Filtrar por gênero
MAELEZO PODCASTS

Sikiliza MAELEZO PODCASTS (Podcasts za Kiswahili kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Tanzania) kupata taarifa na matukio mbalimbali nchini Tanzania. Idara ya Habari (MAELEZO) ipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ikiwa na jukumu la kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera, mipango na miradi ya maendeleo vinavyotekelezwa na Serikali kwa wananchi, kusimamia vyombo vya habari hasa magazeti na machapisho na kuishauri Serikali juu ya Sera na Sheria za habari.
- 58 - Utafiti Kuhusu Kiwango cha Pombe na Athari Katika Moyo
Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Richard Kisenge kuhusu ushiriki wa JKCI katika michuano ya AFCON ambapo taasisi hiyo inatarajia kutoa huduma kwa teknolojia ya kisasa na mpya barani Afrika, pia kutoa taarifa ya utendaji na mafanikio ya taasisi katika kuwafikia wananchi. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Sat, 24 Oct 2026 - 57 - Simulizi ya Mpiga Picha Aliyefanya Kazi na Marais Wote Tanzania
Mazungumzo na Mzee Hokororo, Mtumishi Mstaafu wa Idara ya Habari-MAELEZO anayesimulia historia ya Idara, safari ya sekta ya habari nchini mpaka kuanzishwa kwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na safari yake ya umahiri katika upigaji picha iliyomuwezesha kufanya kazi na marais wa awamu tofauti kuanzia Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hadi awamu ya sita. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Fri, 16 Oct 2026 - 56 - Huduma ya Mama Kujifungua Bila Maumivu Yaanza Kutolewa Tanzania
Dkt. Lugano Wilson, Daktari Bingwa wa usingizi na ganzi tiba kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodona anatupitisha zaidi kwenye hduma hii kuanzia historia yake, sababu za kuanzishwa kwa huduma hii ya uzazi, faida yake, malengo ya huduma hii kwa miezi sita ya kwanza na usalama wa huduma hii kitaalamu ikifahamika epidural. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Fri, 02 Oct 2026 - 55 - Fursa za Kimawasiliano Zilizopo Nchini Hivi Sasa
Mzungumzo na Mhandisi Asajile John kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu hatua iliyopigwa na Tanzania kimawasiliano, fursa za kimtandao zilizopo kwa sasa. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Fri, 25 Sep 2026 - 54 - Si kila mtu au kila mahali unaweza kurusha droni, kwa nini?
Mazungumzo na mkaguzi wa droni (Drone Inspector), Bw. Ibrahim Abdallah kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ambaye ameweka wazi kuhusu taratibu za usajili wa droni na utaratibu wa kufuata ili mtu aweze kupata leseni ya kurusha droni. Unaweza kutazama Episode hii pia kupitia chaneli ya Youtube "Maelezo TV". Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Fri, 18 Sep 2026 - 53 - Je, Tanzania atahodhi mchezo gani AFCON, Ufunguzi au fainali?
Mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa kama vile maandalizi ya AFCON 2027, mipango ya serikali kuhusu mvua za El Nino, maadili na miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Mon, 14 Sep 2026 - 52 - Tahadhari ya Mvua za El Niño Kuanzia Oktoba, 2026
Kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) juu ya uwepo wa mvua kubwa za El Nino, kupitia Maelezo Podcast ili kupata ufafanuzi tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a ambaye anaeleza kuhusu mvua hizi zinavyotokea na tahadhari za kuchukua. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Mon, 31 Aug 2026 - 51 - Aina Tatu za Saratani Zinazoathiri Maisha ya Wengi Nchini.
Katika kujenga uelewa kuhusu ugonjwa wa saratani, kupitia Maelezo Podcast tumemualika Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dkt. Chrispin Kahesa, tumezungumza kuhusu saratani na namna inavyoathiri makundi mbalimbali katika jamii, jitihada za kuzuia na tiba ya saratani. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Sat, 29 Aug 2026 - 50 - Changamoto ya Afya ya Akili, ni Akina Nani Waathirika Zaidi?
Kupitia Maelezo Podcast tunajadili kuhusu afya ya akili kwa kumualika Daktari Veronica Lyimo, Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili kutoka Taasisi ya Afya ya Akili Tanzania, ambaye anatupitisha kwenye visababishi vya changamoto ya afya ya akili, dalili, utofauti wa ugonjwa wa akili na changamoto ya afya ya akili na namna ya kukabiliana na changamoto hizo. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Fri, 21 Aug 2026 - 49 - Kwanini ni marufuku kutunza kwa kutupa fedha chini?
Mazungumzo na Bw. Atufigwege Mwakabalile, Afisa Mwandamizi wa Benki kutoka Benki Kuu Tanzania (BOT) kuhusu sheria ya fedha nchini na marufuku iliyotilewa ya kutotunza fedha kwa kutupa chini. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Mon, 17 Aug 2026 - 48 - Sheria ya Kuasili Mtoto (Child Adoption) Tanzania
Kupitia MAELEZO PODCASTS leo tunazungumza na Bi. Ludovicka Samare, Afisa Ustawi Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, anatupitisha kwenye utaratibu na Sheria ya kuasili mtoto (Child Adoption), nchini Tanzania Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Fri, 31 Jul 2026 - 47 - Elimu ya Hisa, Hati Fungani, Uwekezaji
Mazungumzo na Imani Mhingo, Mtaalamu wa Elimu ya Fedha na Mitaji ya dhamana kutoka Benki ya CRDB kuhusu elimu ya hisa; nani anatakiwa kuwa na hisa? uvumi upi usio wa kweli kuhusu hisa? Angalizo na namna ya kutengeneza faida kwa njia ya umiliki wa hisa. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Fri, 24 Jul 2026 - 46 - Tiba ya Upandikizaji wa Uume kwa Wanaume
Dkt. Rugakingira kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma anatupitisha kwenye huduma hii iliyojizolea umaarufu ya upandikizaji wa uume kwa wanaume wenye changamoto za uzazi. Amejibu kuhusu nani anaweza kupandikiziwa uume, gharama na matarajio baada ya huduma. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Fri, 17 Jul 2026 - 45 - Ukweli Kuhusu Faida za Vyama vya Ushirika
Mazungumzo na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania, Bw. Florian Haule kuhusu ushirika na ukweli wake vile umesaidia kuinua uchumi wa Watanzania tangu zamani hadi sasa. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Mon, 13 Jul 2026 - 44 - Fursa kwa Watanzania Kuelekea AFCON 2027
Kuelekea Michuano ya AFCON 2027 ambayo Tanzania anatarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano hii mikubwa Barani Afrika, tumemualika Bw. Allan Allex, Afisa Michezo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Afisa Programu wa Baraza la Michezo la Afrika Kanda ya Nne. Tumezungumza kuhusu fursa zilizopo, zinazoendelea kujitokeza na zinazotarajiwa kujitokeza katika michuano hiyo na namna Mtanzania anaweza kunufaika nazo. Support the show Msemaji...
Fri, 10 Jul 2026 - 43 - Siri ya Tarehe 7 Julai na Historia ya Tanzania Iliyowafanya UNESCO kuichagua kuwa Siku ya Kiswahili Duniani
Mazungumzo na Profesa Rehema Erasto., Mhadhiri wa Kiswahili kutoka Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma kuhusu historia ya siku ya Kiswahili Duniani, nafasi ya lugha za kijamii (makabila), makosa kwenye lugha ya kiswahili na namna ya kusahihisha. Mazungumzo haya yanapatikana pia kupitia chaneli ya Youtube ya Maelezo TV. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Mon, 06 Jul 2026 - 42 - Kwanini Kongamano la Kiswahili Ufaransa na si kwingine? Majibu ya Msemaji Mkuu wa Serikali
Gerson Msigwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; na Msemaji Mkuu wa Serikali akitoa majibu ya ni kwanini Kongamano la Kiswahili la Pili la Kimataifa limefanyika nchini Ufaransa na si kwingineko. Pia tumezungumzia asili ya makongamano ya kiswahili ya kimataifa, fursa na ushiriki wa wananchi katika makongamano haya. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Tue, 30 Jun 2026 - 41 - Kuelekea Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa, Paris - Ufaransa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inatarajia kufanya Kongamano la pili la kimataifa la Kiswahili kati ya Julai 4 - 7, 2026, jijini Paris, Ufaransa. Tumezungumza na Bw. Tito Lulandala, Afisa Utamaduni Mwandamizi, kutoka Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Maandalizi ya Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa kuhusu maendeleo ya Kiswahili, fursa zilizopo, ajenda mu...
Thu, 18 Jun 2026 - 40 - Fursa, Ushirikiano kati ya Algeria na Tanzania: Balozi Matinyi
Mheshimiwa Balozi Mobhare Matinyi akizungumza mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho wa kibalozi kwa Mheshimiwa Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, katika hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya Algiers tarehe 10 Juni, 2026. Balozi Mobhare Matinyi anayeiwakilisha Tanzania nchini Algeria, ametoa wito kwa Watanzania kutumia fursa za ushirikiano mzuri baina ya nchi hizi kufaidika katika nyanja mbalimbali. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Fri, 12 Jun 2026 - 39 - Balozi Kombo Aeleza Umuhimu wa Ziara ya Rais Samia katika Kuimarisha Mahusiano ya Tanzania na Urusi
Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Urusi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 7 Juni, 2026. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Mon, 08 Jun 2026 - 38 - Miaka 10 ya BMH: Jinsi Hospitali ya Benjamin Mkapa Ilivyobadilisha Huduma za Kibingwa Tanzania
Hospitali ya Benjamin Mkapa ni hospitali ya rufaa ya kanda iliyopo jijini Dodoma, iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa huduma za kibingwa ambazo kwa sasa zipo 20 na ubingwa bobezi zipo 17 kwa wananchi wa Tanzania na nchi jirani. Tangu kuanza kutoa huduma zake, hospitali hiyo imeendelea kukua kwa kasi na kuwa miongoni mwa vituo vinavyoongoza nchini katika huduma za matibabu ya moyo, figo, saratani, upasuaji mkubwa pamoja na huduma za kisasa za uchujaji damu na upandikizaji wa figo. Aidha, ...
Thu, 04 Jun 2026 - 37 - Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 (Mei 4, 2026)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Mei 4, 2026, bungeni, jijini Dodoma. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Wed, 27 May 2026 - 36 - Hotuba ya Mhe. Rais Samia na Mhe. Rais, Paul Kagame, Mei 03, 2026
Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame, amefanya ziara ya siku moja nchini Tanzania, akizungumza na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu ushirikiano na kukuza uchumi wa pande zote, Mei 3, 2026. Viongozi hawa walikubaliana kuendelea kukuza biashara na uwekezaji kwa kuondoa vikwazo vya kikodi, ili kunufaika na masoko ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA). Support the show Msemaji Mkuu wa S...
Sun, 24 May 2026 - 35 - Hotuba ya Rais, Dkt. Samia Kwenye Kongamano la Biashara Baina ya Tanzania na Kenya, Mei 4, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Kenya (Tanzania & Kenya Business Forum 2026), tarehe 04 Mei, 2026, JNICC, jijini Dar es Salaam ambapo kongamano hili lilihudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Samoei Ruto. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Fri, 22 May 2026 - 34 - Elimu kuhusu ugonjwa wa Seli Mundu na Dkt. Catherine Mhando
Pata ufahamu sahihi kuhusu chanzo, dalili, matibabu pamoja na kinga ya ugonjwa wa Seli Mundu (Sickle Cell) na Dkt. Catherine Mhando wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Support the show Msemaji Mkuu wa Serikali
Sat, 25 Apr 2026 - 33 - Buriani Benjamin mkapa (Julai 25, 2020)Thu, 15 Jan 2026
- 32 - Elimu kwa umma kuhusu zoezi la SENSA YA WATU NA MAKAZI (2022)
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni kwa ajili ya mipango jumuishi na maendeleo endelevu ya nchi na yataongeza uwazi katika kugawa rasilimali zilizopo kuendana na uwiano wa idadi ya watu katika ngazi zote za utawala. Halikadhalika matokeo yatatumika na Serikali na wadau wengine katika kufuatilia na kutathmini mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikijumuisha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Dira ya Zanzibar 2050, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2021/22 - 20...
Thu, 15 Jan 2026
Podcasts semelhantes a MAELEZO PODCASTS
El Partidazo de COPE COPE
Herrera en COPE COPE
La Linterna COPE
Panda Show - Sin Picante El Panda Zambrano
Es la Mañana de Federico esRadio
La noche de Cuesta esRadio
La Trinchera de Llamas esRadio
Hondelatte Raconte Europe 1
Affaires sensibles France Inter
LEGEND Guillaume Pley
El colegio invisible OndaCero
La Rosa de los Vientos OndaCero
Les grands dossiers de l'Histoire par Franck Ferrand Radio Classique
Espacio en blanco Radio Nacional
Entrez dans l'Histoire RTL
Le grand récit RTL
Les Grosses Têtes RTL
L'Heure Du Crime RTL
Parlons-nous RTL
El Larguero SER Podcast
Nadie Sabe Nada SER Podcast
SER Historia SER Podcast
Todo Concostrina SER Podcast
Un Libro Una Hora SER Podcast