Podcasts by Category
- 192 - STORY YANGU NA MWENYE UMAR SHARIFFMon, 27 Nov 2023 - 41min
- 191 - STORY YANGU NA MOHAMMAD ABBASMon, 13 Nov 2023 - 35min
- 190 - STORY YANGU NA SALIM MOHAMMEDTue, 10 Oct 2023 - 49min
- 189 - STORY YANGU MOHAMMED THABITSat, 30 Sep 2023 - 35min
- 188 - STORY YANGU NA SWALEH YAHYATue, 19 Sep 2023 - 30min
- 187 - STORY YANGU NA MURAD SWALEHWed, 13 Sep 2023 - 50min
- 186 - STORY YANGU NA CHARITY CHIGULUFri, 08 Sep 2023 - 27min
- 185 - Nipe Sanitary pads na miti nikupe chupa za plastiki tukabili climate change
Utunzaji wa mazingira umekua changamoto kubwa sana kote ulimwenguni kwani mabadiliko ya hali ya hewa imeathiri vigezo vingi katika jamii ikiwemo afya, hewa safi, maji safi ya kunywa,chakula na makazi salama.
Kufuatia hali hio wanafunzi katika shule ya Salex Transition Academy iliyoko eneo la Mtongwe kaunti ya Mombasa wamejitosa katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi,kwa kutumia mbinu ya kubadilishana chupa za plastiki kwa sodo,miti na vifaa vingine vya masomo.
Fatuma Hamisi mwenye umri wa miaka 13 ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Salex Transition Academy.Yeye ni mwanafunzi wa gredi ya 6 na pia ni miongoni mwa wanafunzi wanaojishughulisha na utunzaji wa mazingira katika shule hiyo.
Mwandishi:Athuman Luchi
Tue, 08 Aug 2023 - 08min - 184 - WANAWAKE WATUMIA TEKNOLOGIA KUJIIMARISHA KIUCHUMI
Licha ya idadi ya wanawake katika taalum ya teknologia kuwa ndogo ikilinganishwa na idadi ya wanaume, wanawake wameonekana kupambana ili kukabiliana na tofauti hiyo.
Ripoti kutoka benki kuu ya dunia inaonyesha kuwa wanawake wako chini ya thuluthi moja ya wafanyikazi ulimwenguni katika nyanja zinazohusiana na teknolojia.
Ambapo wanashikilia asilimia 28 ya kazi zote za kompyuta na hisabati, na asilimia15.9 ya kazi za uhandisi na usanifu
Mwandishi:Nuru Mwalimu
Mon, 07 Aug 2023 - 12min - 183 - Mtiririko wa taka baharini, tishio la kuangamia kwa viumbe vya bahariMon, 15 May 2023 - 12min
- 182 - Challenges of teenage pregnancy facing girls with mental disability.Tue, 25 Apr 2023 - 08min
- 181 - Wakulima Wanavyokabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na Climate Change
Mabadiliko ya Tabia Nchi yameathiri sana wakulima na wafugaji hatua inayo wafanya wengi kukumbwa na tatizo la afya ya Akili.Kufuatia hatua hio sasa baadhi ya wakulima wanajizatiti kukabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na mabadiliko hayo.Sasa wakulima hao,wamejitosa katika ufugaji wa nyuki na vipepeo,huku wengine wakifanya biashara ndogo ndogo za kukimu mahitaji ya familia.
Athuman Luchi,ametuandalia makala hayo aliyoyapa jina la Wakulima Wanavyokabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na Climate Change
Mon, 03 Apr 2023 - 04min - 180 - Kumaliza Dhulma za Mtandao Hatua kwa HatuaFri, 17 Mar 2023 - 10min
- 179 - Ujangili wa viumbe vya bahariniThu, 09 Mar 2023 - 09min
- 178 - Teknolojia ya Rangi Katika Kukabiliana na Uhalifu MombasaTue, 07 Mar 2023 - 11min
- 177 - Ushirikiano unavyosaidia kupambana na mbinu za uvuvi haramu Shimoni-Kwale.Mon, 06 Mar 2023 - 15min
- 176 - Watu wenye ulemavu wanavyonufaika na utengenezaji wa siagi ya njugu MombasaWed, 18 May 2022 - 06min
- 175 - Mti Wa Kukabiliana Na Mabadiliko Ya Tabia Nchi Katika Kila Boma.
Ukataji wa miti kiholela umesababisha mabadiliko ya tabianchi,kiangazi,mmomonyoko wa udongo,mafuriko na ongezeko la hewa chafu hatua inayochangia athari mbali mbali kwa jamii.
Kufuatia mabadiliko hayo ya tabia nchi,sasa jamii imejitokeza kuja na mbinu mbali mbali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Makundi ya wanawake na vijana katika kaunti ya kwale yanaendeleza mpango wa upanzi wa miti,walioupa jina laMti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika kila boma.
By Rose Tawa.
Thu, 02 Mar 2023 - 08min - 174 - Uhifadhi Wa Mazingira Umesababisha Kujengwa Kwa Mkahawa Unaovutia Watalii Dabaso.Thu, 02 Mar 2023 - 13min
- 173 - Watu wenye ulemavu wanavyokabili climate change
Mabadiliko ya tabia nchi yanazidi kuathiri kila mtu kila siku,kufuatia hayo watu wenye ulemavu wamejikita katika mbinu mbali mbali za kukabiliana na mabadiliko hayo ya tabia nchi jijini Mombasa.Mwanahabri wetuNuru Mwalimuametuandalia makala yanayosimulia juhudi za watu wenye ulemavu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Wed, 01 Mar 2023 - 06min - 171 - Wanahabari wa Radio Wanavyopambana na ongezeko la habari za KupotoshaMon, 13 Feb 2023 - 11min
- 170 - Kifafa Siyo Uchawi
Kifafa ni ugonjwa wa ubongo unaosababisha mtu kupoteza fahamu kwa muda.
Ugonjwa huu unaweza kumsababishia mtu kufanya vitendo visivyokuwa vya kawaida kama vile kuanguka, kufifitika na hata baadhi ya wagonjwa kutojielewa.
Kulingana na takwimu kutoka kwa shirika la afya dunia WHO, takriban watu milioni 50 duniani wanaugua maradhi haya, na kuyafanya kuwa miongoni mwa maradhi maarufu zaidi ya ubongo duniani.
Tue, 31 Jan 2023 - 03min - 169 - Uji Wa ChekecheaFri, 27 Jan 2023 - 02min
- 168 - Habari ghushi kuhusu coronaWed, 11 Jan 2023 - 05min
- 167 - Dosari Ya Shilingi katika kaunti ya Mombasa
Makala ya Dosari Ya Shilingi yalioandaliwa na Oscar Ochieng yanahusu madeni katika kaunti ya Mombasa. Makala haya yanazamia sababu zinazopelekea kaunti hii kushuhudia madeni ya kiwango cha juu ndani ya miaka mitano ya kifedha iliyopita wakati ambapo utawala wa sasa umeunda jopo kung'amua ukweli kuhusu madeni hayo.
Thu, 29 Dec 2022 - 10min - 166 - Malkia wa GasiThu, 22 Dec 2022 - 15min
- 165 - Wanawake wakumbatia kilimo cha agrivoltaics kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Hali ya kiangazi na mabadiliko ya tabia nchi inaendelea kukumba sehemu mbali mbali humu nchini, hivyo basi inasababisha kushuka kwa kiasi kikubwa kwa mazao ya chakula.Hali hii imeathiri mapato na kupanda kwa bei za vyakula.
Katika kutafuta suluhu zinazowezekana kukabili hali hii, kikundi cha wanawake wakulima kutoka eneo la Lunga Lunga,walianzisha mradi unaoitwa "agrivoltaics,"yaani kutumia paneli za jua katika ukulima ambao husaidia kukabiliana na hali ya ukame unaozidi kuongezeka.
Sun, 25 Dec 2022 - 09min - 164 - Soka inavyotumika kukabili mimba za mapema Kilifi
Kaunti ya Kilifi katika miaka ya hivi karibuni imetajwa kuwa Moja wapo ya kaunti zinazoongoza Kwa idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimba za mapema nchini.
Takwimu kutoka kwa mfumo wa taarifa za afya nchini yaani Kenya Health Information System zikionyesha kuwa jumla ya wasichana 4,909 walio na umri wa kati ya miaka 15-18 walipata mimba katika kipindi Cha mwezi Januari Hadi Agosti Mwaka 2021.
Na kama anavyosimulia Ali Mwalimu kwenye makala haya, mashirika mbalimbali kaunti ya Kilifi yamejitokeza kukabiliana na tatizo hilo.
Sat, 04 Feb 2023 - 15min - 163 - Mwelekeo Kwa wajane waliodhulumiwa
Licha ya kuwa na haki ya urithi pindi mwanawake anapofiliwa na mumewe, jamii imekua tishio kubwa kwa kina mama pindi wanapofiliwa kutona na mila na desturi potofu katika jamii huku takwimu nchini zikionesha kuwa takriban wajane milioni 8 nchini wametelekezwa kutokana na mila potofu na umaskini.
Mwandish: Nuru Mwalim.
Fri, 25 Nov 2022 - 21min - 162 - Kaa La WanawakeTue, 22 Nov 2022 - 16min
- 161 - Kilimo Baharini/Part 2Thu, 10 Nov 2022 - 11min
- 160 - Kilimo Baharini/Part 1Thu, 10 Nov 2022 - 10min
- 159 - Wazazi wakiume waanza kukumbatia ulezi wa watoto walio na Maradhi yanayosababisha ulemavu/Part 2
Kina mama wanaolea Watoto walio na maradhi ya kichwa maji (hydrocephalus) na mgongo wazi (Spinabifida) hupitia changamoto chungu nzima ikiwemo kutelekezwa na waume zao.
Hata hivyo chakutia moyo hapa ni kwamba kuna baadhi ya wazazi wanaume ambao wameanza kuwa na ufahamu kuhusu magonjwa hayo,
Na wanasaidia wazazi wa kike kuwapeleka Watoto hao hospitalini kwa matibabu, na mazoezi.
Kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Tue, 08 Nov 2022 - 08min - 158 - Wazazi wakiume waanza kukumbatia ulezi wa watoto walio na Maradhi yanayosababisha ulemavu/Part 1
Kina mama wanaolea Watoto walio na maradhi ya kichwa maji (hydrocephalus) na mgongo wazi (Spinabifida) hupitia changamoto chungu nzima ikiwemo kutelekezwa na waume zao.
Hata hivyo chakutia moyo hapa ni kwamba kuna baadhi ya wazazi wanaume ambao wameanza kuwa na ufahamu kuhusu magonjwa hayo,
Na wanasaidia wazazi wa kike kuwapeleka Watoto hao hospitalini kwa matibabu, na mazoezi.
Kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Tue, 08 Nov 2022 - 07min - 157 - Ahudumia jamii licha ya changamoto ya kuona
Kila mwaka Alhamisi ya pili ya mwezi Oktoba ni maalumu kwa kuelimisha jamii kuhusu ulemavu wa kuona, athari zake na njia za kuzuia matatizo ya macho.
Mwaka huu,siku hiyo iliadhimishwa tarehe 13 mwezi wa Oktoba. Makala haya ambayo yametayarishwa na Ruth Keah, yanazungumzia kuhusu mwanamke ambaye ana changamoto ya kuona lakini amepuuza changamoto hiyo na anahudumia jamii kwa njia mbalimbali.
Mon, 31 Oct 2022 - 07min - 156 - Hamasa zilivyosaidia wakazi wa Rabai-Kilifi kuepuka homa ya Chikungunya - Part TwoFri, 21 Oct 2022 - 10min
- 155 - Hamasa zilivyosaidia wakazi wa Rabai-Kilifi kuepuka homa ya Chikungunya - Part OneFri, 21 Oct 2022 - 07min
- 154 - Mradi wa Skills Mtaani waboresha elimu kwa Vijana MombasaFri, 21 Oct 2022 - 13min
- 153 - Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part Two
Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni.
Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha.
Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Fri, 21 Oct 2022 - 09min - 152 - Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part One
Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni.
Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha.
Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Fri, 21 Oct 2022 - 07min - 151 - Uhifadhi wa Mikoko kupitia ufugaji wa Nyuki
Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi ambazo wakazi wa Kijiji cha Ganahola, eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa wanafanya kulinda mikoko baharini.
Wakazi hao wanafanya ufugaji wa nyuki ambao hutoa ulinzi kwa mikoko eneo la Tudor Creek hiyo saa 24/7 hivyo hakuna watu wanaweza kuiharibu.
Imatayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Fri, 21 Oct 2022 - 11min - 150 - Kijana anayesakata soka ya kimataifa licha ya ulemavu wake
Makala haya yanaangazia juhudi za kijana kutoka kaunti ya Kilifi-Kenya anayeng'aa katika soka ya kimataifa licha ya kuwa mlemavu. Licha ya kukatazwa kucheza na wazazi wake, hakufa moyo na kuendeleza kipaji chake na kwasasa anategemewa na familia yake kutokana na kipato anachopata kutokana na kucheza soka.
Thu, 13 Oct 2022 - 11min - 149 - Wasichana waendeleza elimu kupitia mchezo wa soka Rabai Part Two
Kijiji cha Jimba, wadi ya Ruruma eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, ni kijiji ambacho kimetegemea sana ukulima kama njia ya kujipatia riziki.
Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kilimo zimepungua kwa kiasi kikubwa, hivyo basi kupelekea jamii nyingi katika kijiji hicho kuishi katika hali ya chini ya Maisha na kushindwa kujiendeleza kimasomo.
Lakini kuna matumaini ya tatizo hilo kuzikwa katika kaburi la sahau kupitia mchezo upendwao na wengi wa soka.
Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Mon, 10 Oct 2022 - 07min - 148 - Wasichana waendeleza elimu kupitia mchezo wa soka Rabai Part One.
Kijiji cha Jimba, wadi ya Ruruma eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, ni kijiji ambacho kimetegemea sana ukulima kama njia ya kujipatia riziki.
Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kilimo zimepungua kwa kiasi kikubwa, hivyo basi kupelekea jamii nyingi katika kijiji hicho kuishi katika hali ya chini ya Maisha na kushindwa kujiendeleza kimasomo.
Lakini kuna matumaini ya tatizo hilo kuzikwa katika kaburi la sahau kupitia mchezo upendwao na wengi wa soka.
Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Mon, 10 Oct 2022 - 10min - 147 - Chupa zageuzwa kuwa mazalia ya Samaki baharini.
Mirundiko ya takataka sio tu katika nchi kavu bali pia baharini kwa miaka mingi imekuwa shida kubwa kuthibiti, taka za baharini zikichangia kuharibika kwa miamba ya matumbawe.
Lakini katika Kijiji cha Mkwiro kaunti ya Kwale Ukanda wa pwani, baadhi ya taka za baharini na zile za nchi kavu zimegeuzwa kuwa thamani kwa kutumia mchakato mbadala wa kutengeneza chupa za matumbawe.
Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Mon, 10 Oct 2022 - 11min - 146 - Kukomesha Unyanyapaa na Ubaguzi kwa wanaokabiliwa na tatizo la Afya ya Akili
Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu nchini Kenya asilimia 0.3% ya watu wanaugua ulemavu wa akili jijini Mombasa.
Wengi wa wenye ulemavu wa akili ukumbwa na unyanyapa,msongo wa mawazo na utengwa katika jamii,hivyo wanajipata wakirandaranda mitaani.
Juma Ali ni kijana mwenye umri wa miaka 30, aliyepona matatizo ya akili yaliyomsumbua kwa muda wa miaka 5.
Anasema alianza kurukwa na akili baada ya kumpoteza mchumba wake katika ajali ya barabarani.Anataja kifo hicho kilimfanya kukabwa na msongo wa mawazo na kuanza kutembea uchi na kushambulia watu.
Mwandishi:Athuman Luchi.
Mon, 10 Oct 2022 - 08min - 145 - Kilio cha mtoto mwenye ulemavu wa akili aliyebakwa na kupachikwa mimba
Watoto wengi wenye matatizo ya akili upitia unyanyasaji wa kingono,kupachikwa ujauzito na wengi wa wanao bakwa usalia kimya wasijue wapi pa kuripoti kisa hicho,Mariam mwenye umri wa miaka 16 ni kati ya watoto wenye ulemavu wa akili walionajisiwa na kupachikwa mimba.
Mariam ambalo si jina lake kamili alibakwa na kusalia kimya bila hata kumjulisha mamake.
Kwa Sasa Mariam analea mtoto mvulana mwenye umri wa miezi mitatu.Anataja kuwa alikuwa ameenda msalaani kujisaidia na huko ndiko alikumbana na jamaa aliyemdhulumu kwa kumbaka.
Mwandishi:Athuman Luchi
Tue, 27 Sep 2022 - 07min - 144 - Changamoto za usalama wa barabarani kwa watu wenye Ulemavu
Bara la afrika limemulikwa sana katika ukuaji wa miundo msingi yake katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi na upanuzi wa barabara.
Licha ya miradi hiyo kurahisisha usafiri kwa mwananchi,bado kuna changamoto kubwa kwa jamii ya watu wenye ulemavu kutokana na ukosefu wa miundo mbinu rafiki kwao.
Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.
Sun, 25 Sep 2022 - 10min - 143 - Jinsi Homa ya Chikungunya Ilivyokabiliwa Mombasa/Part 2
Mwaka wa 2017 hadi mwaka 2018, kaunti ya Mombasa ilishambuliwa na mkurupuko wa homa ya Chikungunya.
Homa ambayo ilikua mara ya kwanza kushuhudiwa.
Ili kukabili mkurupuko huo,kaunti ya Mombasa iliweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhusisha wahudumu wa afya wa kujitolea.
Hatua ambazo zilizaa matunda kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.
Sun, 25 Sep 2022 - 11min - 142 - Jinsi Homa ya Chikungunya Ilivyokabiliwa Mombasa/Part 1
Mwaka wa 2017 hadi mwaka 2018, kaunti ya Mombasa ilishambuliwa na mkurupuko wa homa ya Chikungunya.
Homa ambayo ilikua mara ya kwanza kushuhudiwa.
Ili kukabili mkurupuko huo,kaunti ya Mombasa iliweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhusisha wahudumu wa afya wa kujitolea.
Hatua ambazo zilizaa matunda kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.
Sun, 25 Sep 2022 - 09min - 141 - Nafasi za kisiasa kwa watu wenye ulemavu zayumbayumba.
Watu wenye ulemavu ni miongoni mwa makundi ya jamii zilizotengwa.
Na ili kuimarisha uwakilishi wao katika ulingo wa siasa,Kumekuwa na kila juhudi kuhakikisha kuwa makundi yaliyotengwa yamepata nafasi sawa za uwakilishi.
Hata hivyo kulingana na matokeo yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 humu nchini Kenya, hayakuwapendeza watu wenye ulemavu.
Kama anavyoarifu mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.
Sun, 25 Sep 2022 - 10min - 140 - Simulizi za kutafuta uhuru mikononi mwa maafisa wa usalama
Kutokana na ajali nyingi za barabarani zinazoshuhudiwa humu nchini hasa kwa watu wanaotembea, Serikali iliweka mikakati ya kupunguza ajali hizo kwa kujenga madaraja ya juu ili mwananchi atumie kwa usalama wake mwenyewe.
Lakini licha ya hatua hiyo ya serikali, bado kuna baadhi ya watu wanaopuuza kutumia daraja hizo,mwishowe huishia kutiwa nguvuni na polisi ama askari wa kaunti kwa kukiuka sheria.
Mhariri wetu Ruth Keah amefanya mahojiano na baadhi ya watu walioshikwa na kueleza yaliyojiri mikononi mwa maafisa hao wa usalama.
Sun, 25 Sep 2022 - 07min - 139 - Gharama ya maisha inawadumaza wanawake wenye ulemavuSun, 18 Sep 2022 - 08min
- 138 - Changamoto za mimba za utotoni kwa wasichana wenye matatizo ya akili
Wizara ya afya nchini Kenya ilirekodi visa 45,724 vya mimba za utotoni mnamo Januari na Februari mwaka 2022.Visa hivyo ni vya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 10 na 19 wakiwemo watoto wenye ulemavu wa akili.Watoto hao wenye ulemavu wengi ubakwa na kupachikwa mimba na kuachwa wakiangaika pasi usaidizi.
Mwandishil:Rose Tawa
Mon, 05 Dec 2022 - 08min - 137 - Umuhimu Wakunyonyesha Watoto
Licha ya wanawake waliojifungua kusisitizwa kunyonyesha watoto wao,bado kunao ambao hawanyonyeshi watoto.
Kulingana na shirika la afya duniani WHO, karibu watoto 2 kati ya 3 hawanyonyeshwi maziwa ya mama pekee kwa miezi 6 iliyopendekezwa—kiwango ambacho hakijaimarika katika miongo 2.
Mwandishi:Zahra Nakaya Akosa.
Thu, 15 Sep 2022 - 05min - 136 - Juhudi za kupungunza mkurupuko wa homa ya Dengue Mombasa /Part 2
Kaunti ya Mombasa imekuwa ikishuhudia mkurupuko wa homa zinazosababishwa na mbu ikiwemo homa ya Dengue, Chikungunya na Malaria.
Magonjwa ambayo yanasababishwa na aina Fulani ya mbu.
Mhariri wetu Ruth Keah katika Makala yafuatayo,ameeleza juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na wadau wa afya kuhakikisha kuwa inatokomeza magonjwa hayo.
Mon, 05 Sep 2022 - 09min - 135 - Juhudi za kupungunza mkurupuko wa homa ya Dengue Mombasa/ Part 1
Kaunti ya Mombasa imekuwa ikishuhudia mkurupuko wa homa zinazosababishwa na mbu ikiwemo homa ya Dengue, Chikungunya na Malaria.
Magonjwa ambayo yanasababishwa na aina Fulani ya mbu.
Mhariri wetu Ruth Keah katika Makala yafuatayo,ameeleza juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na wadau wa afya kuhakikisha kuwa inatokomeza magonjwa hayo.
Mon, 05 Sep 2022 - 08min - 134 - Ahudumia jamii kwa kujitolea licha ya kuwa Mlemavu.
Katika miji mingi kumeshuhudiwa ombaomba wa aina tofauti tofauti.
Katika kundi la ombaomba kuna makundi makuu matatu ambao ni watoto, walemavu na wazee.
Kundi kumbwa ambalo lina wahusika wengi katika kuomba ni kundi la watu wenye ulemavu.
Lakini kwa Naima Omar Ali, amekataa kuwa katika kundi hilo la kuomba na badala yake kujitolea kufanya kazi za kusaidia jamii bila malipo.
Naima alifanya mahojiano na muhariri wetu Ruth Keah kwenye makala ifuatayo.
Fri, 26 Aug 2022 - 09min - 133 - Ukakamavu Wangu
Licha ya jamii na baadhi ya familia kuonekana kuwakejeli watu wenye ulemavu,hali ilikuwa tofauti kwa familia ya Lucy Chesi na dadazake wawili ambao wote walizaliwa na ulemavu wa viungo.Wazazi wake walijizatiti na kuwalea vyama na kuwapa elimu ya kutosha.Katika msururu huo wa maisha,Lucy na wenzake walipitia unyanyasaji lakini,waliupuzilia mbali na kusonga mbele kimaisha na kutibithishia umma kuwa ulemavu sio ugonjwa na haustahili kukejeliwa na unyanyasaji.
Mwandishi:Athuman Luchi
Thu, 25 Aug 2022 - 10min - 132 - Wanawake wenye ulemavu wanaowania viti vya siasa kama wagombea huru wakumbwa na changamoto za usafri wa kufanyia kampeni
Licha ya wanawake wenye ulemavu kujitosa kwenye siasa,bado wanakumbwa na changamoto ya usafiri kufuatia maumbile yao,hasa kwa walemavu wenye matatizo ya viungo vya miguu na wale wasioona.
Wanasiasa hawa ambao wanawania kama wawaniaji huru jijini Mombasa,hawana gari za kufanyia kampeni mashinani,hatua inayowafanya kulemaza kampeni zao.
Mwanahabari wetu Athuman Luchi ametusimulia.
Mon, 08 Aug 2022 - 06min - 131 - Ubaguzi wa Wanawake wenye ulemavu wanaowania viti vya kisiasa MombasaSun, 07 Aug 2022 - 09min
- 130 - Kura isiyosiriThu, 04 Aug 2022 - 14min
- 129 - Ugonjwa wa upungufu wa akili watibiwa Mombasa
Takwimu zilizowasilishwa kwa kamati ya Seneti ya Afya mwezi Machi na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe zinaonyesha ugonjwa wa mfadhaiko ndio aina ya ugonjwa wa akili unaoenea zaidi nchini.
Amina Abdalla ni Mwanzilishi wa kituo cha Women Empowerment for Mental illiness Treatment and Rehabilitation Centre, anasema aliamua kuanzisha makao hayo baada ya kuona hakuna makao ya kuishi ya watu wenye akili punguani wanaorandaranda ovyo mitaani na barabarani.
Mwandishi: Nuru Mwalimu.
Fri, 15 Jul 2022 - 13min - 128 - Saratani Ya Matiti Sio Kifo, Inatibika.
Idadi kubwa ya wanawake wenye saratani ya matiti maeneo ya vijijini wamezongwa na kasumba kwamba saratani ya matiti ni kifo na sio rahisi kwa mgonjwa kupona.
Ili kufutilia mbali kasumba kuwa saratani ya matiti ni kifo,nilifanikiwa kufanya mahojiano na Anna Nyambura ambaye alipona saratani ya matiti baada ya kupata matibabu humu nchini pamoja na Daktari Riyaz Kasmani ambaye ni mtaalamu wa ungojwa wa saratani.
Mwandishi: Rose Tawa.
Tue, 17 Jan 2023 - 12min - 127 - Chanjo ya Saratani –Tumaini kwa vizazi Vya baadaye
Mwaka wa 2019 raisi Uhuru Kenyatta alizindua rasmi zoezi la wasichana walio na umri wa miaka 10 kupewa chanjo ya saratani yaani HPV, lakini zoezi hilo lilipata pingamizi kutoka kwa wadau mbalimbali nchini.
Katika Makala haya,mhariri wetu Ruth Keah ameangazia kuhusu habari za urongo ambazo zilifanya wazazi kupuuza chanjo hiyo na wataalamu ambao wamekosoa habari hizo za urongo.
Mon, 04 Jul 2022 - 10min - 126 - Uregeshaji Wa Matumbawe Kwale Part 2
Mabadiliko ya tabia nchi yaani climate change, uvuvi haramu,ongezeko la chupa za plastiki baharini na kuharibiwa kwa matumbawe kumetajwa kuwa moja wapo ya mambo yanayoathiri viumbe wa majini na shughuli za uvuvi.
Lakini ongezeko la joto na kiwango cha maji ya bahari ni miongoni mwa mambo yanayotishia ustawi wa bahari ambayo ni tegemeo kwa Maisha ya binadamu.
Mhariri wetu Ruth Keah alizuru eneo la Shimoni na kuangazia jinsi jamii ya eneo hilo inavyotunza na kupanda miamba ya matumbawe baharini.
Mon, 27 Jun 2022 - 08min - 125 - Uregeshaji Wa Matumbawe Baharini Part 1
Mabadiliko ya tabia nchi yaani climate change, uvuvi haramu,ongezeko la chupa za plastiki baharini na kuharibiwa kwa matumbawe kumetajwa kuwa moja wapo ya mambo yanayoathiri viumbe wa majini na shughuli za uvuvi.
Lakini ongezeko la joto na kiwango cha maji ya bahari ni miongoni mwa mambo yanayotishia ustawi wa bahari ambayo ni tegemeo kwa Maisha ya binadamu.
Mhariri wetu Ruth Keah alizuru eneo la Shimoni na kuangazia jinsi jamii ya eneo hilo inavyotunza na kupanda miamba ya matumbawe baharini.
Mon, 27 Jun 2022 - 10min - 124 - Changamoto Za Usafiri Zinazowakumba Wanasiasa Wanawake Wenye Ulemavu
Licha ya wanawake wenye ulemavu kujitosa kwenye siasa,bado wanakumbwa na changamoto ya usafiri kufuatia maumbile yao,hasa kwa walemavu wenye matatizo ya viungo vya miguu na wale wasioona.
Wanasiasa hawa ambao wanawania kama wawaniaji huru jijini Mombasa,hawana gari za kufanyia kampeni mashinani,hatua inayowafanya kulemaza kampeni zao.
By Rose Tawa
Wed, 22 Jun 2022 - 08min - 122 - Ubaguzi Wa Kisiasa Kwa Wanawake Wenye Ulemavu Wanao Wania Viti Vya Kisiasa.
Licha ya Kifungu 81[1c] cha katiba kusisitiza uwakilishi wa usawa na haki kwa watu wenye ulemavu bado wanawake wenye ulemavu waliojitosa kwenye siasa,wanakumbwa na ubaguzi wa kisiasa kutoka kwa wapinzani wao na hata wafuasi wa wapinzani hao.
Pia kifungu cha katiba cha 27[5] kinaeleza kuwa Mtu hatabaguliwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja dhidi ya mtu mwingine kwa sababu zozote zilizotajwa au kuzingatiwa katika Ibara ya 4.
Wanasiasa hao wenye ulemavu hukejeliwa na kutengwa katika harakati za kisiasa kufuatia maumbile yao,ubaguzi huo unawaathiri wanasiasa hao wenye ulemavu,hatua inayowafanya wenzao kushindwa kuendeleza azima yao ya kuwania viti vya kisiasa.
Mwandishi:Nuru Mwalimu
Fri, 17 Jun 2022 - 09min - 120 - Vifo vya uzazi vyapungua Kwale.Tue, 19 Apr 2022 - 05min
- 119 - Ulemavu Wangu
Jamii nyingi uhusisha ulemavu na laana pamoja na ushirikina,huku wengine wakihusisha ulemavu huo na kasoro zinazotokana kwa mzazi haswa wa kike.Kufuatia madai hayo baadhi ya wanajamii uonekana kuwatenga watoto wanaozaliwa na ulemavu.
Ukweli ni kwamba watu wenye ulemavu wako sawa tu kama wengine wasio walemavu.Katika Makala haya “Ulemavu Wangu” leo tunaangazia dada watatu waliozaliwa na ulemavu,licha ya baadhi ya watu katika jamii kuwatenga,wazazi wao walijizatiti katika kuwalea na kuwasomesha na kwa sasa wote watatu ni wanaharakati wa kutetea haki za wanawake wenye ulemavu jijini Mombasa chini ya shirika lao la Tunaweza Women With Disability.
Lucy Chesi pamoja na dadazake wawili wote walizaliwa na ulemavu na cha kufurahisha ni kwamba licha ya kupitia unyanyasaji na kukashifiwa kwa sababu ya maumbile yao,walipuuza kashifa hizo na kujitahidi katika maisha.
Lucy anasimulia stori yake.
By:Trezer Odero
Sat, 09 Apr 2022 - 10min - 118 - Watu wenye ulemavu wanavyonufaika na utengenezaji wa siagi ya njugu MombasaMon, 04 Apr 2022 - 06min
- 117 - Kuwanusuru wanawake na watoto wenye ulemavu waliobakwa Mombasa
Idadi kubwa ya wanawake na watoto wenye ulemavu wa akili,ulemavu wa kuskia na wale wanaokabiliwa na ulemavu wa kuona wanapitia dhulma mbali mbali ikiwemo ubakaji katika jamii,wengi wa wanaobakwa hutishiwa maisha na husalia kimya wasijue wapi pa kwenda ili kupiga ripoti angalau wapate haki zao za kisheria.
Katika eneo la Kisauni ambapo ninakutana na msichana mwenye umri wa miaka 16 na ambaye ana ulemavu wa akili,pia mtoto huyu ana ujauzito wa miezi 7 alioupata baada ya kubakwa tangu mwezi wa tisa mwaka jana.
By:Nuru Mwalimu
Wed, 30 Mar 2022 - 10min - 115 - Gharama ya mawasiliano kwa watu wenye changamoto ya matamshi.
Mawasiliano ni mchakato wa kuhamisha taarifa kutoka chombo kimoja hadi kingine.
Mawasiliano yanaweza kueleweka vyema kama mchakato kati ya wahusika wawili una mwelekeo uliokubaliwa.
Lakini kwa jamii ya watu wenye changamoto ya matamshi, utumiaji wa simu hizo za mkononi hasa kwa mazungumzo ni changamoto kwao,kama anayosimulia mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Mon, 28 Mar 2022 - 10min - 114 - Takataka Za Plastiki Zinavyotumiwa Kuimarisha Mazingira.
Idadi ya uchafu wa plastiki baharini imeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni, Likiwa ni tatizo kubwa linalokabili mazingira duniani.
Jambo ambalo limeathiri sana upatikanaji wa Samaki kwa sasa katika maeneo mbalimbali ya bahari eneo la pwani, Lakini kikundi cha Gazi Women Magrove Boardwalk kimejitolea kulinda msitu wa mikoko katika eneo hilo la Gazi ili mbali na kulinda mazingira, pia wapate kipato cha kujikidhi kimaisha.
Kama anavyotueleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.
Mon, 21 Mar 2022 - 12min - 113 - Wahudumu wa afya nyanjani waelimisha jamii kuhusu taratibu stahiki za ulaji wa dawa/Part 2.
Mara nyingi watu wanapougua wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari kutokana na uwepo wa dawa madukani.
Bila kujua kwamba dawa hizo zinaweza kumletea mtu madhara makubwa kwenye afya yake ikiwemo kufanya magonjwa kuwa sugu.
Hatua ambayo imepelekea wahudumu wa afya wa nyanjani katika Kijiji cha Ribe eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, kuelimisha wananchi kuhusu taratibu nzuri za utumiaji wa dawa katika Makala yaliyotayarishwa na mhariri wetu Ruth Keah.
Wed, 16 Mar 2022 - 07min - 112 - Wahudumu wa afya nyanjani waelimisha jamii kuhusu taratibu stahiki za ulaji wa dawa/Part 1
Mara nyingi watu wanapougua wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari kutokana na uwepo wa dawa madukani.
Bila kujua kwamba dawa hizo zinaweza kumletea mtu madhara makubwa kwenye afya yake ikiwemo kufanya magonjwa kuwa sugu.
Hatua ambayo imepelekea wahudumu wa afya wa nyanjani katika Kijiji cha Ribe eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, kuelimisha wananchi kuhusu taratibu nzuri za utumiaji wa dawa katika Makala yaliyotayarishwa na mhariri wetu Ruth Keah.
Wed, 16 Mar 2022 - 08min - 111 - Ukulima Wa Unyunyiziaji Maji Kwale.
Nchi nyingi za Afrika zinazopatikana Kusini mwa jangwa la Sahara hazina chakula cha kutosha.
Hali hii hutokana na sababu nyingi ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi ambapo wakulima wanaotegemea mvua mara nyingi huishia kutopata mavuno mvua inapokosa kunyesha.
Mhariri wetu Ruth Keah ametembelea wakulima wa Unyunyiziaji Maji huko Kinango kaunti ya Kwale na kutuandalia Makala yafuatayo.
Mon, 14 Mar 2022 - 10min - 110 - Sumu Ya PlastikiTue, 01 Mar 2022 - 11min
- 109 - Watu Wenye Ulemavu Wanavyotunza Mazingira Mombasa
Kufuati kukithiri kwa mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazingira duniani,Hapa jijini Mombasa watu wenye ulemavu wamejitosa katika utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazingira.
Watu hao wenye ulemavu chini ya shirika la 'Tunaweza Women With Disability' wameanzisha mradi wa kutengeneza bidhaa za urembo kama vile bangili,vipuli na shangaa kwa kutumia karatasi aina mbali mbali ambazo urushwa ovyo kwenye majaa ya taka na kisha kuchomwa hivyo kuchafua mazingira.
Mwandishi:Athuman Luchi
Thu, 24 Feb 2022 - 07min - 108 - Changamoto wanazopitia wanawake wanaojifungua watoto Walemavu
Idadi kubwa ya wanawake wanaojiufungua watoto wenye ulemavuhujikuta wamepewa talaka au kutengwa na waume zao hatua inayowafanya kuishi maisha magumu.Hata hivyo yapo mashirika yaliyojizatiti katika masuala ya kusaidia watoto walemavu ili kuyaboresha maisha yao ya baadae. Mashirika haya yamewapa wanawake hawa matumaini katika maisha.
Mwandishi: Mwanaharusi Rashid
Wed, 16 Feb 2022 - 16min - 107 - Munga Aupuuza ulemavu na kung’aa kimataifa kwenye mchezo wa SokaMon, 14 Feb 2022 - 11min
- 105 - Programu ya rununu inavyosaidia watu wenye ulemavu kupata ajira.
Watu wenye ulemavu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukutana na miundo msingi isiyo rafiki na kunyimwa ajira.
Hatua, iliyosababisha shirika moja la kibinafsi kuzindua programu ya simu ya rununu inayowawezesha watu wenye ulemavu kupata kazi bila kubaguliwa.
Kama anavyosimulia Mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala- programu ya rununu inavyosaidia watu wenye ulemavu kupata ajira.
Mon, 31 Jan 2022 - 10min - 104 - Makala Habari Za Urongo Zaathiri Utoaji wa HPV
Raisi Uhuru Kenyatta alizindua rasmi zoezi la wasichana walio na umri wa miaka 10 kupewa chanjo dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya uzazi ya Human Papilloma Virus yaani HPV.
Lakini zoezi hilo limekumbwa na pingamizi kutoka kwa wadau mbalimbali.
Mhariri wetu Ruth Keah ameandaa Makala maalum ya jinsi habari za urongo mitandaoni pia zimechangia jamii kutokumbatia utoaji huo wa chanjo.
By:Ruth Keah
Mon, 24 Jan 2022 - 11min - 103 - Uvuvi wa kamba mwani wapigwa jeki Lamu
Uvuvi wa Kamba mwani kwa kimombo Lobsters ni maarufu katika kaunti ya Lamu haswa katika eneo la Kizingitini kisiwa cha Pate.
Wavuvi wa Kamba mwani katika kaunti ya Lamu kwa ushirikiano na washikadau mbalimbli wanaendeleza mikakati ya kupata kibali cha kimataifa ili kulifikia soko kubwa, mikakati hii iliyoanza mwaka wa 2011 ni kutokana na uhutaji wa lobsters ulioyopo katika soko.
Kibali hiki kikitarajiwa kutolewa na Marine stewardship council MSC
By:Mwanaharusi Rashid
Fri, 31 Dec 2021 - 15min - 102 - Unyanyasaji wa wanawake walio na matatizo ya akili.Thu, 30 Dec 2021 - 13min
- 101 - Kupigania Haki za Wanawake Wenye Ulemavu Waliodulumiwa Kingono
Idadi kubwa ya wanawake wenye ulemavu wa akili,ulemavu kutosikia na ulemavu wa kuona wanapitia dhulma mbali mbali ikiwemo ubakaji katika jamii, wengi wa wanaobakwa usalia kimya wasijue wapi pa kwenda ili kupiga ripoti angalau wapate haki zao za kisheria.
Jijini Mombasa Pwani ya Kenya shirika la “Tunaweza Women With Disability” limeanza kutoa usaidizi wa kisheria na mafunzo mbali mbali kwa wanawake wenye ulemavu sawia na wazazi wenye watoto walemavu ili waweze kuzinduka na kupigania haki zao.
By:Athuman Luchi
Mon, 27 Dec 2021 - 13min - 100 - Uchunguzi wa habari kuwa vyandarua vya mbu vyaleta kunguni nchini Kenya.
Licha ya shirika la afya duniani WHO,kuidhinisha matumizi ya vyandarua vya mbu vilivyotibiwa,hapa nchini Kenya mkakati huu unakabiliwa na changamoto nyingi kwa sababu kuna taarifa za uongo zinazosambaa kwamba vyandarua hivyo husababisha uvamizi wa kunguni majumbani pindi tu vinapotumika.
By:Mwanaharusi Rashid.
Tue, 21 Dec 2021 - 12min - 99 - ATHARI YA KUJAMIANA KINYUME NA MAUMBILE WAKATI WA KUJIFUNGUASat, 04 Dec 2021 - 11min
- 98 - Changamoto za watu wenye ulemavu wa ngozi maarufu kwa jina albinism
Kulingana na wataalamu wa afya ni kwamba miale ya jua ni kiungo muhimu kwa afya ya binadamu, ila kuna jamii ya watu ambao jua ni hatari kwao na huchukuliwa kama adui mkubwa kwenye ngozi zao.
Kwenye Makala haya ya afya tunaangazia changamoto za watu wenye ulemavu wa ngozi maarufu kwa jina albinism.
Mtayarishi ni Ibrahim Juma Mudibo.
Wed, 01 Dec 2021 - 10min - 97 - WAJIPATIA RIZIKI KUPITIA KILIMO CHA MBUYU
Wengi hufahamu jina mabuyu yaliyozoeleka kuliwa kwa kumumunya utamu wake ambapo hupikwa kwa kuchanganya na sukari, rangi iwe ya kijani nyekundu au hata njano pamoja na viungo vyengine ambapo badae huuzwa katika paketi kati ya shilingi 5-50
Lakini je unapomumunya utamu wake unafahamu pale yanapotokaa?.Yanatoka kwa mti wa m'buyu kwa kimombo baobab tree.
Ni mti mkubwa wa ukanda wa tropiki na matunda yake ndio yanaitwa mabuyu na lile gamba la tunda linaitwa kibuyu na ubuyu ndio hupikwa na kisha tunaomumunya utamu wake.
Mti wa m'buyu ambao huzalisha mabuyu hustawi sana katika maeneo yenye joto ,yaliyo makavu ya Afrika na una uwezo wa kuhimili makali ya kiangazi.
La zaidi ni kwamba wapo wakulima waliozama katika ukulima wa m'buyu kutokana na manufaa mengi yenye kuendeleza uhai.
Wakulima hawa wanategemea mibuyu iliyopo mashambani mwao pamoja na ile iliyostawi katika msitu wa Kaya Kauma kaunti ya Kilifi.
By: Mwanaharusi Rashid
Mon, 29 Nov 2021 - 12min - 96 - Chanjo za Corona haziathiri nguvu za kiumeSun, 28 Nov 2021 - 05min
- 95 - Vyama vya pesa mashinani wakati wa Corona
Ujio wa virusi vya Corona humu nchini ulivuruga shughuli nyingi ikiwemo za kiuchumi.Kina mama wengi wamelazimika kujiunga na vyama vya mashinani ambapo wanapata mikopo bila riba na kujiendeleza na bisahara zao ndogo ndogo. Ruth Keah amezungumza na baadhi ya wanawake waliojiunga na vikundi hivyo na kutuandalia makala haya.
By:Ruth Keah
Fri, 26 Nov 2021 - 09min - 94 - Juhudi za kunasua familia kimawazo dhidi ya makovu ya mauaji ya kiholela
Familia nyingi hupata msongo wa mawazo wanapopoteza wapendwa wao kutokana na mauaji ya kiholela.Katika makala haya Ruth Keah amezungumza na baadhi ya waathiriwa ambao wamepoteza jamaa zao mikononi mwa maafisa wa usalama.Wengi kwa sasa wamejiunga na vikundi vya kubadilishana mawazo ili kupunguza msongo wa mawazo wanaopitia.
By:Ruth Keah.
Fri, 26 Nov 2021 - 11min - 93 - Ukumbatiaji wa Bayoteknolojia kwa usalama wa chakula
Mhogo ni chakula kinachoenziwa na wengi na zao ambalo limewapa wakulima mapato humu nchini.
Chakula chake ni maarufu katika baadhi ya mataifa ya bara la Afrika, Asia na Amerika Kusini.
Kulingana na shirika la utafiti wa kilimo na mifugo humu nchini KALRO, mihogo inapandwa katika hekari laki moja na elfu sabini na mbili nchini ambapo asilimia 60 hupandwa kutoka eneo la Magharibi, Pwani asilimia 30 na eneo la Mashariki likiwa na asilimia 10.
Licha ya kuwa tegemeo kwa wakulima, ukulima huo unakabiliwa na changamoto za maradhi ya aina mbili na kusababisha hasara ya mapato kwa wakulima. Moja wapo ya maradhi hayo ni yale ya cassava brownstreak disease yanayofanya mhogo kuwa rangi ya kahawia na yale ya cassava mosaic ambayo yanaweza kudhibitiwa.
By:Ali Mwalimu
Thu, 25 Nov 2021 - 11min - 92 - MAKALA YA JINSI SEKTA YA AFYA ILIVYOIMARIKA BAADA YA UGATUZI KWALEWed, 24 Nov 2021 - 09min
- 91 - Tamu Tamu ya asali yapotea kwa ukame
Mbali na kuwa mdudu mkali wapo waliozama katika ufugaji wa nyuki kwa ajili ya uzalishaji wa asali kwa matumizi mbalimbali ikiwemo dawa.
Ikumbukwe kuwa si wengi wenye ujasiri na ukakamavu wa kufuga nyuki kutokana na dhana na kasumba kuwa ni wadudu hatari kufuga licha ya kuwa na manufaa tele.
Ufugaji wa nyuki hauna mahitaji mengi ikilinganishwa na ufugaji mwengine wowote cha msingi ni mfugaji kuwa na mizinga.
Kama ukulima na ufugaji wengine wowote ule Nyuki pia hutegemea mvua kwa sababu nyuki hutegemea maua kama chakula na wakati wa mvua ufugaji wa nyuki na uzalishaji asali hushamiri.
By:Mwanaharusi Rashid
Sun, 21 Nov 2021 - 14min - 90 - Uongozi wa wanawake Wapigiwa upatu Pwani.
Wanawake wengi wameshindwa kuafiki katika maswala ya uongozi kutokana na kasumba inayoendelezwa na baadhi yao kwamba mwanamke hawezi kuwajibikia majuku yake ipasavyo.
Kulingana na takwimu za shirika la kimataifa la wanawake UN Women, duniani kuna nchi 27 ambapo wanawake wanachangia chini ya asilimia 10 ya wabunge.
By:Nuru Mwalim
Sat, 20 Nov 2021 - 09min - 89 - Kilimo Cha Pamba ya kisasa chaimarisha Maisha Ya Wakulima Kwale-Part 2
Pamba ni zao ambalo hustawi vizuri katika sehemu kubwa humu nchini. Lakini licha ya hivyo watu wengi hawajaukumbatia sana ukulima wa mmea huo.
Mhariri wetu Ruth Keah aliwatembelea baadhi ya wakulima wanaoendeleza ukulima wa pamba ya kisasa katika kaunti ya Kwale na kutuandalia Makala yafuatayo awamu ya pili- Kilimo Cha Pamba ya kisasa chaimarisha Maisha Ya Wakulima Kwale.
By:Ruth Keah
Thu, 18 Nov 2021 - 08min - 88 - Kilimo Cha Pamba ya kisasa chaimarisha Maisha Ya Wakulima Kwale-Part 1
Pamba ni zao ambalo hustawi vizuri katika sehemu kubwa humu nchini. Lakini licha ya hivyo watu wengi hawajaukumbatia sana ukulima wa mmea huo.
Mhariri wetu Ruth Keah aliwatembelea baadhi ya wakulima wanaoendeleza ukulima wa pamba ya kisasa katika kaunti ya Kwale na kutuandalia Makala yafuatayo- Kilimo Cha Pamba ya kisasa chaimarisha Maisha Ya Wakulima Kwale.
BY:Ruth Keah
Thu, 18 Nov 2021 - 08min
Podcasts similar to RadioRahma
- Conversations ABC listen
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- 財經一路發 News98
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- アンガールズのジャンピン[オールナイトニッポンPODCAST] ニッポン放送
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 吳淡如人生實用商學院 吳淡如
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR
Other Society & Culture Podcasts
- Global News Podcast BBC World Service
- Dateline NBC NBC News
- James O'Brien's Mystery Hour Global
- Parlons-Nous RTL
- Krimpodden VG
- Rain Sounds Sol Good Media
- Maisha Intentional Mercy Kinyodah
- BONGO Classy Isaya A Mwaseba
- Les Brown Greatness Radio Les Brown
- So This Is Love Julia Gaitho
- Erotic Stories Sexuality and Erotica
- The Vybez Hyphē Hyphē
- WERU 89.9 FM Blue Hill, Maine Local News and Public Affairs Archives WERU 89.9 FM Blue Hill, Maine Local News and Public Affairs Archives
- Woman Evolve with Sarah Jakes Roberts The Black Effect and iHeartPodcasts
- Maisha Teya Maisha Teya
- C dans l'air France Télévisions
- TED Talks Daily TED
- Les odyssées France Inter
- NBS Radio NBS Radio Indonesia
- Luo Inspired Luo Inspired