Filtrar por gênero

Iran-Tanzania Podcast

Iran-Tanzania Podcast

Iran.Tanzania

Audio za Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

12 - MALENGA WA KIIRANI SAADI SHIRAZI
0:00 / 0:00
1x
  • 12 - MALENGA WA KIIRANI SAADI SHIRAZI

    Musharraf al-Din Mosleh ibn Abdullah ibn Musharraf, ambaye baadaye alijulikana kama Saadi Shirazi, ni mmoja kati ya malenga na mshairi mkubwa na mashuhuri nchini Iran. Wanahistoria wanaamini kwamba Saadi Shirazi alizaliwa kati ya mwaka 600 na 610 Hijiria (sawa na takriban mwaka 1210 Miladia). Walakini, hakuna tarehe kamili inayojulikana ya kuzaliwa kwa malenga huyu, ingawa wanahistoria wanakadiria mwaka huo wa kuzaliwa kulingana na athari za kazi zake. Saadi alizaliwa katika familia ya wanazuoni, wasomi na watu wenye maadili mema. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa Mahakama ya Atabak na Shah Saad bin Zangi. Wengine wanaamini kwamba mshairi huyu amechagua jina la ukoo la Saadi kama ni mtu mwenye utambuzi wa haki. Mbali na kuhudumu katika mahakama, baba yake pia alikuwa akijishughulisha na masuala ya kidini na alikuwa akimshajiisha mno mtoto wake kujifundisha elimu ya kisekula na kidini pia. Kwa msaada wa baba yake, Saadi alipata ujuzi wa kina katika nyanja za historia na fasihi. Wakati wa kuzaliwa kwake, mtawala wa Shiraz alikuwa mfalme wa tatu wa serikali ya Atabakan. Nguvu ya Waseljuk ilipodhoofika siku baada ya siku katika kutawala nchi, uliibuka mlolongo wa utawala wa kieneo. Mbali na Shiraz, Atabak pia alikuwa na nguvu za kiutawala huko Damascus, Mosul, Aleppo (Halab), Mesopotamia ( Furati na Hidekeli), na Azerbaijan. Baba yake Saadi alifariki dunia, wakati Saadi akiwa na umri wa miaka 12, na babu yake mzaa mama, Massoud ibn Mosleh, alichukua jukumu la kumlea na kumtunza mjukuu wake. Katika wasifu wa Saadi, tunasoma kwamba baada ya mshairi huyu kujifunza misingi ya elimu ya kidini na fasihi huko Shiraz, alikwenda Baghdad akiwa bado barobaro na kijana chini ya usimamizi wa Atabak na akajiunga katika madrasa ya Nidhamiyyah. Shule hii ilikuwa inatoa elimu maalumu kwa watu wanaotaka kujikita zaidi katika nyanja za fiqh ( sheria za Kiislamu) na falsafa. Wanazuoni wakubwa kama vile Suhrawardi walimlea kielimu Saadi katika madrasa hiyo. Baada ya kumaliza mafunzo, Saadi akaazimia kufanya safari katika maeneo ya Hijaz, Sham na Syria kwa lengo la kupata elimu na uzoefu zaidi. Baada ya hapo akashika njia na kuelekea Makka. Wakati huo huo, alifanikiwa kufunga ndoa, na kisha alifanikiwa kupata mtoto, lakini baada ya kumpoteza mtoto wake huyo, Saadi aliamua kusafiri tena ili kuvumilia mateso hayo, mateso ambayo yalimfanya awe mwenye kupenda zaidi mashairi. Saadi alitembelea miji mbalimbali duniani kote na huko alijishughulisha zaidi na kufundisha na kuhubiri katika miji hiyo. Wataalamu wengine wa historia wamethibitisha kufanya safari yake ya India na sehemu nyingine kadhaa za dunia, na wanaeleza kuwa, safari hizo zilidumu takriban miaka 30. Hata hivyo, muda wa safari na maeneo aliyotembelea Saadi, ni mambo ambayo bado yanatiliwa shaka mno. Hatimaye, baada ya kupita miaka mingi na kupata uzoefu wa kutosha, malenga huyu aliamua kurudi katika nchi yake na mji wake wa asili wa Shiraz. Wakati wa kurejea kwake Shiraz, Abu Bakr ibn Sa'd, mfalme wa Atabaki, alikuwa akitawala huko Shiraz wakati huo. Na kulingana na baadhi ya maelezo ya watu, mshairi huyo alichukua jina la ukoo wa Saadi kutoka kwa jina la mfalme (Saad). Baada ya Saadi kurejea Shiraz, mshairi huyu alianza kuandika na kukusanya kazi zake. Kazi yake ya kwanza aliyoiandika ilikuwa kuandika kitabu cha mashairi alichokipa jina la Bustan, mnamo mwaka 655 Hijria, na kukabidhi mkusanyiko wa mashairi hayo kwa mfalme aliyekuwa akitawala kipindi hicho aitwaye Abubakar ibn Sa'd Zangi. Kitabu cha mashairi cha Golestan kilichoandikwa na malenga huyu mkubwa kilitungwa mwaka wa 656 Hijiria, mwaka mmoja baada ya kuandikwa kwa kitabu cha Bustan. Saadi alikamilisha uandishi wa mashairi ya kitabu hicho kwa muda mfupi. Kuandikwa kwa vitabu viwili katika muda mfupi kunaonyesha kwamba, kwa kiasi kikubwa mashairi hayo yalikuwa yameshatayarishwa mapema, bali alichokifanya ni kukusanya na kufanya masahihisho katika hatua za mwisho kabla ya kuchapishwa. Mengi yamesemwa kuhusu Saadi juu

    Thu, 21 Apr 2022 - 13min
  • 11 - ATTAR NEYSHABURI MALENGA WA KIIRANI

    ATTAR  NEYSHABURI  MALENGA WA KIIRANI

     

    Tarehe 25 Farvardin kwa mujibu wa ( Kalenda ya Kiirani) inayosadifiana na tarehe 14 Aprili,  ni siku ya  kumkumbuka na kumuadhimisha malenga wa Kiirani Farid al-Din Abu Hamid Muhammad bin Abu Bakr Ibrahim bin Is- haq Attar Neyshabouri, ambaye ni mmoja wa washairi mashuhuri, aaref na mwanafikra mkubwa wa Kiirani aliyeishi  mwishoni mwa karne ya sita na mwanzoni mwa karne ya saba Hijria. Baadhi ya wanahistoria wameandika kuwa, mwanafikra na malenga huyo wa Kiajemi amezaliwa mwaka  513 na wengine wanaeleza kuwa alizaliwa mwaka 537 Hijiria. 

    Attar Neyshabouri alizaliwa katika kijiji cha Kadkan au Shadiakh, ambacho wakati huo kilikuwa sehemu ya jiji la Neyshabour. Hakuna habari inayoelezea taarifa zake za utotoni mwake, isipokuwa baba yake aliishi katika mji wa Shadiakh  akifanya kazi ya kuuza dawa za asili,  na alikuwa mahiri na hodari mno katika biashara hii ya kuuza dawa za asili, na baada ya kufariki dunia baba yake, Farid al Din Attar Neyshabouri  aliendeleza shughuli za marehemu  baba yake ya kuuza dawa  za asili. Wakati akishughulika na uuzaji wa dawa za asili Attar Neyshabouri alikuwa akitoa tiba ya asili na wala haijulikani utaalamu huo  wa kutoa tiba ya asilii aliupata kutoka kwa nani. Attar Neyshabouri aliendelea na shughuli zake za kutoa tiba ya asili sanjari na kuuza dawa za asili hadi pale yalipopatikana mapinduzi ya kiroho na kimaanawi kwa upande wake, na jambo  hili limebainishwa kwa kutolewa visa kadhaa, lakini kisa maarufu ni hiki kifuatacho:

     “Siku moja Attar Neyshabouri alikuwa dukani kwake akifanya shughuli zake, mara akaingia “Darwesh" na akaanza kusema maneno kadhaa yanayohusiana na Mwenyezi Mungu, ili Attar aweze kuvutika na  kumsaidia, lakini Darwesh hakupata msaada wowote kutoka kwa Attar Neyshabouri. Darwesh akamwambia Attar : Ewe kijana unataka ufariki duniani  kwa kifo cha namna gani? Attar akajibu: Kwa njia ileile ambayo wewe unataka kufa. Darwesh akasema; Wewe unataka kufa kama nitakavyokufa mimi? Attar akajibu: Ndio, Darwesh akachukua bakuli lake lililotengenezwa kwa mbao na kuliweka chini ya kichwa chake na akasema maneno ya Mwenyezi Mungu na hatimaye  kufariki dunia. Kwa vile Attar Neyshabouri aliliona tukio hilo kwa macho yake aliathirika mno na kubadilika na akaamua kutoka dukani na kubadilisha kikamilifu mtindo na  mwenendo wa maisha yake” .

    Attar Neyshabouri aliposhuhudia tukio hilo la Darwesh , akaacha kabisa shughuli za tiba na biashara za dawa za asili, na akaamua kuelekea kwa Sheikh Mkuu Aref Rukniddin Akaf , wakati huo Sheikh Aref alikuwa mtu maarufu na mashuhuri mno na kwa miaka kadhaa Attar Neyshabouri alikuwa akipata elimu na maarifa  kutoka kwa sheikh Aref Rukniddin Akaf. 

    Attaf Neyshabouri aliweza kutumia nusu ya umri wake kwa kufanya safari katika miji mbalimbali, na katika safari zake hizo alifanikiwa kukutana na masheikh wakubwa wakubwa katika zama hizo, na safari hizo ziliweza kumfikisha hadi kwa sheikh Majiduddin Baghdadi. 

    Inasemekana kuwa Sheikh Aref alipofikia marika ya uzee, Bahauddin Muhammad baba wa Jalaluddin Balkhi alikuwa pamoja na mwanawe walifanya safari ya kuelekea Iraq , wakiwa njiani walipitia Neyshabouri na wakafanikiwa kumtembelea Attar Neyshabouri, hivyo Sheikh Attar Neyshabouri alitoa nakala moja kati ya makala zake za mashairi na kumpa Jalaluddin ambapo wakati huo alikuwa bado kijana mdogo mno.


    Mon, 18 Apr 2022 - 07min
  • 10 - Siku kuu ya Nowruz Mwaka Mpya wa Kiiran

    Jumatatu ya Tarehe 21 Machi 2022 Miladia inayosadifiana na tarehe (Mosi / Farvardin 1401) ni siku ya kuanza mwaka mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia. Siku hii ambayo hujulikana kama Nowruz, ni mwanzo wa sherehe za kale na za muda mrefu na matawi yake yameenea katika kona mbalimbali za Dunia hadi Afrika Mashariki. Asili ya sherehe za Mwaka Kogwahuko Makunduchi visiwani Zanzibar, ni sherehe hizo za Nowruzi za nchini Iran.

    Sun, 27 Mar 2022 - 15min
  • 9 - Mwanamalenga wa Kiirani Nezami

    Jamaluddin Abu Mohammad hakuweza kupata upendo wa wazazi  wake kwa muda mrefu; kwani wazazi wake walifariki dunia  akiwa  bado mtoto na kupata malezi akiwa mtoto yatima. Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kuwa, Nezami Ganjavi hakuwahi kuondoka katika mji wa Ganja akiwa bado na umri mdogo, na alipofikia marika ya ujana , aliweza kujifunza sanaa na ujuzi  mbalimbali na hatimaye alikuwa na ufasaha wa kuzungumza na kuandika lugha za Kiazeri, Kiarabu, Kiajemi na Kipahlavi.

    Nezami ni bingwa na mshairi anayepaswa  kuzingatiwa kwenye mihimili na nguzo za ushairi wa Kiajemi. Yeye ni mmoja wa malenga aliyekuwa na kipaji cha kuandika mashairi na kuyasoma kwa sauti nzuri, iliyowavutia wasikilizaji. Ingawa hekaya na simulizi za hadithi za Kiajemi hazikuanzishwa na Nezami, lakini  gwiji huyo anahesabiwa kuwa ni mshairi pekee  aliyeweza kuendeleza ushairi wa mafumbo  kwa  kiwango cha juu zaidi kufikia mwisho wa karne ya sita.

    Nezami aliweza kujiwekea nafasi maalumu katika fasihi ya lugha ya Kifarsi inayotumika  Iran na ametumia takriban miaka thelathini ya maisha yake akitunga mkusanyiko wake wa mashairi yanayoitwa "Hazina Tano" au "Khamseh". Mkusanyiko huu una mashairi matano marefu, ambayo ni: "Makhzan al-Asrar", "Khosrow na Shirin", "Lalya na Majnoon", "Haft Peykar" na "Iskander Nameh" ni hazina tano. Pia, mkusanyo wa mashairi yaliyosalia kutoka kwa Nezami ni pamoja na mashairi, mashairi ya sauti vipande ambavyo vina nafasi maalumu katika fasihi ya Kiajemi.

    Ingawa umaarufu mwingi wa Nezami unatokana na kutunga mashairi ya mapenzi, yenye hekima na sahili. Kwa maneno mengine, mashairi yake ni rahisi lakini ya kina, na mashairi yake yalikuwa yanamfanya mtu kufikiria na kutafakari kwa kina ili kupata siri iliyofichwa katika maneno yake. Kuna jumbe nyingi za kifalsafa ambazo zimeelezwa kwa kutumia maneno mepesi  na fasaha,  badala ya kutumia maneno magumu na mazito. Nyingi za beti zake za mashairi zilikuwa zikielezea  maisha ya akhera, sanjari na kuyafurahia maisha mafupi ya ulimwenguni. 

    Kuna tofauti za maoni kuhusu kuzaliwa kwa baba wa mshairi Nezami Ganjavi, na baadhi ya vyanzo vinaeleza kuwa anatoka Tafresh au Farahan. Lakini Behrouz Thorotian (mtafiti wa fasihi, mwanasayansi na profesa mstaafu) anaeleza kuwa,  mwanzo wa beti za mashairi ya Layla na Majnoon, zinaonyesha kuwa alikuwa na asili ya Kiajemi. Ameendelea kusema kuwa, ubeti wa 36 wa shairi la Leyla  na Majnoon, unafichua kazi na nafasi ya mshairi ambaye alikuwa Dehqan yaani “mkulima” na kuitambulisha jamii yake kuwa ni  Muajemi.

    Kwa Wairani neno Dehqan "mkulima" linamaanisha  mmiliki wa ardhi ya kilimo;  malenga  Ferdowsi naye katika beti zake amefafanua kuwa,  tafsiri ya neno hilo  lilitumika baadaye kwa Wairani wote. Kwa kuongezea, neno Dehqan "mkulima" lilitumiwa pia kwa maana ya  "mwanahistoria". Kwa hivyo, inaweza kueleweka kuwa Nezami  Ganjavi anajitambulisha kama malenga, mkulima wa Iran, mwanahistoria, muimbaji wa mashairi  na mmiliki wa ardhi ya kilimo. Wakulima wamekuwa na jukumu la kuhifadhi tamaduni na historia ya Iran katika kipindi cha Kiislamu, na kwa ufupi, familia ya Nezami Ganjavi inaweza kuchukuliwa kuwa familia ya wakulima wenye ufahamu wa kitamaduni na utajiri wa mali ambao wamekuwa na nafasi muhimu katika fasihi.

    Nezami Ganjavi alikuwa mshairi mashuhuri, mwandishi wa riwaya, mwenye hekima na ambaye amekuwa  na ushawishi mkubwa katika fasihi ya Kiajemi na daima ametajwa kuwa mtu muhimu katika historia.

    Dola la Uajemi ni moja kati ya madola makubwa yaliyokuwa yakitawala duniani. Jamhuri ya Azerbaijan, iliyoko katika eneo la Caucasia kati ya Ulaya na Asia ilikuwa chini ya himaya ya dola la Uajemi katika zama hizo. 


    Fri, 11 Mar 2022 - 12min
  • 8 - Kumbukizi ya Miaka miwili ya Luteni Jenerali Qassem Suleimani 3 January 2020

    kumbukizi ya miaka 2 ya shujaa mpigania haki na amani Haj Qassem Suleimani, ambapo aliuiliwa Shahidi na Majeshi dhalimu ya Marekeni mjiini Baghdad nchini Iraq. Kamanda Soleimani ambaye amepewa lakabu ya bwana wa mashahidi wa muqawama, katika umri wake wote uliojaa baraka na akiwa kamanda wa IRGC, alikuwa mstari wa mbele kuyasaidia na kuyaunga mkono mataifa yote yanayodhulumiwa ya Waislamu, bila ya kujali ni mataifa ya watu gani. Muhimu kwake muda wote ilikuwa ni kupigania Uislamu na mafundisho sahihi ya Qur'ani Tukufu. Shujaa huyu (Qassem Soleimani) alizaliwa tarehe 11 Machi 1957, katika kijiji cha Qanat-e Malek, Mkoa wa Kerman nchini Iran. Baada ya kumaliza masomo akiwa na umri wa miaka 18, alihamia mjini Kerman na huko aliajiriwa na Shirika la Maji la mji huo. Wakati wa harakati za mapinduzi ya Kiislamu zikiwa zimepamba moto, Qassem Soleimani alifahamiana na mwanachuoni mmoja wa kidini aliyeitwa Sheikh Reza Kamyab aliyetoka mji wa Mashhad, ulioko kaskazini mashariki mwa Iran na kwenda mjini Kerman kulingania dini, sanjari  na kuelezea dhulma na ukandamizaji unaofanywa na utawala wa kifalme dhidi ya wananchi wa matabaka mbalimbali nchini humo. Kuhusiana na mauaji hayo, Ripota Maalumu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN), Agnès Callamard amesema kuwa, mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni ugaidi wa kiserikali wa Marekani na yalikiuka sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa. Msimamo huo wa Umoja wa Mataifa umewakasirisha sana maafisa wa serikali ya Marekani ambao waliharakisha kutetea kitendo cha mauaji hayo.  Callamard ameongeza kuwa, Marekani imeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha wa kuyapa nguvu madai yake kwamba kamanda Soleimani alikuwa tishio kwa taifa hilo.  Nchi kadhaa za Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu, Umoja wa Mataifa na jumuiya mbalimbali za kutetea haki za binadamu duniani zililaani kitendo hicho cha kigaidi cha Marekani dhidi ya afisa wa ngazi za juu wa jeshi la Iran.   Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea

    Tue, 04 Jan 2022 - 10min
Mostrar mais episódios