Filtrer par genre
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
- 312 - Kiwanda cha kusafisha mafuta Lamu: mwanzo wa mapinduzi ya nishati Afrika Mashariki?
Kenya inaagiza karibu mahitaji yake yote ya bidhaa za Petroli kutoka nje, hii ikiwa na maana kuwa bei na upatikanaji wa mafuta katika nchi hii, na kwa kiasi kikubwa katika ukanda unaweza kuathiriwa na mambo yanayotokea katika masoko ya kimataifa, hata hivyo habari njema ni kuwa bilionea wa Afrika Aliko Dangote anajenga kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lamu. Kwanini hatua hii ni muhimu? Tufuatilie
Wed, 30 Sep 2026 - 311 - Hormuz na Bab el-Mandeb: Njia za baharini zinazotikisa uchumi wa dunia.
Msikilizaji hebu fikiria mafuta unayoweka kwenye gari lako, bidhaa zinazofika kwenye maduka yetu kutoka Asia, mbolea inayotumika kwenye kilimo, au hata gharama ya kusafirisha kahawa na chai kutoka Afrika kwenda masoko ya nje, kwa namna moja au nyingine, sehemu ya uchumi huu inategemea bahari na kufungwa kwa njia ya Hormuz na sasa ile ya Bab el-Mandeb kunauweka uchumi wa dunia hatarini. Ungana nami kwenye makala ya wiki hii kufahamu zaidi.
Wed, 23 Sep 2026 - 310 - Maisha mapya: Jinsi akina mama vijana wanavyobadilisha ujuzi kuwa fursa
Nchini Kenya, suala la mimba za utotoni ni changamoto. Kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu ya taofa nchini Kenya kupitia utafiti wa mwaka 2022 asilimia 15 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 walikuwa wamewahi kupata ujauzito.
Katika makala ya Gurudumu la Uchumi wiki hii, tunaangazia namna akina mama hawa wanavyogeuza ujuzi, juhudi na fursa za kiuchumi kuwa njia ya kujitegemea na kuwajengea watoto wao maisha yenye matumaini zaidi.
Wed, 09 Sep 2026 - 309 - Umeme unaweza kuwa injini ya ukuaji wa uchumi Afrika Mashariki?
Wikendi iliyopita, Tanzania ilizundua rasmi Mradi wa Umeme wa Maji wa bwawa la Julius Nyerere, lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115. Mradi huu, uliogharimu takribani shilingi trilioni 7.45 za Tanzania sawa na karibu dola za Marekani bilioni 2.9, unaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme.
Katika Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunajiuluza Je, megawati hizi zitageuka kuwa uzalishaji, ajira, biashara na ukuaji wa uchumi?
Wed, 26 Aug 2026 - 308 - Goma: Wanawake wapambana na umaskini licha ya changamoto za usalama.
Msikilizaji katika mazingira ambayo migogoro na changamoto za kiuchumi zimeathiri maisha ya kila siku ya wananchi, wanawake wengi wamekuwa wakitafuta njia mbadala za kujipatia kipato na kuendesha familia zao.Hali hii inashuhudiwa katika mji wa Goma, mashariki mwa DRC, ambako baadhi ya wanawake wamegeukia ufugaji wa kuku kama njia ya kujikimu, hasa baada ya shughuli za baadhi ya taasisi za kifedha kutatizika katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa AFC-M23.
Wed, 19 Aug 2026 - 307 - Je, Nchi Inaweza Kuendelea Bila Dira ya Maendeleo?
Msikilizaji taifa linaweza kuishi siku moja baada ya nyingine bila kujua linaelekea wapi. Lakini taifa linalotaka kujenga uchumi imara, ajira bora na maisha bora kwa wananchi wake, linahitaji zaidi ya mipango ya leo, kwa kifupî linahitaji dira.
Kwenye makala ya wiki hii tunaangazia dira ya taifa ni nini.
Wed, 12 Aug 2026 - 306 - Sehemu ya Pili: Hatifungani ni nini na kwanini inakuhusuWed, 05 Aug 2026
- 305 - Hatifungani za serikali na hazina: Kwa nini zinahusu kila mwananchi?Wed, 29 Jul 2026
- 304 - Migogoro ya kimataifa inavyoathiri uchumi wa wananchi Afrika
Katika Makala haya hivi leo tunajadili uhusiano kati ya siasa za kimataifa na uchumi wa wananchi wa Afrika, mara yingi tunasikia taarifa za vita, migogoro ya kisiasa au mivutano kati ya mataifa makubwa kama Urusi na Ukraine, Mashariki ya Kati, au migogoro inayovuruga usafirishaji wa bidhaa duniani. Kuzungumzia hili, hivi leo nimemualika Safari Fungo, mtaalamu wa masuala ya uchumi, utangamano wa kikanda na biashara za kimataifa akiwa Dar es Salaam, Tanzania.
Wed, 22 Jul 2026 - 303 - Sarafu za kidijitali ‘Cryptocurrency’ uwekezaji wa kisasa wenye fursa na hatari
Katika miaka ya hivi karibuni, sarafu za kidijitali maarufu kama cryptocurrency zimezidi kuvutia watu wengi duniani. Wapo waliopata faida kubwa, lakini pia wapo waliopoteza fedha nyingi kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu hizo.
Leo katika Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza: Je, sarafu za kidijitali ‘cryptocurrency’ ni uwekezaji wa kweli, au ni uwekezaji wenye hatari kubwa ambao watu wanapaswa kuuchukulia kwa tahadhari?
Wed, 15 Jul 2026 - 302 - Kodi na Maendeleo: Je, tunapata thamani ya kodi tunazolipa?Wed, 08 Jul 2026
- 301 - Je, kukopa kunasaidia ukuaji wa uchumi au kunaleta hatari za siku zijazo?
Msikilizaji nchi nyingi za Afrika Mashariki zimeendelea kukopa ili kufadhili maendeleo, na huku wadau wengine wakisema mikopo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi, Wengine wanaonya kuwa madeni yanapoongezeka kupita kiasi, serikali hulazimika kutumia fedha nyingi kulipa madeni hayo badala ya kuboresha huduma muhimu kama vile afya, elimu na ajira.
Katika Makala ya Gurumu la Uchumi hivi leo, tunauliza: Je, deni la taifa ni daraja la maendeleo au ni mzigo unaoweza kuathiri uchumi wa Afrika?
Wed, 24 Jun 2026 - 300 - Kutoka taslimu hadi kidijitali: Namna simu zinavyobadili mfumo wa malipo Afrika
Ufanyaji biashara na utumaji wa fedha kwa njia ya simu za kiganjani barani Afrika unakua kwa kasi, pochi za simu zimerekodi takriban asilimia 19 ya uingiaji wa pesa kwenye eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku wastani wa gharama ya utumaji pesa ukishuka hadi karibu asilimia 3.54 hii ni kwa mujibu wa benki ya dunia.
Kwanye Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunaangazia matumizi ya telknolojia za malipo ya mtandaoni hasa kupitia simu, jina langu ni Emmanuel Makundi, Karibu.
Wed, 10 Jun 2026 - 299 - Sekta ya maua Kenya yatikiswa na gharama na kuyumba kwa masoko ya kimataifaThu, 04 Jun 2026
- 298 - Umuhimu wa bara la Afrika kufanya biashara za ndaniWed, 03 Jun 2026
- 297 - Mkutano wa 'Africa Forward' una maana gani kwa mustakabali wa Afrika
Tarehe 11 na 12 ya wiki ijayo, Jiji la Nairobi, Kenya litakuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa kihistoria wa ‘Africa Forward’ kati ya Ufaransa na Afrika, mkutano ambao unafanyika kwenye nchi inazungumza Kingereza, ambapo viongozi wa Afrika, wafanyabiashara na wabunifu vijana kutoka Afrika na Ufaransa watakongamana kwa siku mbili.
Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi hivi leo tunaangazia uhusiano mpya kati ya Ufaransa na Afrika, wachambuzi wetu ni Ali Mkimo na Hamduni Marcel.
Wed, 06 May 2026 - 296 - Akili unde na mustakabali wa uchumi wa Afrika: Fursa mpya kwa vijana wabunifu
Katika kipindi ambacho Afrika inaendelea kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii, teknolojia ya Akili Unde (AI) inaibuka kama nyenzo muhimu ya kuleta mabadiliko. Kutoka kilimo hadi afya, na kutoka elimu hadi utawala bora, ubunifu wa kidijitali unaanza kubadilisha namna matatizo ya muda mrefu yanavyotatuliwa.Katika makala hii, tunazungumza na Kevin Obote kijana mbunifu wa teknolojia ambaye anatumia AI kuunda suluhisho zinazolenga mazingira halisi ya Afrika.
Wed, 22 Apr 2026 - 295 - Kwa nini vikwazo vya usafirishaji ni kizuizi kikubwa cha biashara Afrika Mashariki
Kupitia ripoti iliyozinduliwa juma hili na shirikisho la wazalishaji nchini Kenya, inaonyesha kuwa kusafirisha bidhaa katika njia muhimu za biashara za Afrika bado ni ghali na haitabiriki, ambapo wakati mwingine hugharimu hadi dola 7,000 za Marekani kwa kontena moja kati ya Nairobi na Lusaka. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tumezungumza na Tobias Alando, mkurugenzi mtendaji wa shirikisho la wamiliki wa viwanda nchini Kenya.
Wed, 01 Apr 2026 - 294 - Uwazi kwenye ubinafsishaji wa mashirika ya uma ni muhimu kwa maendeleo
Msikilizaji Katika miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi za Afrika Mashariki zimekuwa zikifanya mageuzi makubwa ya kiuchumi. Mojawapo ya mageuzi hayo ni ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Leo tunajiuliza, Je, ubinafsishaji ni kweli unasaidia uchumi kukua, au serikali inapaswa kubaki na umiliki wa mashirika muhimu?
Wed, 11 Mar 2026 - 293 - Vita ya Iran: Afrika imejipangaje kukabiliana na athari za kiuchumiWed, 04 Mar 2026
- 292 - Ushirikishwaji wa wanawake katika sekta za kiuchumi chanzo cha ukuaji wa uchumi
Benki ya Dunia inasema hata katika nchi zenye sheria za kisasa kuhusu usawa kazini, nchi hizo zimeshindwa kuzitekeleza, hadi sasa hakuna nchi iliyofikia kiwango cha juu cha usawa kazini, n ani asilimia kidogo tu ya wanawake wanaishi kwenye nchi zenye angalau sheria bora, huku mataifa 70 ikiwemo Misri, Madagascra na Somalia zikipiga hatua katika kuboresha mazingira ya usawa kati yam waka 2023 na 2025.
Wed, 25 Feb 2026
Podcasts similaires à Gurudumu la Uchumi
El Partidazo de COPE COPE
Herrera en COPE COPE
La Linterna COPE
Dante Gebel Live Dante Gebel
Es la Mañana de Federico esRadio
La noche de Cuesta esRadio
La Trinchera de Llamas esRadio
Hondelatte Raconte Europe 1
Affaires sensibles France Inter
LEGEND Guillaume Pley
El colegio invisible OndaCero
La Rosa de los Vientos OndaCero
Les grands dossiers de l'Histoire par Franck Ferrand Radio Classique
Espacio en blanco Radio Nacional
Enquêtes criminelles RTL
Entrez dans l'Histoire RTL
Le grand récit RTL
Les Grosses Têtes RTL
L'Heure Du Crime RTL
Parlons-nous RTL
El Larguero SER Podcast
SER Historia SER Podcast
Todo Concostrina SER Podcast
Un Libro Una Hora SER Podcast
Autres podcasts de Affaires
BFM Bourse BFM Business
C'est votre argent BFM Business
UNBX, le podcast de la réussite UNBX
Les experts BFM Business
Entendez-vous l'éco ? France Culture
Choses à Savoir ÉCONOMIE Choses à Savoir
QR Podcast QR PODCAST
Freedom to be Happy Sukriti Vadhera Kohli
Sound Laws of Success Podcast James Karl Butler
Le marché de François-Régis Gaudry France Inter
Dubai Owen
Culture IA BFM Business
La librairie de l'éco BFM Business
BFM Crypto BFM Business
Tanguy Pastureau maltraite l'info France Inter
Grands Leaders, les leçons de l'Histoire Radio Classique
Info éco FRANCE 24
مُلخص كتاب Podcast Record
Tout pour investir BFM Business
UNBX, le podcast de la réussite UNBX
