Podcasts by Category

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu

488 - Je, Wafahamu Siri ya Miaka 28 ya Radio Maria Tanzania kwa Wanautume wake?
0:00 / 0:00
1x
  • 488 - Je, Wafahamu Siri ya Miaka 28 ya Radio Maria Tanzania kwa Wanautume wake?

    Uinjilishaji  ni wajibu wa kila Mkristo Mbazitwa, Radio Maria Tanzania inarahisisha kazi hiyo ya  Uinjilishaji kupitia vipindi vyake Mbalimbali  Katika miaka 28 ya Radio Maria Tanzania, karibu  uwasikilize Wanautume wa Radio Maria Tanzania wakielezea  Utume huu Miaka 28 iliyopita  kupitia Makala hii iliyotayarishwa na Agatha Kisimba.

    Fri, 26 Apr 2024 - 54min
  • 487 - Miaka 28 ya Utume wa Radio Maria nchini Tanzania

    Karibu usikilize Makala maalumu ya Miaka 28 ya Uinjilishaji wa Radio Maria Tanzania  Katika makala hii , Rais wa Radio Maria Tanzania Ndugu Humphrey Julius Kira, amezungumzia Miaka 28 ya Radio Maria Tanzania tangu kuanzishwa  kwake  Aprili 26,1996 na pia ameelezea kwa undani namna Taasisi hii ilivyokuwa na kuenea kwa wigo wa Matangazo hapa nchini […]

    Fri, 26 Apr 2024 - 58min
  • 486 - Fahamu dalili za wito wa maisha ya wakfu.

    Ungana na Fredy William katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, ambapo Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania,  anazungumzia juu ya dalili za wito wa maisha ya wakfu.

    Fri, 26 Apr 2024 - 53min
  • 485 - Fahamu dalili au cheche za wito.

    Karibu Ungane nami Happiness Mlewa,  katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania,  Mada ni muendelezo wa dalili au cheche za wito.

    Fri, 26 Apr 2024 - 56min
  • 484 - Je, ni kweli Makadinari wa Afrika hawachaguliwi kuwa Mapapa?

    Karibu katika Kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu la Songea, Frateri Noah Mwamfupe anajibu swali lililoulizwa, Kwanini Makadinari wa Afrika hawachaguliwi kuwa Mapapa?

    Wed, 24 Apr 2024 - 24min
Show More Episodes