu ya kumi na Moja] proviene da Radio Maria.
Wed, 17 Apr 2024 - 52min - 462 - Nini Maana ya Wito?
Ungana na Mtangazaji wako Martin Joseph katika kipindi cha Fahamu Wito wako kupitia Radio Maria Tanzania ambapo tuko naye Padre Innocent Bahati Mushi, OFMCap akizungumzia nini maana ya Wito?
Tue, 16 Apr 2024 - 53min - 461 - Amka na Mama Dominika ya pili Pasaka[ Sehemu ya Kumi]
L'articolo Amka na Mama Dominika ya pili Pasaka[ Sehemu ya Kumi] proviene da Radio Maria.
Tue, 16 Apr 2024 - 55min - 460 - Fahamu Utofauti kati ya Sikukuu ya Pasaka na Sikukuu ya Vibanda.
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateli Jackob Venusto Mkandawile, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Misikilizaji linalojibiwa linasema Je kwa Wayahudi kulikua na tofauti kati ya Sikukuu ya Pasaka na Sikukuu ya vibanda.
Tue, 16 Apr 2024 - 25min - 459 - Je, Wafahamu Fadhila za Kimungu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Hugo Venance, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema, Tunaomba ufafanuzi juu ya Fadhila kuu tatu za kimungu , yaani Imani, Matumaini na Mapendo
Mon, 15 Apr 2024 - 23min - 458 - Askofu Minde” Mwanga wa Kwanza wa mbali wa Wokovu wa Siku”
Karibu katika kipindi cha Nena nami Bwana ambapo anayenena nasi ni Mhashamu Ludovick Minde, Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi
Mon, 15 Apr 2024 - 55min - 457 - Nini Maana ya INRI?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Faxon Polycarp Mpili, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema, Juu ya Msalaba wa Yesu yameandikwa Maneno haya INRI maneno hayo yanamaana gani?
Mon, 15 Apr 2024 - 23min - 456 - Je, ni dhambi kwa Mkristo kutumia dawa za mitishamba?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateli Jackob Venusto Mkandawile, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Misikilizaji linalojibiwa linasema Je ni dhambi kwa Mkristo kutumia dawa za mitishamba.
Mon, 15 Apr 2024 - 27min - 455 - Fahamu waraka wa Baba Mtakatifu Yohane xxiii, Kanisa ni Mama na mwalimu.
Karibu katika kipindi cha Mtaguso Mkuu wa Vatcan na Padre Richard Matanda Tesha kutoka Parokia ya Mtakatifu Thomas Mtume Mrao Rombo Jimbo Katoliki Moshi, anazungumzia waraka wa Baba Mtakatifu Yohane xxiii, Kanisa ni Mama na mwalimu.
Fri, 12 Apr 2024 - 50min - 454 - Fahamu waraka wa Baba Mtakatifu Yohane Paulo ii kwa vijana.
Karibu katika kipindi cha Mtaguso Mkuu wa Vatcan, Muwezeshaji ni Padre Richard Matanda Tesha kutoka Parokia ya Mtakatifu Thomas Mtume Mrao Rombo Jimbo katoliki Moshi, anazungumzia juu ya Waraka wa Baba Mtakatifu Yohane Paulo ii kwa vijana.
Fri, 12 Apr 2024 - 55min - 453 - Je, wafahamu Salamu ya Matumaini?
Karibu Ungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania, akizungumzia Salamu ya Matumaini
Fri, 12 Apr 2024 - 50min - 452 - Fahamu Mateso katika Furaha ya Pasaka[Sehemu ya Pili]
Karibu Ungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania, ambapo ni muendelezo wa mada Mateso katika Furaha ya Pasaka
Fri, 12 Apr 2024 - 54min - 451 - Ni, kwanini Bibilia imekataza Wanawake kuongoza ibada mbalimbali Kanisani?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Caspary Moses Nyihwili, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema, mbona Makatekista Wakike wanaongoza ibada mbalimbali Kanisani, wakati Bibilia imekataza Wanawake kuongoza ibada yeyeto ile katika 1Wakorintho 14; 34-35?
Fri, 12 Apr 2024 - 20min - 450 - Je, Wafahamu namna ya kuepuka ajari za Barabarani.
Ungana na Mtangazaji Happiness Mlewa Katika Kipindi cha Usalama wa Barabarani, mada inayozungumziwa ni ajari za Barabarani , koplo Silvesta Mahumba kutoka Trafiki Makao Makau kitengo cha Dawati la Elimu.
Wed, 17 Apr 2024 - 52min - 449 - Fahamu namna ya kubaini ubora na usalama wa Dawa.
Karibu ungane na Ester Magai katika kipindi cha Ijue Afya Yako, Muwezeshaji wetu ni Nelson Nyenza, Mtekilojia wa Dawa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Fransisko Ifakara, leo anazungumzia juu ya namna ya kubaini ubora na usalama wa Dawa.
Fri, 12 Apr 2024 - 49min - 448 - Je, Mtu anaweza kushukiwa na Roho Mtakatifu na akanena kwa lugha?
Ungana nami Mhashamu Method Kilaini, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba katika muendelezo wa kipindi Historia ya Kanisa Maswali na majibu kutokana na mada mbalimbali zilizowasilishwa katika vipindi vya nyuma.
Thu, 11 Apr 2024 - 57min - 447 - Kwanini tunatumia matawi ya mitende siku ya Dominika ya matawi?
Frateri Cassian Lebba wa Jimbo Katoliki Sumbawanga anayefanya utume wake wa mwaka wa kichungaji katika Seminari Ndogo ya Mtakatifu Yosefu Kaengesa yuko pamoja nasi kutupitisha kwa kina na kwa ufafanuzi uliojitosheleza kutokana na swali la Msikilizaji linalosema Kwanini tunatumia matawi ya mitende siku ya Dominika ya matawi?
Thu, 11 Apr 2024 - 26min - 446 - Kwanini Padre/Askofu anatumia Chetezo & Ubani awapo Altareni?
Karibu katika kipindi cha Historia ya Kanisa na Mhashamu Method Kilaini, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba ambapo ni muendelezo wa kipindi cha Maswali na majibu kutokana na mada mbalimbali zilizowasilishwa katika vipindi vya nyuma.
Thu, 11 Apr 2024 - 56min - 445 - Askofu Musomba: “Kutangaza Ufufuko wa Kristo sio kitu Binafsi sio kitu cha kuweka uvunguni”
Karibu katika kipindi cha Nena nami Bwana ambapo anayenena nasi ni Mhashamu Stephano Lameck Musomba, OSA Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Thu, 11 Apr 2024 - 51min - 444 - Ifahamu Liturujia katika kipindi cha Pasaka & Siku 50 za Maadhimisho ya Pasaka.
Ungana na Padre Dkt.Clement Kihiyo, Mkuu wa Idara ya Litrujia Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) akituongoza kuangazia Litrujia katika kipindi cha Pasaka & Siku 50 za Maadhimisho ya Pasaka.
Thu, 11 Apr 2024 - 53min - 443 - Je, ni halali Mkristo kunywa mvinyo kwa kiasi kidogo?
Karibu katika kipindi cha Historia ya Kanisa na Mhashamu Method Kilaini, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba ambapo ni muendelezo wa kipindi cha Maswali na majibu kutokana na mada mbalimbali zilizowasilishwa katika vipindi vya nyuma.
Thu, 11 Apr 2024 - 57min - 442 - Je, Wafahamu Utofauti wa Sadaka ya Yesu Kristo na Sadaka ya Wayahudi?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Cassian Lebba, Kutoka Seminari ndogo ya Kaengesa Jimbo Katoliki Sumbawanga swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Je kuna Mahusiano gani kati ya Sadaka ya Yesu Kristo na Sadaka ya Wayahudi?
Wed, 10 Apr 2024 - 28min - 441 - Je, Wafahamu Mateso katika Furaha ya Pasaka?
Karibu Ungane nami Fredy William, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania, akizungumzia juu ya Mateso katika Furaha ya Pasaka
Wed, 10 Apr 2024 - 57min - 440 - Nini Maana ya Katekisimu Katoliki na aina za Katekisimu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Daudi Fungameza, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema nini maana ya Katekisimu Katoliki na aina za Katekisimu?
Mon, 08 Apr 2024 - 24min - 439 - Zifahamu Sheria za Sakramenti ya Kipaimara[Sehemu ya Pili]
Ungana nami John Samky katika kipindi cha Sheria za Kanisa na Padre Ladsilaus Mgaya, Mwanasheria wa Sheria za Kanisa kutoka Jimbo Katoliki Njombe ambapo ni muendelezo wa mada ya Sakramenti ya Kipaimara.
Mon, 08 Apr 2024 - 59min - 438 - Ni, kwanini Sikukuu ya Pasaka haina Tarehe maalumu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Bendict Lazaro Luvanga, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema, Tarehe 25 kila mwaka tunasherekea kuzaliwa kwa Yesu kristo kwanini Sikukuu ya Pasaka haina tarehe maalumu?
Mon, 08 Apr 2024 - 20min - 437 - Nini Maana ya Malipizi?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Ayuto Kongo, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema, Je mtu akiungama na asipofanya malipizi utaratibu ukoje?
Mon, 08 Apr 2024 - 27min - 436 - Fahamu juu ya mashangilio ya Pasaka.
Karibu Uungane na Mtangazaji Happiness Mlewa Katika Kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania, mada inayozungumziwa ni juu ya mashangilio ya Pasaka.
Fri, 05 Apr 2024 - 25min - 435 - Je, Wafahamu juu ya Tafakari ya Mwanga?
Karibu Uungane na Mtangazaji Happiness Mlewa Katika Kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania, mada inayozungumziwa ni juu ya Tafakari Mwanga.
Fri, 05 Apr 2024 - 40min - 434 - Fahamu Mateso Saba ya Yesu Msalabani.
Karibu Uungane na Mtangazaji Happiness Mlewa Katika Kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania, mada inayozungumziwa ni juu ya Mateso Saba Yesu Msalabani.
Fri, 05 Apr 2024 - 55min - 433 - Je, Ugumba ni Ugonjwa?
Karibu ungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Ijue Afya yako mwezeshaji ni Daktari Angello Nyamtema, kutoka H0spitali ya Rufaa Mtakatifu Francisco Ifakara, akizungumzia Ugumba.
Fri, 05 Apr 2024 - 46min - 432 - Je, Wafahamu Alama na Ishara za Ufufuko?
Ungana nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Katekisimu katoliki shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe Mkurugezi wa Radio Mbiu sauti ya Faraja Kagera, na Paroko wa Parokia Kaazi Jimbo Katoliki Bukoba ambapo ni muendelezo wa mada Alama na Ishara za Ufufuko
Fri, 05 Apr 2024 - 52min - 431 - Je, Sala za Masifu hufundishwa kwa Watawa tu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Daudi Fungameza, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema je sala za Masifu zinafundishwa kwa watawa tu?
Fri, 05 Apr 2024 - 29min - 430 - Tafakari ya Ijumaa Kuu.
Ungana na Happiness Mlewa katika Tafakari ya Ijumaa Kuu, inayoletwa kwako na Padre Dominic Mavula C.PP.S Mkurugenzi wa matangazo Radio Maria Tanzania.
Wed, 03 Apr 2024 - 44min - 429 - Zifahamu siku Tatu kuu za Pasaka.
Karibu ungane na Mtangazaji Happiness Mlewa katika kipindi cha Katekisimu katoliki Shirikishi mwezeshaji ni Padre Leonard Maliva Mkurugezi wa Utume wa Walei Jimbo Katoliki la Iringa ambae pia Paroko wa Parokia ya Isimani jimboni humo, mada inayozungumziwa ni muendelezo mwa Tafakari juu ya siku tatu kuu za Pasaka.
Wed, 03 Apr 2024 - 56min - 428 - Fahamu juu ya Alama na Ishara za Ufufuko.
Karibu ungane nami Erick Paschal katika kipindi cha Katekisimu katoliki shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe Mkurugezi wa Radio Mbiu sauti ya Faraja Kagera, na Paroko wa Parokia Kaazi Jimbo Katoliki Bukoba akizungumzia Alama na Ishara za Ufufuko.
Wed, 03 Apr 2024 - 51min - 427 - Je, Wafahamu namna ya Hitaji la Kuongozwa kupitia Ujumbe wa kwaresma kutoka TEC?.
Karibu Uungane na Mtangazaji Agatha Kasimba katika kipindi cha Utume wa Walei, mada inayozungumziwa ni juu ya Hitaji la kuongozwa kutoka Ujumbe wa Kwaresma uliotolewa na Balaza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC, Mwezeshaji Bi Rose Gerald Katibu kamati uinjilishaji kutoka Jimbo kuu la Dar es salaam.
Wed, 03 Apr 2024 - 56min - 426 - Fahamu maana ya Siku tatu kuu za Pasaka.
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Jackob Venusto Mkandawile, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema nini maana ya siku tatu kuu za Pasaka.
Wed, 03 Apr 2024 - 23min - 425 - Fahamu Udereva wa kujihami.
Karibu ungane nami Fredy William, katika kipindi cha Usalama Barabarani Studio tupo na Mkaguzi wa Polisi Dumu Mwalugenge na Staff Sergeant Aurelian Chuwa kutoka Makao Makuu ya Traffic, kitengo cha elimu, wakizungumzia juu ya Udereva wa kujihami na katazo la namba za 3D.
Wed, 03 Apr 2024 - 52min - 424 - Je, wafahamu maana ya Mti wa Msalaba?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Shemasi Paul Mbwelo, kutoka Kanisa kuu la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Amri ya Mungu inasema usichonge wala usiabudu sanamu, lakini padre ijumaa kuu husema huu ni mti wa msalaba Waamini huitikia njooni tuuabudu Inaonesha kuvunja amri ya Mungu.
Wed, 03 Apr 2024 - 19min - 423 - Kwanini Yesu alimwambia Mariam Magdalena usinishike, wakati huo Thomaso alimwambia leta mkono wako uutie ubavuni mwangu?
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, tukiungana na Frateri Daudi Fungameza kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu la Songea, na anajibu swali linalosema kwanini Yesu alimwambia Mariam Magdalena usinishike, wakati Thomaso alimwambia leta mkono wako uutie ubavuni mwangu?
Wed, 03 Apr 2024 - 26min - 422 - Fahamu maana ya Mshumaa wa Pasaka.
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu la Songea, leo Frateri Benedict Lazaro Luvanga anajibu swali lililoulizwa, nini maana ya Mshumaa wa Pasaka?
Wed, 03 Apr 2024 - 21min - 421 - Ifahamu Kwaresima na utetezi wa Uhai wa Binadamu.
Ungana na Agatha Kisimba katika kipindi cha Pro – Life na mada inayozungumziwa ni muendelezo wa mada ya Kwaresima na utetezi wa uhai wa Binadamu, wawezeshaji ni Janeth Akalo, Grace Shayo, Frida Mwanga na Witness Joachim wanautetezi wa uhai kutoka Pro – Life Tanzania.
Wed, 27 Mar 2024 - 48min - 420 - Ni, kwa namna gani Mapaji ya Roho Mtakatifu yanafanya kazi katika Utashi wetu?
Karibu ungane nami Elizabeth Masanja, katika kipindi cha Roho Mtakatifu na Kanisa leo tupo Askofu Mkuu Mstaafu Josaphat Louis Lebulu wa Jimbo Katoliki Arusha akifundisha juu ya Mapaji ya Roho Mtakatifu yanavyofanya kazi katika utashi wetu.
Wed, 27 Mar 2024 - 58min - 419 - Fahamu siku tatu kuu za Pasaka.
Karibu uungane nami Mtangazaji wako Happiness Mlewa katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, ambapo niko naye Padre Leonard Maliva, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga Isimani na Mkurugenzi wa Utume wa Walei Jimbo Katoliki Iringa, akizungumzia juu ya siku tatu kuu za Pasaka.
Wed, 27 Mar 2024 - 54min - 418 - Je, wafahamu maana ya kubusu Msalaba?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Caspary Moses Nyihwil, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema nini maana ya Kubusu Msalaba.
Wed, 27 Mar 2024 - 19min - 417 - Amka na Mama Dominika ya Matawi-Sehemu ya Tisa
L'articolo Amka na Mama Dominika ya Matawi-Sehemu ya Tisa proviene da Radio Maria.
Mon, 25 Mar 2024 - 52min - 416 - Ni kwanini Yesu alimwambia Mnyang`aji Dismas leo utakuwa pamoja nami Paradiso?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Balthazar Boa kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo kuu la Songea swali la Msikiizaji linalojibiwa linasema Yesu alipokuwa msalabani alimwambia Mnyang`aji Dismas, leo utakuwa pamoja nami peponi Je, hii siyo rushwa ? Na ni kwanini alimkubalia kabla hajamuondolea dhambi ?
Mon, 25 Mar 2024 - 21min - 415 - Ni kwanini katika mwanzo wa Ibada ya Ijumaa Kuu Padri hujilaza kifudifudi mbele ya Altare?
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani na Frateri Michael Mangazini, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu la Songea, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kwanini kwenye Ibada ya Ijumaa Kuu, Padri anayeongoza Ibada anajilaza kifudifudi mbele ya Altare.
Mon, 25 Mar 2024 - 25min - 414 - Kwanini Lugha chafu ni shinikizo la Marafiki katika Uraibu?
Karibu Ungane nami John Albert Samky, Katika kipindi cha Uraibu na Padri Richard Matanda Tesha, Kutoka Jimbo Katoliki Moshi leo tunajifunza Lugha chafu na shinikizo la Marafiki katika kufanya Uraibu.
Mon, 25 Mar 2024 - 53min - 413 - Unafahamu Kwanini Kanisa linaitwa Mama na wakati huo Mungu ni Baba?
Karibu katika Kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, ambapo majibu yanatolewa na Frateri Oscar Mwamoto kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu la Songea, akijibu swali linalosema kwanini Kanisa linaitwa Mama, wakati huo Mungu ni Baba. Je kuna uhusiano wowote hapo?
Fri, 22 Mar 2024 - 25min - 412 - Je, Kitubio kina Umuhimu sana wakati huu wa Kwaresima kuliko wakati mwingine?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Peter Peter, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kwanini wakati wa Kwaresima tunasisitizwa zaidi kufanya kitubio kuliko nyakati zingine.
Fri, 22 Mar 2024 - 25min - 411 - Je, wafahamu kipindi cha Kwaresima Mtu akiwa amefunga anaruhusiwa kupokea Ekaristi Takatifu.
Karibu katika Kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu la Songea, ambapo Frateri Felix Ulindula Kilasile, anajibu swali lililoulizwa kipindi cha Kwaresima Mtu akiwa amefunga anaruhusiwa kupokea Ekaristi Takatifu?
Fri, 22 Mar 2024 - 25min - 410 - Je, wafahamu Makosa yanayofanya na Wazungumzaji wa Kiswahili?
Ungana na Mtangazaji wako Tekla Revoctaus, katika kipindi cha Elimu Jamii Leo tupo na Msanifu Lugha Kusanja Emmanuel Kusanja, kutoka Baraza la Kiswahili Taifa [BAKITA] akizungumzia Makosa yanayofanya mara kwa mara na wazungumzaji wa Kiswahili.
Tue, 19 Mar 2024 - 44min - 409 - Ni kwanini wakristo hasa wakatoliki tunatumia Msalaba Kanisani kwaajili ya nini?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Oscar Mwamoto, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramihio Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Msalaba ulitumika na Yesu zama hizo na yeye hayupo tena msalabani .sasa kwanini wakristo hasa wakatoliki tunatumia Msalaba Kanisani ni kwaajili ya nini?
Tue, 19 Mar 2024 - 29min - 408 - Ni kwa namna gani mapaji ya Roho Mtakatifu yanakuwa na kukomaa nafsini mwetu?
Karibu ungane nami Tekla Revoctaus, katika kipindi cha Roho Mtakatifu na Kanisa leo tupo Askofu Mkuu Mstaafu Josaphat Louis Lebulu wa Jimbo Katoliki Arusha akizungumzia juu ya kukuwa na kukomaa kwa Mapaji ya Roho Mtakatifu nafsini mwetu.
Tue, 19 Mar 2024 - 54min - 407 - Amka na Mama Kwaresima-Sehemu ya Nane.
L'articolo Amka na Mama Kwaresima-Sehemu ya Nane. proviene da Radio Maria.
Tue, 19 Mar 2024 - 56min - 406 - Amka na Mama -Kwaresima Sehemu ya Saba
L'articolo Amka na Mama -Kwaresima Sehemu ya Saba proviene da Radio Maria.
Mon, 18 Mar 2024 - 53min - 405 - Je, Wafahamu namna ya kuzuia Matatizo ya Figo?
Karibu katika kipindi cha ijue Afya yako kupitia Radio Maria Tanzania ambapo leo tupo na Nesi Calista Kayombo, Mkuu wa Idara ya Figo Hospitali ya Rufaa Mtakatifu Francisco Ifakara, akizungumzia Afya ya Figo kwa wote.
Mon, 18 Mar 2024 - 49min - 404 - Ni, Kwanini Misalaba inafunikwa kipindi cha Kwaresima?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Elikana Nyagabona, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kwanini katika kipindi cha Kwaresima misalaba inafunikiwa .
Mon, 18 Mar 2024 - 24min - 403 - Fahamu Utaratibu wa Masomo ya Misa katika kipindi cha kawaida cha Mwaka -Sehemu ya Nne
Karibu Ungane nami Mtangazaji wako Tekla Revocatus katika kipindi cha Ijue Liturujia kupitia Radio Maria Tanzania Mwezeshaji wetu Padri Dkt.Clement Kihiyo, Katibu Mtendaji idara ya Liturujia Baraza la Maaskofu Tanzania [TEC] ikiwa ni muendelezo wa mada Utaratibu wa Masomo ya Misa katika kipindi cha kawaida katika Mwaka.
Mon, 18 Mar 2024 - 47min - 402 - Zifahamu Sheria za Sakramenti ya Kipaimara.
Karibu ungane na Mtangazaji John Samky katika Kipindi cha Sheria za Kanisa ambapo kwa namna ya pekee Padre Ladsilaus Mgaya, Mwanasheria wa Sheria za Kanisa kutoka Jimbo Katoliki Njombe akiwa anaangazia mada ya Sakramenti ya Kipaimara.
Mon, 18 Mar 2024 - 55min - 401 - Je, wafahamu utofauti kati ya Hekalu na Sinagogi?
Karibu katika Kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, majibu yanatolewa na Frater Maurus Zacharia Msigwa , akijibu swali linalouliza kuna utofauti gani Hekalu na Sinagogi.
Mon, 18 Mar 2024 - 25min - 400 - Itambue Huruma ya Mungu Kipindi cha Kwaresima.
Ungana nami Martin Joseph katika kipindi cha Fahamu Wito ambapo Padre Innocent Bahati Mushi, OFMCap anatuongoza kuangazia Huruma ya Mungu kipindi cha Kwaresima.
Fri, 15 Mar 2024 - 53min - 399 - Kwanini tunaambiwa funga Jumatano ya majivu na usile nyama siku ya Ijumaa kuu?
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu Katoliki Songea, ambapo swali linalojibiwa linalosema kuwa Kwanini tunaambiwa funga Jumatano ya majivu na usile nyama siku ya Ijumaa kuu? na majibu yanatolewa na Frateri Michael Paulo Mangazini.
Fri, 15 Mar 2024 - 25min - 398 - Je, Mtu anaokoka akiwa duniani au baada ya kifo?
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu Katoliki la Songea ambapo swali linalojibiwa linasema Je, Mtu anaokoka akiwa duniani au baada ya kifo? majibu ya swali hili yanatolewa na Fratel Felix Olindula.
Fri, 15 Mar 2024 - 24min - 397 - Rozari Takatifu Matendo ya Mwanga – Makao Makuu Mikocheni Dar es salaam
Karibu tusali sala ya Rozari Takatifu ya Fatima Matendo ya Mwanga tukiongozwa na baadhi ya Wanautume wa Radio Maria Makao Makuu Mikocheni Dar es salaam.
Fri, 15 Mar 2024 - 38min - 396 - Rozari Takatifu Matendo ya Uchungu – Makao Makuu ya Radio Maria Tanzania
Karibu tusali sala ya Rozari Takatifu ya Fatima Matendo ya Uchungu tukiongozwa na baadhi ya Wanautume wa Radio Maria Tanzania Makao Makuu Mikocheni Jimbo Kuu la Dar es salaam.
Fri, 15 Mar 2024 - 38min - 395 - Yafahamu madhara ya matumizi holela ya dawa.
Karibu katika kipindi cha Ijue Afya yako kupitia Radio Maria Tanzania ambapo leo tunaangazia madhara ya matumizi holela ya dawa.
Fri, 15 Mar 2024 - 54min - 394 - Rozari Takatifu ya Huruma ya Mungu – Kiabakari, Jimbo Katoliki Musoma.
Karibu tusali kwa pamoja sala ya Rozari Takatifu ya Huruma ya Mungu kutoka Parokia ya Kiabakari, Jimbo Katoliki Musoma sala hii inaongozwa na Padre Wojciech Adam, Mhifadhi wa Huruma ya Mungu katika kituo cha Kiabakari Jimboni humo.
Fri, 15 Mar 2024 - 11min - 393 - Ni kwa namna gani Mama Bikira Maria ni Mwalimu wa Huruma ya Mungu?
Ungana nami Mtangazaji wako Erick Paschal Jnr katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi ambapo niko naye Padre Dominic Mavula C.PP.S Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania akiendelea kutupitisha kwa kina katika mada ya Huruma ya Mungu wakati wa kipindi cha Kwaresima na kwa namna ya kipekee mada ndogo ya Mama Bikira Maria Mwalimu wa Huruma […]
Wed, 13 Mar 2024 - 57min
Podcasts similaires à Radio Maria Tanzania
- Conversations ABC listen
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Dateline NBC NBC News
- 財經一路發 News98
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- アンガールズのジャンピン[オールナイトニッポンPODCAST] ニッポン放送
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 吳淡如人生實用商學院 吳淡如
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR
Autres podcasts de Religion et Spiritualité
- Translation of the Quran in Swahili Unknown
- Uhusiano Kati ya Huduma Ya YESU na Ile Ya YOHANA MBATIZAJI Kama Ilivyoandikwa Katika Injili Nne The New Life Mission
- Joel Osteen Podcast Joel Osteen, SiriusXM
- Joyce Meyer's Talk It Out Podcast Joyce Meyer
- Neno @ttb.twr.org/swahili Thru the Bible Swahili
- قصص القرآن علم ينتفع به
- Unter Pfarrerstöchtern ZEIT ONLINE
- FUATA BIBLIA IKUONGOZE FUATA BIBLIA
- Joyce Meyer Enjoying Everyday Life® Radio Podcast Joyce Meyer
- Swahili Bible With Phillip Odera phillip odera
- KOINONIA CONNECT with Apostle Joshua Selman Blessing Masawi
- Apostle Joshua Selman Apostle Joshua Selman
- Living a Legacy Moody Radio
- IQRA (Read) IQRA
- تفسير القرآن الكريم محمد متولي الشعراوي
- Mufti Menk Muslim Central
- Sein und Streit Deutschlandfunk Kultur
- العلم والإيمان - د. مصطفى محمود علم ينتفع به
- Islamic Podcast Islamic Archive
- Islamic Tel- Tech