Filtrer par genre

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

RFI Kiswahili

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

261 - Je unafahamu umuhimu wa kuzuia upotevu na uharibifu wa chakula?
0:00 / 0:00
1x
  • 261 - Je unafahamu umuhimu wa kuzuia upotevu na uharibifu wa chakula?

    Mwaka huu ni maadhimisho ya saba ya siku ya kimataifa ya kutoa hamasisho kuhusu utupaji na upotevu wa chakula, ambao unachangia kati ya asilimia 8–10 ya utoaji wa gesi joto

    Lengo la maendeleo endelevu nambari 12.3 linalenga kuona dunia ikipunguza  upot’evu na uharibufuwa chakula kwa nusu ifikapo mwaka 2030.

    Mon, 28 Sep 2026
  • 260 - Septemba 22, siku ya kimataifa ya kutotumia magari mijini

    Wananchi katika miji mbalimbali ya dunia wanahimizwa kuacha magari yao binafsi nyumbani na kukumbatia mbinu zingine za usafiri zilizo endelevu kama kutumia baiskeli au kutembea kwa miguu.

    Makala haya yanaangazia namna baiskeli za umeme zinaweza kuwa moja ya suluhu ya uchafuzi wa hewa kwenye miji unaotokana na sekta ya usafiri.

    Wed, 23 Sep 2026
  • 259 - Kenya: Wanaharakati watoa mapendekezo mapya dhidi ya plastiki zinazochafua mazingira

    Kenya inakabiliwa na changamoto ya plastiki zinazotumiwa mara moja tu kama vile mifuko inayotumiwa sokoni kupakia mboga ambazo huchangia katika uchafuzi wa mazingira licha ya kupigwa marufuku.

    Ni Kutokana na hili ambapo wanaharakati wa mazingira wamekuja na mapendekezo mapya ya kukabiliana na tatizo hili, mbali na suluhu la uchakataji.

    Moja ya matokeo ya mapendekezo haya ni kuiweka Kenya katika nafasi ya uongozi wa kikanda katika uvumbuzi wa mifumo ya kutumia tena bidhaa.

    Hellen Kahaso Dena kutoka shirika la Greenpeace Africa amechambua swala hilo. Sikiliza zaidi kwa kubofya.

    Mon, 14 Sep 2026
  • 258 - Kenya: Nyenzo(Tool) mpya inavyoanika matumizi ya ufadhili wa tabianchi Kenya

    Matumizi ya ufadhili wa hali ya hewa imekuwa swala kuu kwa wadau wa mazingira, kutokana na mianya ya ufuatiliaji.

    Nchini Kenya, shirika la Transparency International, sasa linajaribu kuziba mwanya uliopo ambapowakenya watakuwa wakifuatilia miradi na matumizi ya fedha hizi nchini humo kupitia jukwaa jipya la mtandaoni la Climate Finance Watch Tool.

    Wed, 26 Aug 2026
  • 257 - Kenya: Ubunifu wa unaogeuza magugu maji kuwa mifuko ya kupakia bidhaa na matumizi mengine

    Kwa wavuvi katika ziwa Niavasha, kama vile Simon Macharia na Joseph Kimani, Magugu maji yamekuwa kero kwa muda mrefu, na wakati mwingine kuwasababishia hasara.

    Lakini sasa kutokana na ubunifu wa Joseph Nguthiri, kijana bingwa wa dunia wa Mazingira wa UNEP mwaka wa 2025, na mwanzilishi wa kampuni yaHyapak wavuvi wanaweza kujipatia kipato zaidi.

    Mon, 24 Aug 2026
Afficher plus d'épisodes