Filtrar por género
Karibu kwenye podcast inayokupa maarifa ya teknolojia, sayansi na majibu ya maswali ya maisha kwa Kiswahili! Tunaangazia maendeleo ya kisasa, kuanzia akili unde yaani AI hadi ukubwa wa ulimwengu. Kila wiki, tunashirikisha uchambuzi wa habari za teknolojia, ufafanuzi wa dhana ngumu, na ushauri wa kivitendo. Jiunge nasi kupata elimu na burudani kupitia lugha yenye utajiri na asili ya Kiafrika. Kiswahili Kitukuzwe kwani ni lugha yetu na urithi wetu #TeknolojiaAfrika #SayansiKiswahili #AfrikaImara
- 84 - Kuzaliwa Kwa Mwezi
Je, umewahi kujiuliza Mwezi ulitoka wapi? 🌕Kwa mabilioni ya miaka, Mwezi umekuwa ukiangaza anga la usiku, lakini historia ya kuzaliwa kwake ni ya kushangaza kuliko wengi wanavyofikiri.Katika video hii utajifunza:✅ Jinsi Mfumo wa Jua ulivyokuwa miaka bilioni 4.5 iliyopita✅ Nadharia ya kisayansi inayoeleza kuzaliwa kwa Mwezi✅ Sayari ya Theia ilikuwa nini?✅ Mgongano mkubwa uliobadilisha historia ya Dunia milele✅ Ushahidi unaowaongoza wanasayansi kuamini nadharia hii✅ Je, Mwezi uliwahi kuwa karibu zaidi na Dunia?Video hii imeandaliwa kwa kutumia ushahidi kutoka tafiti za kisasa za sayansi ya anga, NASA, Lunar and Planetary Institute, na misheni za Apollo.Kama unapenda video za sayansi, anga za juu, historia ya ulimwengu na teknolojia, usisahau kujiunga na channel ya Afrika Imara.🌍 Karibu tujifunze sayansi kwa Kiswahili.
Thu, 24 Sep 2026 - 09min - 83 - MFUMO WA JUA: Siri za Sayari 8 Ambazo Hazijawahi Kufundishwa Shuleni!
Vipi kama ungepata nafasi ya kutembelea kila sayari katika Mfumo wa Jua?Katika documentary hii ya Afrika Imara, tunaanza safari kutoka kwenye Jua, tukitembelea Utaridi, Zuhura, Dunia, Mirihi, Mshtarii, Zohali, Uranusi na Neptuni kabla ya kufika Pluto na Ukanda wa Kuiper.Utajifunza:🪐 Kwa nini Zuhura ni moto kuliko Utaridi?🌍 Kwa nini Dunia ndiyo sayari pekee yenye uhai unaojulikana?🔴 Je, Mirihi inaweza kuwa nyumba ya pili ya binadamu?🌪️ Dhoruba kubwa ya Mshtarii ina ukubwa gani?💍 Pete za Zohali zimeundwaje?❄️ Kwa nini Uranusi umeanguka kwa upande?🌊 Ni nini kinachofanya Neptuni kuwa na upepo mkali zaidi?☄️ Pluto ni sayari au sayari kibete?Hii ni safari ya kisayansi iliyoandaliwa kwa Kiswahili rahisi, ikiwa na taarifa zinazotokana na utafiti wa kisasa wa unajimu na uchunguzi wa anga.Ikiwa unapenda maudhui ya sayansi, historia, teknolojia na siri za ulimwengu, jiunge na Afrika Imara na usikose documentary nyingine zinazokuja.
Thu, 24 Sep 2026 - 12min - 82 - Baada ya Neptuni, kuna nini huko nje?
Zaidi ya Neptuni, mahali ambapo Jua huonekana kama nyota tu ya mbali, kuna eneo kubwa la giza na baridi kali — UKANDA WA KUIPER. Ni "friji" kubwa ya Mfumo wa Jua, iliyojaa mamilioni ya dunia ndogo za barafu zilizohifadhi kumbukumbu ya jinsi mfumo wetu ulivyozaliwa miaka bilioni 4.5 iliyopita. ❄️Katika kipindi hiki cha Afrika Imara tunasafiri hadi ukingoni mwa Mfumo wa Jua kuchunguza mahali palipobadilisha kabisa jinsi tunavyoelewa "sayari" ni nini.
Thu, 17 Sep 2026 - 12min - 81 - NEPTUNI: Sayari ya Mwisho Yenye Upepo wa Kutisha
Karibu kwenye sayari ya mwisho ya Mfumo wetu wa Jua, NEPTUNI, sayari ya barafu (ice giant) iliyo mbali zaidi na Jua, kwa umbali wa kilomita bilioni 4.5. 🌊Ni sayari ya ajabu: japo iko mbali kabisa na joto la Jua, ndiyo yenye upepo mkali zaidi katika Mfumo mzima wa Jua, hadi 2000 km/h. Na cha kushangaza zaidi? Iligunduliwa kwa hesabu za hisabati kabla mtu yeyote hajaiona kwa darubinI.
Thu, 10 Sep 2026 - 17min - 80 - URANUSI: Sayari Iliyolala Upande Na IliyosahaulikaThu, 03 Sep 2026 - 15min
- 79 - Zohali - Sayari Mrembo Na Hatari
Zohali ndiyo sayari inayojulikana zaidi kwa pete zake za ajabu. Lakini je, uzuri wake ndio siri yake kubwa zaidi?Katika documentary hii ya Afrika Imara, tunachunguza ukweli wa kushangaza kuhusu Zohali. Utajifunza jinsi pete zake zilivyoundwa, kwa nini huenda zikatoweka siku moja, siri ya dhoruba yenye umbo la hexagon, na miezi yake ya ajabu kama Titan na Enceladus ambayo imekuwa miongoni mwa maeneo muhimu zaidi katika utafutaji wa maisha nje ya Dunia.
Thu, 27 Aug 2026 - 21min - 78 - Mshtarii - Sayari JituSun, 26 Jul 2026 - 18min
- 77 - Mirihi - Sayari Yenye Uwezo Wa Kuwa Nyumba Ya Pili Ya WanadamuThu, 23 Jul 2026 - 24min
- 76 - Zuhura - Sayari Iliyogeuka KuzimuTue, 21 Jul 2026 - 04min
- 75 - Zebaki - Sayari Ambayo NASA Ilihangaika Kuiifikia Kwa Miaka 30!Mon, 15 Jun 2026 - 13min
- 74 - Newton Alikosea? Jinsi Einstein Alivyobadilisha Maana ya Gravity Mwaka 1915
Kwa zaidi ya karne mbili, maelezo ya Newton ndiyo yaliyotawala sayansi. Kisha mwaka 1915, Albert Einstein akaja na wazo lililobadilisha kila kitu: gravity si nguvu ya kuvutana — ni kupinda kwa nafasi na wakati (space-time). 🌌Kwenye video hii utajifunza kwa mifano rahisi: mfano maarufu wa shuka na mpira, jinsi Jua linavyopindisha njia ya Dunia, uthibitisho wa kupatwa kwa Jua wa mwaka 1919, na kwa nini GPS ya simu yako isingefanya kazi bila nadharia ya Einstein. Na mwishoni — fumbo kubwa ambalo bado halijatatuliwa hadi leo.
Fri, 12 Jun 2026 - 04min - 73 - Kwa Nini Kila Kitu Huanguka CHINI? Siri ya Gravity Iliyowashinda WanasayansiThu, 11 Jun 2026 - 04min
- 72 - Acha Niseme - (ep3) - Je, unajua kwa nini jina lako la kwanza ni la kingereza au kikristo?Sun, 17 May 2026 - 35min
- 71 - Acha Niseme - (ep2) - Ujio wa Dini kwenye Ukanda wa Afrika MasharikiSun, 10 May 2026 - 20min
- 70 - Acha Niseme - UtanguliziMon, 27 Apr 2026 - 05min
- 69 - maana ya Conspiracy theorySat, 25 Apr 2026 - 01min
- 68 - Angahewa Ya DuniaTue, 31 Mar 2026 - 15min
- 67 - Sonic boom ni nini?Wed, 18 Mar 2026 - 21min
- 66 - Mauaji ya Kiongozi Mkuu wa Iran Yalifanikiwa Kwa Sababu ya Matumizi ya AI - Akili UndeFri, 06 Mar 2026 - 04min
- 65 - Maelezo ya Muundo wa DuniaMon, 02 Mar 2026 - 18min
- 64 - Artemis II - Binadamu Wanarudi MweziniWed, 25 Feb 2026 - 15min
- 63 - Tanuru la Moto Lisilozima
Kwa miaka bilioni nne na nusu, vita isiyoisha imekuwa ikishindaniwa moyoni mwa Jua, uvutano ukitaka kuliangamiza, na mlipuko wa nyuklia ukipigana kuliokoa. Safari hii ya kushangaza inakupeleka ndani ya nyota yetu, kupitia matabaka ya moto na shinikizo lisilowezekana, hadi kwenye siri inayowasha uhai wote Duniani. Jifunze jinsi mwanga unavyozaliwa, unavyofungwa kwa maelfu ya miaka, na hatimaye unavyofikia uso wako, ujumbe kutoka zamani za mbali.
Wed, 21 Jan 2026 - 08min - 62 - Tofauti Kati Ya Nuclear Fusion Na Fission
Gundua tofauti za kimsingi kati ya mpasuko wa nyuklia (fission) na muungano wa nyuklia (fusion) katika uchambuzi huu mfupi wa kisayansi. Tunafafanua jinsi mpasuko unavyogawanya atomi kuendesha mitambo ya sasa, ukilinganishwa na muungano unaoiga jinsi Jua linavyofanya kazi kwa kuunganisha atomi. Tazama video hii ili uelewe ni kwa nini muungano wa nyuklia unatazamwa kama 'suluhisho kuu' la nishati safi ukilinganisha na hatari za mionzi za teknolojia ya sasa.
Fri, 16 Jan 2026 - 29min - 61 - Jedwali ya ElementiTue, 23 Dec 2025 - 13min
- 60 - Nguvu kuu ya nyukliaTue, 16 Dec 2025 - 14min
- 59 - Utupu wa AtomiTue, 09 Dec 2025 - 13min
- 58 - Chembe Chembe Ndogo Ndani Ya AtomiFri, 05 Dec 2025 - 18min
- 57 - Chaji ya UmemeMon, 01 Dec 2025 - 03min
- 56 - Ni nini huipa atomi umbo lake?
Katika video hii fupi na ya kielimu, tunaingia ndani kabisa ya ulimwengu mdogo wa atomi na kuchunguza siri inayofanya muundo wake kuwa imara na thabiti. Tutatumia mifano rahisi, kama vile sumaku, kukusaidia kuelewa sheria za msingi za fizikia zinazotawala ulimwengu wetu.Jifunze sayansi kwa njia rahisi na ya kuvutia!
Mon, 03 Nov 2025 - 02min - 55 - Maana ya atomiSun, 12 Oct 2025 - 03min
- 54 - Atomu ni nini?
Je, umewahi kujiuliza ni nini hasa kinachojenga kila kitu unachokiona na kukigusa? Kuanzia kikombe chako cha chai, simu yako, hadi mwili wako mwenyewe? Jibu liko katika chembe ndogo sana isiyoonekana kwa macho inayoitwa ATOMU.Katika makala haya, tunakupeleka kwenye safari ya ajabu na ya kustaajabisha kuelewa msingi wa uhai na maada yote. Tutaanza na wazo rahisi la kukata nyanya hadi tufike kwenye chembe isiyoweza kugawanywa tena, na tutaeleza kwa njia rahisi na ya kuvutia:Ni nini hasa kilicho ndani ya Atomu? Gundua ulimwengu mdogo wa protoni, nyutroni, na elektroni.
Mon, 25 Aug 2025 - 07min - 53 - AI, AGI na ASI zinamaanisha nini?
Katika makala haya ya kipekee, tunafichua siri kuhusu Akili Bandia—kuanzia AI ya kawaida, hadi AGI (Artificial General Intelligence), na hatimaye ASI (Artificial Super Intelligence)!
Tunakufafanulia kwa Kiswahili sanifu na kwa lugha rahisi:✅ AI ni nini na kwa nini iko kila mahali sasa?✅ AGI inatishia kazi zako—ina uwezo sawa na binadamu!✅ ASI ni hatua ya hatari sana—inaweza kuwa mwisho au mwanzo mpya kwa wanadamu.✅ Faida na hasara za kila hatua ya maendeleo ya akili unde.✅ Hatua za kuchukua ili kulinda jamii kutokana na madhara ya AI.
Sat, 09 Aug 2025 - 08min - 52 - Akili Unde Na Masomo
Je, AI inaharibu au kuboresha elimu ya juu? Mojawapo ya sekta zilizoathirika zaidi na ujio wa Artificial Intelligence (AI) ni sekta ya elimu, haswa katika vyuo vikuu. Kila siku, matumizi ya AI katika kufanya assignments, utafiti, na kujifunza yanazidi kuongezeka. Lakini hii ina maana gani kwa walimu, wanafunzi, na mfumo mzima wa elimu? Sikiliza podcast hii ili ujue mawazo yangu kisha ushiriki maoni yako.
Sat, 02 Aug 2025 - 25min - 51 - Akili Unde Na KaziFri, 25 Jul 2025 - 15min
- 50 - Sumaku Ya Dunia - Nguvu Ya Ajabu Inayotulinda Kutoka Kwa Hatari Za Angani!
Je, umewahi kujiuliza ni nini hasa hutulinda dhidi ya hatari za anga za juu?Katika video hii ya kuvutia, tunazama ndani ya mojawapo ya miujiza mikuu ya sayari yetu, sumaku ya Dunia. Kutoka kwa sumaku za utotoni hadi kwenye chuma cha kiowevu chenye joto kali maili elfu chini ya miguu yetu, utaelewa jinsi Dunia yetu inavyozalisha kinga yake ya asili dhidi ya upepo wa jua na hatari kutoka angani.
Thu, 12 Jun 2025 - 19min - 49 - Solar Winds - Upepo wa Jua: Siri Kubwa ya Jua Inayoathiri Dunia Yetu!Sun, 25 May 2025 - 21min
- 48 - Goldilocks Zone - Sehemu Yenye Hali Sahihi Kabisa kwa Uhai
Je, unajua kuwa kuna eneo maalum kwenye anga ambapo maisha yanaweza kustawi? 🌍Wanasayansi wanalita Goldilocks Zone – sehemu yenye hali “sahihi kabisa” kwa uwepo wa maji ya kumiminika, na hivyo kuwezesha maisha! Katika video hii ya kuvutia, tunazama ndani ya siri za anga na kueleza kwa Kiswahili fasaha:🔭 Eneo hili linafanya nini kuwa muhimu sana?☀️ Je, ni kwa nini Dunia ina maisha na sayari kama Zuhura na Mirihi hazina?🌌 Tunakueleza kwa mfano rahisi kama moto wa kambi – si moto sana, si baridi sana!Umechoka kusikia “habitable zone” bila kuelewa maana halisi? Sasa unaweza kufurahia maarifa haya kwa lugha unayoipenda – KISWAHILI.
Sun, 18 May 2025 - 08min - 47 - Kwa Nini Uhai Unapatikana Duniani Pekee?Wed, 14 May 2025 - 16min
- 46 - Methali za Kiswahili na Maana ZakeSat, 10 May 2025 - 39min
- 45 - Ulimwengu ni mkubwa kiasi gani?
Je, umewahi kufikiria jinsi ulimwengu ulivyo mkubwa? 🚀 Kutoka safari ya kuzunguka dunia hadi kufikia kwenye mwezi, jua, na hata sayari ya mbali kabisa – Neptuni, makala haya yatakupa mtazamo wa kushangaza kuhusu ukubwa wa ulimwengu!🛻 Ungechukua miaka 171 kusafiri hadi jua kwa gari la kawaida! Na je, kufika Neptuni? 😲 Zaidi ya miaka 5,000!Usikose video hii inayofafanua ukubwa wa ulimwengu kwa njia rahisi na ya kuvutia! 🌠👀 #Sayansi #Ulimwengu #astronomia #motivation #science #news #extraterrestrial #africa #kenya #tanzania #quotes #knowledge #facts
Wed, 07 May 2025 - 07min - 44 - Ukubwa wa Ulimwengu - Mwaka wa Mwangaza (Light Year)
Je, unajua kwa nini wanasayansi hutumia mwaka wa mwanga badala ya kilomita kupima umbali wa nyota na miili mingine ya anga? 🤔✨ Katika makala haya, tunaeleza kwa kina maana ya mwaka wa mwanga, kasi ya mwangaza, na jinsi vipimo hivi vinavyotusaidia kuelewa ukubwa wa ulimwengu wetu.Mambo utakayojifunza:🌍 Kwa nini kilomita hazitoshi kupima umbali wa miili ya anga💡 Kasi ya mwanga na athari zake kwa uchunguzi wa ulimwengu🚀 Jinsi mwaka wa mwanga unavyotumiwa katika kosmolojiaJiunge nasi katika safari hii ya kuvumbua ulimwengu! 🌌💫#sayansi #Ulimwengu #astronomia #motivation #science #news #extraterrestrial #africa #kenya #tanzania #quotes #knowledge #facts #light #neildegrassetyson
Fri, 28 Mar 2025 - 09min - 43 - Methali za KiswahiliTue, 25 Feb 2025 - 03min
- 42 - Je, ulimwengu ni mkubwa kiasi gani
Je, umewahi kufikiria jinsi ulimwengu ulivyo mkubwa? 🚀 Kutoka safari ya kuzunguka dunia hadi kufikia kwenye mwezi, jua, na hata sayari ya mbali kabisa – Neptuni, makala haya yatakupa mtazamo wa kushangaza kuhusu ukubwa wa ulimwengu!🛻 Ungechukua miaka 171 kusafiri hadi jua kwa gari la kawaida! Na je, kufika Neptuni? 😲 Zaidi ya miaka 5,000!Usikose video hii inayofafanua ukubwa wa ulimwengu kwa njia rahisi na ya kuvutia! 🌠👀 #Sayansi #Ulimwengu #astronomia #motivation #science #news #extraterrestrial #africa #kenya #tanzania #quotes #knowledge #facts
Thu, 20 Feb 2025 - 07min - 41 - Msamiati wa Siku
Jua zaidi kuhusu neno "Ukungu", tafsiri yake kwa Kiingereza, maana yake, na jinsi linavyotumika katika sentensi. Huu ni mwongozo rahisi kwa yeyote anayetaka kujifunza au kuboresha Kiswahili chao.🔹 Maneno na maana zake kwa uwazi🔹 Matamshi sahihi🔹 Matumizi halisi katika sentensiJiunge nami na upanue ufahamu wako wa lugha ya Kiswahili! 🎥✨
Tue, 18 Feb 2025 - 00min - 40 - Msamiati wa Siku
Jua hukusu neno "Mlowezi", tafsiri yake kwa Kiingereza, maana yake, na jinsi linavyotumika katika sentensi. Huu ni mwongozo rahisi kwa yeyote anayetaka kujifunza au kuboresha Kiswahili chao.🔹 Maneno na maana zake kwa uwazi🔹 Matamshi sahihi🔹 Matumizi halisi katika sentensiJiunge nami na upanue ufahamu wako wa lugha ya Kiswahili! 🎥✨
Thu, 13 Feb 2025 - 00min - 39 - Methali za KiswahiliTue, 11 Feb 2025 - 01min
- 38 - Methali za KiswahiliThu, 06 Feb 2025 - 01min
- 37 - Aina za Serikali - Nguvu na Udhaifu Wake
Katika makala haya, tunachunguza nguvu na udhaifu wa aina za serikali tofauti duniani. Kutoka kwa demokrasia hadi utawala wa kioligarki, tunafunua jinsi mifumo hii inavyoathiri maisha ya raia. Pitia mifano halisi na tathmini za kitaalamu, na ujifunze kuhusu changamoto na faida zinazoambatana na kila mfumo wa utawala. Jiunge nasi katika kubaini njia bora za uongozi katika jamii zetu!
Tue, 04 Feb 2025 - 08min - 36 - Je, Kiswahili kinapendwa kweli?Thu, 30 Jan 2025 - 11min
- 35 - Methali na MaishaThu, 23 Jan 2025 - 02min
- 34 - Methali na MaishaWed, 08 Jan 2025 - 03min
- 33 - Methali Na MaishaMon, 20 Jan 2025 - 02min
- 32 - Laana Zipo?Thu, 16 Jan 2025 - 07min
- 31 - UFOs Kwa KiswahiliTue, 14 Jan 2025 - 07min
- 30 - AI kwa Kiswahili
Katika video hii, tunachambua tafsiri mpya ya neno 'Artificial Intelligence' katika lugha ya Kiswahili ambapo sasa inajulikana kama 'akili unde'. Tunaangazia maana ya neno hili jipya pamoja na kuelezea tofauti yake na tafsiri zingine zilizokuwa zinatumika awali kama vile akili bandia, akili mnemba au akili tarakilishi. Pia, tunasisitiza umuhimu wa kufuatilia maendeleo ya istilahi za akili unde kutokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia hii.
Fri, 10 Jan 2025 - 03min - 29 - AI Ni Nini?
Video hii imetayarishwa kwa sababu ya wale wanaotaka kujua AI ni nini. Mazungumzo yanayohusiana na AI yamezidi kuongezeka katika dunia ya sasa na wengi wanatamani kujua AI ama Artificial Intelligence kwa urefu ndiyo ni nini. Tazama video hii nzima na utapata kufahamu AI ni nini na manufaa yake kwa wanadamu ni gani. Asante.
Fri, 03 Jan 2025 - 04min - 28 - Makanisa na Siasa MbayaWed, 01 Jan 2025 - 11min
- 27 - Kiswahili Kitukuzwe - Darubini ya JWSTThu, 29 Feb 2024 - 02min
- 26 - Kiswahili Kitukuzwe - Mradi wa ArtemisSun, 25 Feb 2024 - 06min
- 25 - Kiswahili Kitukuzwe - OpenAI SoraMon, 19 Feb 2024 - 04min
- 24 - Kiswahili Kitukuzwe - Magari ya UmemeTue, 13 Feb 2024 - 06min
- 23 - Kiswahili Kitukuze - Misamiati ya MatundaSat, 27 Jan 2024 - 02min
- 22 - Kiswahili Kitukuzwe - Misamiati ya MadiniThu, 25 Jan 2024 - 06min
- 21 - Kiswahili Kitukuzwe - Misamiati Ya RangiTue, 02 Jan 2024 - 04min
- 20 - Kiswahili Kitukuzwe - Misamiati ya TeknolojiaSun, 24 Dec 2023 - 05min
- 19 - Kiswahili Kitukuzwe - Utangulizi
Huu ni utangulizi wa msururu wa vipindi vya kutukuza kiswahili ambavyo vitaangazia kuongezea maarifa ya misamiati kutoka nyaja tofauti tofauti. Lengo kuu ni kukomaaza ufahamu kwa lugha hii tukufu katika miktadha mbali mbali za kimaisha. Karibu sana na kiswahili kitukuzwe!
Thu, 21 Dec 2023 - 08min - 18 - Gemini AI in swahiliMon, 18 Dec 2023 - 02min
- 17 - "Artificial Intelligence" Kwa kiswahili ni nini?Thu, 30 Nov 2023 - 04min
- 16 - Kurushwa Kwa Starship Ya PiliSun, 26 Nov 2023 - 03min
- 15 - Vitate, visawe na vitaweSat, 18 Nov 2023 - 02min
- 14 - Je, neno 'empire' kwa kiswahili ni nini?Wed, 08 Nov 2023 - 02min
- 13 - Je, tafsiri ya neno 'climate' kwa kiswahili ni nini?Wed, 01 Nov 2023 - 02min
- 12 - Je, neno 'browser' kwa kiswahili ni nini?Mon, 30 Oct 2023 - 02min
- 11 - Halmashauri ya ManispaaFri, 27 Oct 2023 - 01min
- 10 - MchakatoWed, 25 Oct 2023 - 01min
- 9 - Umpembuzi YakinifuSat, 21 Oct 2023 - 02min
- 8 - Misamiati ya Matunda
Je? Unajua tunda la 'apple' linaitwaje kwa Kiswahili? Sikiliza podcast hii ndio uwezekujua hio na mengine mengi
Thu, 31 Mar 2022 - 04min - 7 - Misamiati ya madini
Katika kipindi hiki tunakalimani misamiati ya madini kutoka lugha ya kingereza kuja kwa lungha ya Kiswahili. Asanteni
Wed, 09 Mar 2022 - 05min - 6 - Kufanya Kiswahili ifaneThu, 11 Nov 2021 - 26min
- 5 - Kipindi cha TatuSun, 07 Nov 2021 - 20min
- 4 - Kipindi Cha PiliMon, 01 Nov 2021 - 04min
- 2 - Christianity in AfricaSun, 10 Oct 2021 - 18min
- 1 - Kipindi cha kwanzaTue, 11 May 2021 - 02min
Podcasts similares a Kiswahili Kitukuzwe - Afrika Imara (Swahili Podcast)
El Partidazo de COPE COPE
Herrera en COPE COPE
Es la Mañana de Federico esRadio
La noche de Cuesta esRadio
Hondelatte Raconte Europe 1
Affaires sensibles France Inter
LEGEND Guillaume Pley
HistoryExtra podcast Immediate
Motivational Speech Motivational Speech
El colegio invisible OndaCero
La Rosa de los Vientos OndaCero
Les grands dossiers de l'Histoire par Franck Ferrand Radio Classique
Espacio en blanco Radio Nacional
Rhumba Love. Rhumba 001
Enquêtes criminelles RTL
Entrez dans l'Histoire RTL
Le grand récit RTL
Les Grosses Têtes RTL
L'Heure Du Crime RTL
El Larguero SER Podcast
SER Historia SER Podcast
Todo Concostrina SER Podcast
Un Libro Una Hora SER Podcast
DJ TOPHAZ MIXES Tophaz
