Nach Genre filtern
- 267 - Kenya : Polisi watuhumiwa kuwaua raia kiholela zaidi ya raia 118 wakiuawa mwaka 2023
Makala haya tunaangazia ripoti ya mashirika ya kiraia nchini kenya kuhusu vifo vya kiholela vinavyodaiwa kutekelezwa na polisi.
Ripoti hiyo inakaria kwa mwaka uliopita wa 2023, polisi waliwaua zaidi ya raia 118, masharika hayo yakisema licha ya mauwaji hayo ya raia hakuna hatua ambazo zimechukuliwa na serikali waathibu wahusika.
Hata hivyo masharika hayo yanasema idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na mwaka 2022 ambapo zaidi ya watu 130, wanadaiwa kuuawa na polisi nchini Kenya.
Mauwaji haya ya raia kwa mjibu wa masharika haya yanayojumuisha, shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International , tume ya haki za binadamu nchini Kenya , na masahrika mengine, ni kwamba yalitekelezwa wakati wa operesheni ya uhalifu.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Thu, 02 May 2024 - 266 - Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu
Unamkumbuka kiongozi wa wa dini Paul Mackenzi anayetuhumiwa kwa kushiwishi waumini wake kususia chakula hadi kufa, ili kukutana na yesu nchini Kenya.
Baada ya takriban mwaka moja na mwezi mmoja wa serikali ya Kenya kufukua miili ya waumini waliofariki na kuzikwa katika msiku wa Shakahola na kuzifanyia uchuguzi wa vina saba yaani DNA, serikali sasa imeanza kutoa miili hiyo kwa familia za jamaa waliofariki.
Serikali ya Kenya kupitia kwa mwanapatholijia wake mkuu daktari Johason Odour, imesema ilichukuwa muda mrefu kutoa miili kwa family zilizoathirika kutokana na kuharibika kupita kiasi.
Soma piaWazee wauliwa pwani ya Kenya kwa tuhuma za kwamba ni wachawi
Katika haya mwanahabari Diana Wanyonyi kutoka pwani ya Kenya alihudhuria mazishi ya baadhi ya waathiriwa wa mafunzo ya itikadi kali Paul Mackenzie na anasimulia hali ilivyokuwa
Thu, 25 Apr 2024 - 265 - Haki ya watoto chotara shirika la African Futures Lab linataka Ubelgiji kuwatambua
Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za binadamu la African Futures Lab, lenye makao yake jijini Brussels nchini Ubelgiji, lilizindua ripoti kushinikiza watoto chotara na mama zao kutoka nchini DRC, Rwanda na Burundi, kulipwa fidia, kutambuliwa kuwa raia wa Ubelgiji na kupata haki nyingine za msingi.
Wakati wa ukoloni wa nchi ya Ubelgiji kwa nchi hizo za maziwa makuu, wakoloni, wanaume wazungu kutoka nchini Ubelgiji, waliwachukua kwa nguvu wanawake kutoka DRC, Rwanda na Burundi na kuwapeleka Ubelgiji na kuwazalisha, huku wengine wakifanyiwa hivyo wakiwa kwenye nchi zao.
Makala haya yameandiliwa na Benson Wakoli
Soma piaHaki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)
Wed, 17 Apr 2024 - 264 - Madaktari nchini Kenya wagoma kuishinikiza serikali kuzingatia haki zao
Muungano wa madaktari, wauza dawa na madakrati wa meno, KMPDU, ambao unawakilisha zaidi ya wanachama 7,000 uliitisha mgomo Machi 15, ili kudai mishahara iliyocheleweshwa, pamoja na kupewa ajira mara moja kwa madaktari wanafunzi.Mgomo ambao umesababisha hali ya sintofahamu kwa wagonjwa kwa takribani wiki tatu sasa.
Tue, 16 Apr 2024 - 263 - DRC : Jamii ya mbilikimo yalilia serikali kuwapa nafasi kuhudumu serikalini
Nchini DRC , mara kwa mara jamii ya mbilikimo ama wambute kama wanavyo julikana katika taifa hilo, wamekuwa kilalamikia kile wanachodai kubaguliwa na raia kutoka jamii ya wabantu nchini DRC.
Jamii hiyo imekuwa ikidai wameachwa nje kwenue nyadhifa kama vile viongozi wa nyumba 10 hadi cheo cha rais, wanadai hakuna raia kutoka jamii hiyo anashikilia wadhifa wowote serikali.
Moja ya mashirika za haki za binadamu kwa jina " Greats lakes Human Right Programme" katika ripoti ya hivi karibuni , imesema kwamba sheria nzuri zipo za kuwalinda na kutetea haki za mbilikimo , ila utekelezaji wake ndio umekuwa changamoto.
Mwandishi wetu wa Beni nchini DRC Eriksson Luhumbwe amezungumza na raia hao kutoka jamii ya mbilikimo na kutuandalia ripoti hii, skiza.
Wed, 10 Apr 2024 - 262 - Haki za raia wa mataifa ya Afrika wanaofanya kazi katika mataifa ya ughaibuni.Thu, 04 Apr 2024
- 261 - Kenya : Dhuluma za kijinsia na mrundiko wa kesi mahakamaniTue, 19 Mar 2024
- 260 - DRC: Waasi wa CODECO wadaiwa kutekeleza mauwaji ya kikabila
Mashariki mwa DRC , vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vinazidi kushika kasi hasa mauwaji ya raia, vinavyoendelezwa na makundi ya waasi.
Makundi haya ni yale ya ndani na ya kigeni kutoka mataifa jirani ya Uganda "ADF" Sudan kusini "Bororo" na Jamuhuri ya Afrika ya kati "LRA" .
Wapiganaji Hao sasa hivi wame fikia hata kiwango cha kushambulia vituo vya afya na kuwazika raia wakiwa hai.
Makala haya yamlika hali wilayani Djugu mkowani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC , ambapo zaidi ya raia 800 wameuawa kikatili na kundi lenye silaha la CODECO katika kipindi cha miaka 6 , kwa mujibu wa mashirika ya kirai mashariki mwa DRC .
Fri, 15 Mar 2024 - 259 - Kenya: siku ya wanawake duniani nini Kipya?
Siku ya wanawake duniani huadimishwa kila kila tarehe nane ya mwezi machi, kuangazia mchango wa mwanamke katika jamii na pia changamoto zinazowakumba wanawake.
Kauli mbiu ya maadimisho ya mwaka huu, nchini Kenya ni uwekeza kwa wanawake ili kufanikisha maendeleo kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Fri, 08 Mar 2024 - 258 - Kenya : Wasanii walilia haki yao
Muungano wa wanamziki nchini Kenya (MAAK), unamtaka mwenyekiti wa Shirika la Hakimiliki ya Muziki ya Kenya, Ezekiel Mutua kujiuzulu kutokana na kile wanadai amekuwa akipora peza za wamziki.
Kupitia taarifa muungano huo, unasema Mutua amekuwa akijilimbikizia pesa za wasanii huku wahusika wakiendelea kusalia maskini.
Ili kufahamu zaidi skiza makala haya.
Sat, 02 Mar 2024 - 257 - Haki ya kutali Africa bila vikwazoWed, 21 Feb 2024
- 256 - Valentine : Haki ya wanaume na wanawakeSat, 17 Feb 2024
- 255 - Kenya : Viongozi wa dini wapinga ushoga
Kwenye haya tunajadili hatua viongozi wa dini nchini Kenya kulitaka bunge kuanza uchuguzi wa haraka kuhusiana na madai kwamba kuna njama ya makusudi kueneza sera za ushoga nchini Kenya.
Viongozi hao wa dini wanadai kwamba kuna mpango wa ambao tayari umepangwa kupinga vita dhidi ya mashoga na wasagaji, na watu wanaodai kutetea haki za mashoga, hulka ambayo inaenda kinyume kabisa na maadili ya jamii za kiafrica.
Kufahamu zaidi skiza makala haya.
Fri, 09 Feb 2024 - 254 - DRC : Je haki za raia zilikiukwa kipindi cha uchaguzi?Sat, 03 Feb 2024
- 253 - Haki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)
Katika haya tunaangazia haki ya watoto kupata elimu ambapo utaskia kwa wadau mbalimbali walioazisha kutuo cha elimu cha Fizi kinatoa elimu ya somo la kifaransa nchini Kenya kwa watoto wakimbizi kutoka nchini DRC , Rwanda na Burundi.
Kituo hiki kilianzishwa mwaka 2014 lengo likiwa kuwasaidia watoto wakimbikizi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ili kuendelea kujifunza na kuendeleza tamaduni ya lugha ya Kifaransa,hasa ikizingatiwa kwamba nchini Kenya raia wengi huzungumza kingereza na Kiswahili.
Fri, 26 Jan 2024 - 252 - Human watch yatahumu jamii ya kimataifa kwa kukosa kusadia Sudan
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch limetuhumu jamii ya kimataifa kwa kukosa kushughulikia vita vinavyoendelea nchini Sudan.
Kwa mjibu wa ripoti ya kila mwaka ya shirika hilo, jamii ya kimataifa haijafanya juhudi za kutosha kushawishi pande hasimu nchini Sudan Kusitsha vita.
Ili Kufahamu negi zaidi skiza makala haya.
Sun, 21 Jan 2024 - 251 - Hali ya haki za binadamu nchini Kenya na Tanzania
Visa vya raia kupotea na kisha kuonekana baada ya siku kadhaa nchini Kenya si vipya tena, hili likishuhudia mara kwa mara nchini Kenya, polisi wakituhumiwa kuhusika kwenye visa hivi
lakini je tume ya haki za binadamu nchini Kenya inafahamu hili? na je nchini Tanzania hali ya hali za haki za binadamu ipo je?
Maswali haya yanajibiwa ndani ya makala.
Tue, 09 Jan 2024 - 250 - Mashirika ya misaada ya kibinadamu yakumbwa na uhaba wa fedha
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR, limeonya kuwa mashirika ya misaada yanakabiliwa na uhaba wa fedha, na kwamba yanahitaji dola milioni 400 kufikia mwisho wa mwaka huu.
Katika kongamano la siku tatu kuhusu wakimbizi huko Geneva, Wiki iliyopita, Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi, alisema asilimia 75 ya wakimbizi wanaishi katika nchi maskini na zile zinazoendelea.
Grandi ameiomba jamii ya kimataifa kutofumbia macho mamilioni ya waliokimbia makazi yao huko Ukraine, Sudan, Syria, Afghanistan, na vile vile DRC.
Kuzungumzia haya na pia haki za wakimbizi kwa ujumla, Bi. Faith Kasina, msimamizi wa UNHCR ukanda wa Afrika mashariki alizungumza na George Ajowi.
Tue, 19 Dec 2023 - 249 - Ipo siku watu wanaoishi na walemavu watapata nafasi sawa katika jamii
Tarehe 3 Disemba mwaka huu, dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya watu wanaoishi na ulemavu. Siku hii iliasisiwa mwaka 1992 na umoja wa mataifa.
Nchini Kenya, siku hii ilifana sana huku sherehe ikiandaliwa katika maeneo mbalimbali. Katika eneo la Dagoreti, jijini Nairobi, tulikutana na Grace Wanjiku Maina ambaye alizaliwa na ulimavu lakini amejizatiti na kufanikiwa sana katika Jamii.
Licha ya kuishi na Ulemavu Grace ni mshinda wa tuzo ya urembo ya kinadada wanaotumia vitu vya magurudumu, tuzo alioyoishinda 2017 na 2018, vile vile ni mwakilishi wa watu wanaoishi na ulemavu katika eneo la Dagoreti na pia mkurugenzi katika wakfu wa Sweet Aroma foundation, wakfu ambao unawatetea walemavu. Katika makala ya leo nimeanza kwa kumuuliza, nini kimebadilika tangu aliposhinda taji la urembo la miss Wheelchair miaka 6 iliyopita?
Mon, 11 Dec 2023 - 248 - Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kushinikiza serikali kutekeleza maamuzi ya mahakama
Mtandao wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Kibinadamu za Kiafrika (NHRI)kwa ushirikiano na Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) pamoja na Taasisi ya Sheria ya Kibinadamu na Haki za Kibinadamu ya Raoul Wallenberg iliyo na makao yake makuu nchini Sweden iliandaa warsha ya kutathmini miradi kuhusu mafunzo ya Haki za Kibinadamu barani Afrika na ufuatiliaji wa jinsi ya Kutekeleza mapendekezo ya Maamuzi.
Katika makala haya Petronila Mukaindo, naibu mkurugenzi wa KNCHR anatoa twasira kamili ya changamoto na hatua za kutetea haki za kibinadamu nchini kenya na katika mataifa mengine.
Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
Mon, 04 Dec 2023 - 247 - Siku 16 za mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake
Kila mwaka dunia hutumia siku 16 kuadhimisha mapambano ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto .
Umoja wa mataifa huongoza kampeni hii na hufanyika kuanzia tarehe 25 Novemba na kumalizika tarehe 10 Desemba ya kila mwaka kwa ajili ya kupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.
Siku hiyo ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1991 na tangu wakati huo zaidi ya asasi 6,000 kwa zaidi ya nchi 187 hushiriki katika maadhimisho haya.
Nchini Kenya katika eneo la Kibra baadhi ya kinadada wamethibitisha kuwa visa vya dhulma bado vipo na kati ya wanawake 5 wawili wamedhulumiwa kisaikologia na hata kingono .
Ili kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Fri, 01 Dec 2023 - 246 - Manufaa ya mitandao, mwandishi Paul Braine anasimulia
Ujio wa mitandao umekuja na masaibu mengi tu, licha ya manufaa mengi, katika makala haya Benson Wakoli anakamilisha mahojiano yake na mwandishi wa kitabu cha Parenting in Dijital Era, yaani uzazi kipindi hiki cha kidijiti, bwana Paul Braine kuhusu manufaa na hasara za mitandao.
Ili kufahamu mengi skiza makala haya.
Tue, 28 Nov 2023 - 245 - Haki ya watoto kipindi hiki cha kidigiti
Paul Braine mwandishi wa vitabu nchini Kenya, amechapisha kitabu kinachoangazia haki za watoto kulelewa kipindi hiki cha dijitali na jukumu la wazazi kuwalea watoto kipindi hiki.
Benson Wakoli amezungumza naye kuangazia haki za kila pande yaani watoto na wazazi katika makala haya ya Jua Haki Zako.
Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
Tue, 07 Nov 2023 - 244 - Kenya : Serikali yaendesha bomoabomoa kwenye ardhi inayodai kuwa yake
Katika makala haya tunajadili hatua ya serikali nchini kenya kubomoa makaazi ya raia wanaodiwa kujenga nyumba zao kwenye ardhi ya serikali, ambayo inamilikiwa na kampuni ya simiti ya East African Portland cement.
Kwa mjibu wa kampuni ya simiti ya East African Portland cement, raia waliojenga kwenye ardhi inayodai kuwa yake walikuwa wameonya dhidi ya kujenga kwenye ardhi hiyo.
Ili kuelewa mengi zaidi skiza makala haya.
Fri, 27 Oct 2023
Podcasts ähnlich wie Jua Haki Zako
- Conversations ABC listen
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Dateline NBC NBC News
- 財經一路發 News98
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- アンガールズのジャンピン[オールナイトニッポンPODCAST] ニッポン放送
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 吳淡如人生實用商學院 吳淡如
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR