Filtra per genere
- 261 - Je unafahamu umuhimu wa kuzuia upotevu na uharibifu wa chakula?
Mwaka huu ni maadhimisho ya saba ya siku ya kimataifa ya kutoa hamasisho kuhusu utupaji na upotevu wa chakula, ambao unachangia kati ya asilimia 8–10 ya utoaji wa gesi joto
Lengo la maendeleo endelevu nambari 12.3 linalenga kuona dunia ikipunguza upot’evu na uharibufuwa chakula kwa nusu ifikapo mwaka 2030.
Mon, 28 Sep 2026 - 260 - Septemba 22, siku ya kimataifa ya kutotumia magari mijini
Wananchi katika miji mbalimbali ya dunia wanahimizwa kuacha magari yao binafsi nyumbani na kukumbatia mbinu zingine za usafiri zilizo endelevu kama kutumia baiskeli au kutembea kwa miguu.
Makala haya yanaangazia namna baiskeli za umeme zinaweza kuwa moja ya suluhu ya uchafuzi wa hewa kwenye miji unaotokana na sekta ya usafiri.
Wed, 23 Sep 2026 - 259 - Kenya: Wanaharakati watoa mapendekezo mapya dhidi ya plastiki zinazochafua mazingira
Kenya inakabiliwa na changamoto ya plastiki zinazotumiwa mara moja tu kama vile mifuko inayotumiwa sokoni kupakia mboga ambazo huchangia katika uchafuzi wa mazingira licha ya kupigwa marufuku.
Ni Kutokana na hili ambapo wanaharakati wa mazingira wamekuja na mapendekezo mapya ya kukabiliana na tatizo hili, mbali na suluhu la uchakataji.
Moja ya matokeo ya mapendekezo haya ni kuiweka Kenya katika nafasi ya uongozi wa kikanda katika uvumbuzi wa mifumo ya kutumia tena bidhaa.
Hellen Kahaso Dena kutoka shirika la Greenpeace Africa amechambua swala hilo. Sikiliza zaidi kwa kubofya.
Mon, 14 Sep 2026 - 258 - Kenya: Nyenzo(Tool) mpya inavyoanika matumizi ya ufadhili wa tabianchi Kenya
Matumizi ya ufadhili wa hali ya hewa imekuwa swala kuu kwa wadau wa mazingira, kutokana na mianya ya ufuatiliaji.
Nchini Kenya, shirika la Transparency International, sasa linajaribu kuziba mwanya uliopo ambapowakenya watakuwa wakifuatilia miradi na matumizi ya fedha hizi nchini humo kupitia jukwaa jipya la mtandaoni la Climate Finance Watch Tool.
Wed, 26 Aug 2026 - 257 - Kenya: Ubunifu wa unaogeuza magugu maji kuwa mifuko ya kupakia bidhaa na matumizi mengine
Kwa wavuvi katika ziwa Niavasha, kama vile Simon Macharia na Joseph Kimani, Magugu maji yamekuwa kero kwa muda mrefu, na wakati mwingine kuwasababishia hasara.
Lakini sasa kutokana na ubunifu wa Joseph Nguthiri, kijana bingwa wa dunia wa Mazingira wa UNEP mwaka wa 2025, na mwanzilishi wa kampuni yaHyapak wavuvi wanaweza kujipatia kipato zaidi.
Mon, 24 Aug 2026 - 256 - Kenya: Familia hatarini kutokana na kupanda kwa kiwango cha maji ziwa Naivasha
Familia katika kijiji cha Kihoto mjini Naivasha, zimeendelea kutaabika kutokana na athari za kupanda kwa kiwango cha maji kwenye ziwa Naivasha, na kusababisha maji kuingia kwenye kijiji ambayo pia yamesababisha kuenea kwa magugumaji.
Nikurejesha nchini kenya, katika eneo la bonde la ufa, ziwa Bogoria, ziwa Baringo na Ziwa Niavasha, ni mfano wa maziwa ambayo yameendelea kushuhudia kupanda kwa kina cha maji ndani ya miaka 10 zilizopita, katika eneo la Afrika mashariki.
Mon, 10 Aug 2026 - 255 - Kenya: Uchunguzi wabainisha uwepo wa kemikali hatari kwenye bidhaa za plastikiTue, 04 Aug 2026
- 254 - El Niño: Wataalam waonya kuhusu mvua kubwa, mafuriko na joto la kali
Hali ya hewa ya El Niño inaendelea kuimarika kwa kasi na inatarajiwa kutawala katika kipindi cha kuanzia mwezi Agosti hadi Oktoba mwaka wa 2026, hali itakayoongeza uwezekano wa viwango vya joto kuzidi wastani katika maeneo mengi ya dunia na kusababisha mabadiliko makubwa katika mifumo ya mvua.
Mashirika ya hali ya hewa likiwemo lile la dunia WMO na KMD nchini Kenya, yameongeza utaratibu, huduma za taarifa za hali ya hewa na usaidizi wa tahadhari za mapema ili kusaidia serikali, mashirika ya kibinadamu, sekta zinazozingatia hali ya hewa kama vile kilimo na afya, na jamii zilizo katika mazingira magumu kujiandaa kwa athari zinazoweza kutokea.
Tumezungumza na wataalam, bofya hapo kusikiliza.
Mon, 03 Aug 2026 - 253 - Fahamu kuhusu chanzo cha wimbi la joto kali linaloshuhudiwa Ulaya.
Wimbi la joto kali limekumba bara la Ulaya kwa muda sasa, hali iliyosababisha viwango vya juu vya joto katika nchi kadhaa na kusababisha maelfu ya vifo.
Zaidi ya watu 300,000 wamehamishwa na angalau mtu mmoja alifariki dunia kutokana na moto wa nyika nchini Ufaransa na Uhispania, huku vikosi vya zimamoto vikipambana na mioto hiyo.
Leo katika uchambuzi wetu tunaungana na Daktari Joyce Kimutai, mwanasayansi wa tabia nchi kutoka mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini Kenya, anayetuelewesha zaidi kuhusu matukio haya na namna nchi zinaweza kuchukua tahadhari kuwalinda raia wake.
Tue, 28 Jul 2026 - 252 - Juhudi za akina mama kuhifadhi fukwe za bahari pwani ya Kenya
Wakati mataifa mbalimbali duniani yakiongeza juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa bahari, nchini Kenya akina mama wamejitokeza mstari wa mbele kulinda mazingira. Katika Kaunti ya Mombasa, wameanzisha kampeni ya kupanda miti ya asili na kurejesha uoto uliopotea kwenye maeneo ya pwani. .Hii leo katika makala mazingira leo dunia yako kesho ,tunaangazia juhudi za akina mama hao.
Tue, 21 Jul 2026 - 251 - Utengenezaji wa mkaa kutoka kwa mmea wa mianziMon, 06 Jul 2026
- 250 - Mkutano wa Innovate4cities: Kuharakisha hatua za kukabili mabadiliko ya tabianchi kwenye miji duniani.
Mkutano huo ulioandaliwa na Global Covenant of Mayors for Climate and Energy (GCoM kwa ushirikiano na UN-Habitat, ulijadili mada tofauti kama vile sayansi ya tabianchi, sera na namna ya kuangazia mianya iliopo katika elimu, data, ufadhili na utakelezaji zinazolemaza mikakati ya kukabili tabainchi kwenye miji.
Katika makala yetu hivi leo, nimezungumza na BiMaryam Wangeshi, ni msanifu wa majengo lakini pia alikuwa katika kamati ya maandalizi ya mkutano huo.
Mon, 29 Jun 2026 - 249 - Mjadala waibuka kuhusu jinamizi la taka za nguo kwa mazingira
Kila wiki, mamilioni ya nguo za mitumba hufika katika masoko kama vile Gikomba jijini Nairobi, Kenya, au Kantamanto mjini Accra, Ghana. Takriban asilimia 40 ya bidhaa hizi zinazoagizwa kutoka nje haziwezi kuvaliwa kabisa, na hivyo kuhamishia mzigo wa udhibiti wa taka za nguo kwa jamii.
Nguo nyingi zilitotengenezwa kwa kutumia poliesta na nailoni, huziba njia za maji za mijini, huchafua fuo za bahari, na zinapochomwa, hutoa gesi yenye sumu na kuchafua mazingira.
Katika makala ya leo tunaangazia jinsi biashara ya mitumba imegeuka tatizo kubwa la mazingira na kuharibu mifumo ikolojia.
Mon, 15 Jun 2026 - 248 - Usimamizi endelevu wa taka kwenye mazingira hauwezi kufanikiwa bila mchango wa wakusanyaji takaMon, 15 Jun 2026
- 247 - Kuna haja ya serikali za Afrika kukumbatia mfumo endelevu ya kukabili taka ngumu kwenye mazingira.
Tatizo la uchafuzi wa mazingira kutokana na taka ngumu, bado ni changamoto katika miji mingi barani Afrika.
Hata hivyo, hivi karibuni, kumekuwa na jitihada kwenye baadhi ya mataifa ambapo sasa nchi zimeanza kuwa na sheria na kanuni za kuhakkisha usimamizi endelevu wa taka, kwa kuwahusisha wazalishaji na waagizaji wa bidhaa.
Mon, 01 Jun 2026 - 246 - Kongamano la siku mbili jijini Nairobi latoa wito wa kubadili simulizi kuhusu maeneo ya nyanda za malisho(Rangelands)
Kwa muda mrefu maeneo ya nyanda za malisho yamekuwa yakitazamwa kama yaliotengwa na yasio na umuhimu, licha ya kuwa na mifumoikolojia muhimu na chanzo cha riziki kwa takriban watu bilioni mbili duniani, Pamoja na kuhifadhi theluthi moja ya hewa ya kaboni duniani.
Lakini sasa wadau wa mazingira, watunga sera, watafiti, wataalam na wawakilishi kutoka jamii za wafugaji baranai Afrika sasa wanatoa wito wa maeneo ya nyanda za malisho na jamii za wafugaji kutambuliwa.
Mon, 25 May 2026 - 245 - Juhudi za kijamii zilivyookoa msitu wa Karura uliokua umegeuka kuwa eneo la uhalifu
Nairobi ni mwenyeji wa msitu mkubwa wa mvua ulio salama ndani ya mipaka yake: Hifadhi ya Karura yenye ukubwa wa hekari 1,000 ni mapafu muhimu ya mji mkuu wa Kenya, katika kuchuja uchafuzi wa mazingira kwa mamilioni. Ilikuwa ishara ya ukosefu wa usalama, sasa ni mfano mkuu wa kimataifa wa uhifadhi unaoongozwa na jamii haswa shirika la marafiki wa Karura maarufu Friends of Karura.
Hata hivyo, msitu wa Karura unakabiliwa na changamoto za kina za kiikolojia. Miti ya kigeni inayokua haraka, uchafuzi wa mazingira wa mijini, magugu vamizi, na kuingiliwa kwa minajili ya upanuzi wa barabara na ujenzi wa miundombinu.
Ili kukabiliana na hili, juhudi kubwa za urejesho zinaendelea. Mpango wa utaratibu wa asilimia 60 unaendelea ili kubadilisha miti isiyo ya asili na spishi za urithi katika kurejesha udongo na bioanuwai.Urejeshaji huu unaoendelea hutumika kama mwongozo wa jinsi miji ya kisasa inaweza kurekebisha urithi wao wa asili.
Thu, 21 May 2026 - 244 - Nchini Colombia, mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu mafuta ya visukuku
Msikilizaji, juma moja lililopita, mawaziri kutoka karibu mataifa 50 duniani walikutana nchini Colombia kwa mkutano wa mazingira uliolenga kujadili mbinu za mataifa kuachana kikamilifu na nishati zinachafua mazingira ikiwemo gesi na mafuta.
Mjadala kuhusu mataifa kuachana na matumizi ya nishati chafu zinazochangia ongezeko la joto duniani, umekuwepo katika mikutano tofauti ya kimataifa ya mazingira, ikiwemo mikutano ya COP inayofanyika kila mwaka.
Tue, 12 May 2026 - 243 - Jamii katika maeneo kame nchini kenya zawezeshwa ili kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi.
Nchini Kenya, mzozo wa rasilimali katika jamii zinazopatikana katika maeneo kame ni changamoto ya muda mrefu, na kumekuwa na jitihada ya mashirika tofauti kuziwezesha jamii hizo kustahimili changamoto zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kupitia mradi wa IMARA, jamii ya wafugaji sasa wamegeukia ukulima wa aina tofauti ambao baadhi yao unawadsaidia hata kupata chakula ya mifugo wao.
Mon, 27 Apr 2026 - 242 - Sera za Mipango miji barani Afrika zinazingatia ustahimilivu wa majanga mijini?
Mkutano wa pili wa Umoja wa Afrika unaofahamika kama 'Jukwaa la Mijini Afrika (AUF) ulianzishwa kwa nia ya kuwezesha mazungumzo na uratibu wa ukuaji endelevu wa miji na makazi ya watu barani Afrika.
Pamoja na Maryam Wangeshi, msanifu wa majengo, tunaangazia matokeo ya mkutano huo na ikiwa mataifa ya Afrika yana mipangilio ilio bora katika kuwezesha miji yetu kustahimili majanga ya kimazingira.
Mon, 20 Apr 2026 - 241 - Ukulima wa mianzi katika kutunza mazingira ya mito nchini Kenya.
Mimea ya mianzi yaani Bamboo ni mojawapo ya mimea kote ulimwenguni inayoweza kupandwa katika mazingira tofauti kama vile sehemu tambarare au chemichemi.
Ukulima wa mianzi unaboresha mazingira kwa kuzuia mmomonyoko wa udongo, kurejesha rotuba kwa udongo haswaa sehemu zilizo karibu na mito na hata kama kitega uchumi.
Fri, 10 Apr 2026 - 240 - Manufaa ya ardhi oevu ya Ondiri kwa jamii ya kikuyu
Katika awamu ya kwanza tuliangazia uluhimu wa maeneo ya ardhi poevu katika mazingira, ikiwa ni pamoja na kutumika kama makazi ya aina tofauti ya spishi ya viumbe hai lakini pia ni mazalia ya samaki.
Sasa ardhioevu ya Ondiri ni nyumbani kwa zaidi ya spishi 90 za ndege, Kwa mfano, tulifanikiwa kumuona ndege aina ya Korongo ambao mara nyingi wao hutoroka katika ardhioevu ambayo mazingira yake yamechafuliwa.
Wed, 01 Apr 2026 - 239 - Uhifadhi wa kinamasi cha Ondiri mjini Kikuyu, nchini Kenya
Vijana katika shirika la uhifadhi la Marafiki wa ardhi oevu ya Ondiri, ambayo ni nyumbani kwa viumbe hai na bayoanuai yenye umuhimu katika mazingira. Katika mazingira, maeneo haya yanya faida kama vile, kufanya kazi kama sponji ya kunyonya hewa ukaa kutoka kwenye anga zaidi ya misitu ya mvua. Hutumika kama makazi ya aina tofauti ya spishi ya viumbe hai lakini pia ni mazalia ya samaki. Ardhi oevu pia hupunguza athari za mafuriko na kusafisha maji machafu.
Tue, 24 Mar 2026 - 238 - Matumizi ya mitego ya wadudu inayotumia sola yaboresha parachichi na mazingira
Wakulima wa Meru kaskazini mashariki mwa Kenya wanakumbatia matumizi ya mitego ya wadudu inayotumia nishati ya jua ili kukabiliana na false codling moth (FCM), mdudu anayeharibu mazao ya parachichi.
Eneo la kaskazi mashariki huzalisha kiwango kikubwa cha parachichi zinazouzwa ulaya na Asia Kupitia teknolojia hii, wakulima sasa wameanza kupata nafasi katika masoko ya nje....vile vile wamepunguza utegemezi wao kwa viuatilifu vya kemikali,hivyo kuongeza kipato cha wakulima.
Tue, 24 Feb 2026
Podcast simili a <nome>
El Partidazo de COPE COPE
Herrera en COPE COPE
La Linterna COPE
Dante Gebel Live Dante Gebel
Es la Mañana de Federico esRadio
La noche de Cuesta esRadio
La Trinchera de Llamas esRadio
Hondelatte Raconte Europe 1
Affaires sensibles France Inter
LEGEND Guillaume Pley
El colegio invisible OndaCero
La Rosa de los Vientos OndaCero
Les grands dossiers de l'Histoire par Franck Ferrand Radio Classique
Espacio en blanco Radio Nacional
Enquêtes criminelles RTL
Entrez dans l'Histoire RTL
Le grand récit RTL
Les Grosses Têtes RTL
L'Heure Du Crime RTL
Parlons-nous RTL
El Larguero SER Podcast
SER Historia SER Podcast
Todo Concostrina SER Podcast
Un Libro Una Hora SER Podcast
