Filtrer par genre
- 3587 - Nani hasa anaiendesha Australia, na una nafasi gani humo | Jinsi Australia Inavyofanya kazi
Je, unajua nani anaweza kusaidia kuhusu kibali cha biashara, tatizo la upangaji nyumba, au msaada wa kifamilia? Kupitia hadithi za Fedele, Carol na Abeer, fahamu jinsi ngazi tatu za serikali nchini Australia zinavyofanya kazi. Jua majukumu ya serikali za mitaa, serikali za majimbo au maeneo ya utawala, na serikali kuu (ya shirikisho), pamoja na mahali pa kupata msaada.
"How Australia Works" ni podikasti ya SBS inayotumia hadithi halisi na maelezo ya wazi kukusaidia kuelewa jinsi serikali inavyofanya kazi nchini Australia, jinsi sheria zinavyotungwa na kubadilishwa, na jinsi unavyoweza kutoa maoni yako. Sikiliza mfululizo huu na upate matoleo mafupi zaidi katika lugha 60 kwenye ukurasa mkuu wa "How Australia Works".Mon, 28 Sep 2026 - 08min - 3586 - Uko tayari ndani ya mfumo | Jinsi Australia inavyofanya kazi
Je, serikali, sheria, na huduma za umma za Australia huathirije maisha yako ya kila siku? Kupitia matukio halisi, sehemu hii ya utangulizi ya mfululizo huu inakuonyesha pa kuanzia unapohitaji taarifa na msaada, pamoja na jinsi ya kupinga uamuzi.
"How Australia Works" ni podikasti ya SBS inayotumia hadithi halisi na maelezo ya wazi kukusaidia kuelewa jinsi serikali inavyofanya kazi nchini Australia, jinsi sheria zinavyotungwa na kubadilishwa, na jinsi unavyoweza kutoa maoni yako. Sikiliza mfululizo huu na upate matoleo mafupi zaidi katika lugha 60 kwenye ukurasa mkuu wa "How Australia Works".Mon, 28 Sep 2026 - 04min - 3585 - Travelling safely in rural and remote Australia - Australia Yafafanuliwa:Kusafiri kwa usalama katika maeneo ya vijijini na yaliyo mbali nchini Australia
Australia is a vast and diverse country to explore, but driving in rural and remote areas can involve conditions you may not encounter in cities. Knowing what to expect and how to prepare can help you travel more safely and confidently. - Australia ni nchi kubwa na yenye mambo mengi ya kuvutia ya kugundua, lakini kuendesha gari katika maeneo ya vijijini na yaliyo mbali kunaweza kuhusisha hali ambazo huenda usikutane nazo mijini. Kujua nini cha kutarajia na jinsi ya kujiandaa kunaweza kusaidia kusafiri kwa usalama zaidi na kwa kujiamini.
Mon, 28 Sep 2026 - 14min - 3584 - Mh Dkt Kosgei"Walemavu hawahitaji huruma, wanahitaji kulindwa kulingana na sheria na katiba ya Kenya"
Mh Dkt Jackson Kosgei ni Askofu mstaafu, na kwa sasa ana hudumu kama mjumbe aliyeteuliwa katika bunge la Kenya.
Sat, 26 Sep 2026 - 12min - 3583 - Taarifa ya Habari:Serikali ya Shirikisho yazingatia hatua zakisheria dhidi ya shirika la OpenAI kwa uvujaji wa taarifa za Medicare
Serikali ya Shirikisho inasema inazingatia hatua za kisheria dhidi ya OpenAI, baada ya mmoja wa mawakala wake kukiuka mfumo wa Medicare wa Australia mnamo Juni, wakati wa tathmini ya ndani ambapo mifumo yake ilikuwa ikitafiti matumizi ya matibabu ya umma.
Fri, 25 Sep 2026 - 14min - 3582 - Albert Mwangi Kuhusu African Australia film fest web
Wanachama wa Jumuiya zawa Afrika wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika ukumbi wa maarufu wa Opera House na Events Cinema Parramatta, kushiriki katika tamasha ya kila mwaka ya filamu zaki Afrika kuanzia 3-6 Septemba.
Fri, 25 Sep 2026 - 07min - 3581 - Noel"ripoti hii ina ushahidi wamambo mazuri tunayo fanya kuliko wanasiasa na vyombo vya habari vinavyo sema"
Shirika la African Australian Advocacy Centre (AAAC), lili zindua ripoti inayo weka wazi michango yawa Australia wenye asili ya Afrika kwa taifa hili usiku wa Jumamosi 19 Septemba 2026.
Fri, 25 Sep 2026 - 07min - 3580 - Dkt Jane "kuna wakati ukienda dukani mlinzi anakufuata fuata, tofauti na wateja wengine ambao si weusi"
Shirika la African Australian Advocacy Centre, lili zindua ripoti inayo weka wazi michango yawa Australia wenye asili ya Afrika kwa taifa hili usiku wa Jumamosi 19 Septemba 2026.
Tue, 22 Sep 2026 - 05min - 3579 - Taarifa ya Habari:Wachumi wasema ripoti ya Serikali kuhusu Vizazi inaonyesha kuwa uchumi utazidi kutegemea ukuaji wa tija katika miongo ijayo
Wanauchumi wanasema kuwa Ripoti ya hivi karibuni ya Serikali kuhusu Vizazi (Intergenerational Report) inaonyesha kuwa uchumi utazidi kutegemea ukuaji wa tija katika miongo ijayo.
Tue, 22 Sep 2026 - 13min - 3578 - Harrison "inabidi tupeleke tamasha hili katika zingine za kanda hili"
Wanachama wa Jumuiya zawa Afrika wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika ukumbi wa maarufu wa Opera House na Events Cinema Parramatta, kushiriki katika tamasha ya kila mwaka ya filamu zaki Afrika kuanzia 3-6 Septemba.
Tue, 22 Sep 2026 - 12min - 3577 - Taarifa ya Habari: Wito watolewa kutokomeza unyanyasaji wa nyumbani nchini Australia
Ripoti mpya kati ya vizazi imetolewa leo, ikionyesha athari za bajeti ya serikali na mitazamo ya uchumi katika miongo minne ijayo.
Naibu Kamishna wa Polisi wa New South Wales Peter McKenna anasema matukio manne tofauti yanayodaiwa kuwa ya unyanyasaji wa nyumbani mwishoni mwa wiki iliyopita yanaonyesha uzito wa janga hilo nchini Australia. Katika tukio lililo ripotiwa katika eneo la Blue Mountains, mvulana wa miaka mitano alikufa, na ndugu zake wawili na mama yake mwenye umri wa miaka 42 walijeruhiwa vibaya baada ya kupatikana na majeraha ya kudungwa visu ndani ya gari katika eneo la Valley Heights.
Kenya imetetea makampuni ya ndani yanayoagiza mafuta yaliosafishwa chini ya makubaliano ya serikali kwa serikali, siku chache baada Kampala kudai kuwa mpango huo ulikuwa umetekwa na madalali hali iliyopelekea kupanda kwa bei ya mafuta nchini Uganda. Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa nishati nchini Kenya, Opiyo Wandayi, kampuni kubwa tatu za mafuta katika nchi za Ghuba zinazouza mafuta yake nchini Kenya, zilichagua kampuni za ndani katika mpango huo na kwamba ikiwa serikali ingesisitiza kuchagua makampuni hayo basi mpango huo ungekufa.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.Mon, 21 Sep 2026 - 05min - 3576 - Yaliyojiri Afrika: Human Rights Watch "Ukosefu wa uchunguzi wa kina na kufunguliwa mashtaka dhidi yawahusika kunaweza endeleza uhalifu nchini Kenya"
Shirika lakutetea haki za binadam la Human Rights Watch lime onya kuwa, makundi ya watu wenye silaha yame endesha mifululizo yamashambulizi dhidi ya mikutano yakisiasa na shughuli za mashirika yakiraia katika maeneo mbalimbali nchini Kenya.
Fri, 18 Sep 2026 - 07min - 3575 - Taarifa ya Habari:Serikali ya shirikisho inatetea hatua yake kali ya uhamiaji inayo imarisha sheria kwa wanafunzi wakimataifa na watalii
Serikali ya shirikisho inatetea hatua yake kali ya uhamiaji, ambayo inaimarisha sheria kwa wanafunzi wa kimataifa na watu ambao wako nchini kwa likizo, inalenga wanao baki nchini zaidi ya muda wa viza zao na wanaohama kutoka viza moja hadi nyingine, na inawapa kipaumbele wafanyakazi wenye ujuzi katika sekta muhimu.
Fri, 18 Sep 2026 - 14min - 3574 - SBS Learn Eng Ep 119 Jinsi yakuzungumza kuhusu mizio ya majaniFri, 18 Sep 2026 - 12min
- 3573 - Makala Leo:Ukandamizaji wa uhamiaji: Labor yaimarisha sheria za viza kwa wanafunzi na watalii
Serikali imefichua mpango wake wa kupunguza uhamiaji halisi wa nje ya nchi hadi watu 225,000 ifikapo 2028, kulingana na utabiri kutoka bajeti ya Mei.
Fri, 18 Sep 2026 - 13min - 3572 - Taarifa ya Habari:Wanafunzi wakimataifa kukabiliwa kwa mkakati wa uhamiaji, wenye sheria kali
Serikali ya shirikisho ime tangaza mabadiliko makubwa katika mfumo wa uhamiaji wa Australia, ikiimarisha sheria kuhusu ni nani anayeweza kuja nchini na ni nani anayeweza baki nchini.
#sbsaudiopodcastThu, 17 Sep 2026 - 06min - 3571 - Mh Dkt Kosgei afunguka kuhusu alipoanza kuamani kuwa ulemavu si kutoweza
Mh Dkt Jackson Kosgei ni Askofu mstaafu, na kwa sasa ana hudumu kama mbunge aliyeteuliwa katika bunge la taifa nchini Kenya.
Thu, 17 Sep 2026 - 18min - 3570 - What are Indigenous Protected Areas in Australia? - Australia Yafafanuliwa:Maeneo Yaliyolindwa yawatu wa Asili nchini Australia ni yapi?
National parks, nature reserves, marine sanctuaries and Indigenous Protected Areas protect different environments and operate under different rules. What makes an Indigenous Protected Area different, and how can you find out whether you are welcome to visit? - Hifadhi za taifa, hifadhi za asili, hifadhi za baharini na Maeneo Yaliyohifadhiwa ya Wenyeji hulinda mazingira tofauti na hufanya kazi chini ya sheria tofauti. Ni nini kinachofanya Eneo Lililohifadhiwa la Wenyeji kuwa tofauti, na unawezaje kujua kama unakaribishwa kupatembelea?
Tue, 15 Sep 2026 - 10min - 3569 - Taarifa ya Habari:Mageuzi ya sheria kuwasilishwa bungeni,kuweka mipaka ya kisheria kwa silaha za Australia na kuweka vikwazo kwa pesa za umma
Kifurushi cha mageuzi ya sheria kitawasilishwa katika Bunge la Shirikisho leo, ili kuweka mipaka ya kisheria kwa silaha za Australia na kuweka vikwazo kwa pesa za umma, uwekezaji na biashara zinazotumika kuunga mkono mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uvamizi haramu.
Tue, 15 Sep 2026 - 15min - 3568 - Yaliyojiri Afrika:Kamati itakayo fanyia kazi mchakato wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar yazinduliwa
Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amezindua Kamati ya Pamoja ya Majadiliano kati ya vyama vya CCM na ACT-Wazalendo, uteuzi huo wa wajumbe 10 unaashiria hatua mpya katika mchakato wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar.
Tue, 15 Sep 2026 - 07min - 3567 - Prostate cancer in Australia: Testing, treatment and support - Australia Yafafanuliwa:Saratani ya tezi dume nchini Australia: Upimaji, matibabu na usaidizi
About one in five Australian men will be diagnosed with prostate cancer in their lifetime. Understanding the prostate, your risk and the options for testing can help with early detection and treatment. In this episode of Australia Explained, learn about prostate cancer, PSA testing, treatment and support. - Karibu mwanaume mmoja kati ya watano wa Australia atagunduliwa ana saratani ya tezi dume katika maisha yake. Kuelewa tezi dume, hatari yako na chaguzi za kupima kunaweza kusaidia katika kugundua na kutibu mapema. Katika makala haya ya Australia Yafafanuliwa, jifunze kuhusu saratani ya tezi dume, upimaji wa PSA, matibabu na usaidizi.
Tue, 15 Sep 2026 - 12min - 3566 - Taarifa ya Habari:Serikali ya shirikisho yaendelea kukabiliana na shinikizo lakutangaza msimamo wayo kwa viwango vya uhamiaji nchini
Serikali ya shirikisho imekuwa chini ya shinikizo la kufafanua malengo yake kuhusu mipaka ya visa, Waziri wa Mambo ya Ndani Tony Burke akiahirisha hotuba ya Klabu ya Kitaifa ya Waandishi wa Habari mwezi Agosti ambako alitarajiwa kutangaza kupunguzwa kwa uhamiaji.
Fri, 11 Sep 2026 - 14min - 3565 - Makala Leo:Tunachojua kuhusu usalama wakimataifa miaka 25 baada ya tukio la 9/11
Ni miaka 25 tangu karibu watu 3,000 waliuawa katika mashambulizi ya Septemba 11, ambayo yalisababisha Vita dhidi ya Ugaidi vilivyoongozwa na Marekani na kuiingiza Australia katika vita nchini Afghanistan na Iraq.
Fri, 11 Sep 2026 - 12min - 3564 - Mumbi afunguka kuhusu mapokezi ya tamasha ya filamu zaki Afrika nchini Australia
Wanachama wa Jumuiya zawa Afrika wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika ukumbi wa maarufu wa Opera House na Events Cinema kushiriki katika tamasha ya kila mwaka ya filamu zaki Afrika kuanzia 3-6 Septemba.
Fri, 11 Sep 2026 - 05min - 3563 - Taarifa ya Habari:Upinzani wa mseto waomba maelezo zaidi kabla ya kura ya mageuzi ya sheria za mitandao ya kijamii zilizo imarishwa
Makampuni ya mitandao ya kijamii yanaweza kuwapa watumiaji chaguo la kuzima algoriti yao, chini ya rasimu za sheria zilizopangwa kufichuliwa na serikali wiki hii.
Tue, 08 Sep 2026 - 13min - 3562 - Yaliyojiri Afrika:Agizo la Rais Ruto lazua hofu miongoni mwa wahamiaji wenye asili ya Burundi
Nchini Kenya, ukosoaji umekuwa ukiongezeka tangu tangazo la Rais William Ruto Jumatano iliyopita. Alisema kwamba biashara ndogo ndogo zinazoendeshwa na wageni nchini Kenya lazima zifunge kuanzia Jumatatu, Septemba 7.
Tue, 08 Sep 2026 - 08min - 3561 - Makala Leo: Unachohitaji kujua kuhusu magonjwa ya msimu huu wa masika
Australia inapo ingia katika majira ya kuchipua, wataalamu wanawasihi watu wasiache kujilinda dhidi ya magonjwa ya msimu.
Tue, 08 Sep 2026 - 13min - 3560 - Taarifa ya Habari:Sera ya malipo ya uzeeni ya One Nation yakosolewa vikali
Chama cha One Nation kina kana kwamba sera yake mpya ya malipo ya uzeeni itasababisha uondoaji mkubwa wa malipo ya uzeeni, au kuongezeka kwa mfumuko wa bei.
Mon, 07 Sep 2026 - 04min - 3559 - Mumbi afunguka kuhusu maandalizi ya tamasha ya filamu zaki Afrika nchini Australia
Wanachama wa Jumuiya za Afrika wanao ishi jijini Sydney, New South Wales wana jiandaa kuhudhuria tamasha maalum.
Wed, 02 Sep 2026 - 12min - 3558 - Makala Leo: Dunia yamkumbuka gwiji wa muziki Dolly PartonFri, 28 Aug 2026 - 09min
- 3557 - Yaliyojiri Afrika: CCM yamtimua Dkt Emmanuel Nchimbi
Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM umemvua uanachama Emmanuel Nchimbi na kumpitisha Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, kujaza nafasi ya Makamu wa Rais.
Fri, 28 Aug 2026 - 07min - 3556 - Taarifa ya Habari:Australia yatoa kifurushi cha usaidizi cha dola milioni 5 kwa jamii zilizoathiriwa nchini Nepal
Serikali ya Australia inaanzisha kifurushi cha usaidizi cha dola milioni 5 kwa jamii zilizoathiriwa nchini Nepal, huku idadi ya Waaustralia waliopotea ikiongezeka hadi 39.
Fri, 28 Aug 2026 - 14min - 3555 - Makala Leo:Kwa nini baraza lamawaziri wakitaifa haliku gusa vituo vya mbadala vya data
Mkutano wa viongozi wa shirikisho, majimbo na wilaya ulimuacha Waziri Mkuu Anthony Albanese akikubali agizo la vituo vya data vinavyoweza kutumika tena.
Fri, 28 Aug 2026 - 10min - 3554 - Makala Leo:Wa Australia 34 miongoni mwa watu ambao wamepotea katika mafuriko Nepal
Takriban watu 160 wameuawa, na mamia wakiwemo watalii na Waaustralia 34 hawajulikani walipo, kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea kwenye mpaka wa Nepal na Tibet.
Fri, 28 Aug 2026 - 11min - 3553 - Taarifa ya Habari:Makumi yawa Australia hawajulikani waliko katika mafuriko nchini Nepal
Waziri Mkuu Anthony Albanese amethibitisha kuwa Waaustralia 34, hawajulikani walipo baada ya mafuriko makubwa ya ghafla kwenye mpaka wa Nepal-Tibet.
Thu, 27 Aug 2026 - 05min - 3552 - Yaliyojiri Afrika:Ujumbe maalum wafuatilia usitishaji mapigano DRC
Ujumbe wa kwanza wa aina yake umetumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatilia utekelezaji wa usitishaji mapigano kati ya jeshi la serikali na kundi la waasi la M23, linaloungwa mkono na Rwanda.
Tue, 25 Aug 2026 - 07min - 3551 - Taarifa ya Habari:Hospitali za New South Wales kupewa nafasi zaidi za matibabu
Hospitali za New South Wales zitapata nafasi zaidi za matibabu za muda mfupi ili kupunguza shinikizo kwa idara za dharura.
Tue, 25 Aug 2026 - 14min - 3550 - Makala Leo: Mrundikano wa visa za wenza unao waacha waaustralia katika sintofahamu
Mchakato mpya wa kipaumbele ambao unaweza fanya baadhi ya raia wa Australia, wasubiri kwa muda mrefu zaidi kwa wenzi wao kupokea visa umesababisha ukosoaji.
Tue, 25 Aug 2026 - 08min - 3549 - Makala Leo:'Usibofye kitu chochote':Jinsi barua pepe moja inavyoweza haribu biashara
Waaustralia wanapoteza mamia ya mamilioni ya dola kutokana na matapeli, huku matapeli wakizidi kutumia akili mnemba kuwadanganya waathiriwa wao.
Tue, 25 Aug 2026 - 07min - 3548 - Taarifa ya Habari:Ripoti mpya yaitaka Australia iboreshe usalama wa dawa na itoe wakalimani kwa jamii za tamaduni mbalimbali
Ripoti mpya imeangazia changamoto kubwa za usalama wa dawa zinazowakabili Waaustralia wenye tamaduni mbalimbali, na inatoa wito wa upatikanaji mkubwa wa taarifa na wakalimani wa dawa zinazotumia lugha nyingi.
Fri, 21 Aug 2026 - 13min - 3547 - Yaliyojiri Afrika:7 wafariki katika ajali ya helikopta Kenya
Watu saba, wakiwemo raia watano wa Marekani na mkuu wa ujasusi wa Ecuador, wamefariki baada ya helikopta ya watalii kuanguka karibu na Mlima Ololokwe, katika kaunti ya Samburu nchini Kenya.
Fri, 21 Aug 2026 - 07min - 3546 - Makala Leo:Mabadiliko ya NDIS yatakuathiri vipi?
Mamia ya maelfu ya watu watapoteza msaada kutoka NDIS, baada ya mabadiliko yanayolenga kupunguza ukuaji katika mpango huo kupitishwa ndani ya Seneti kwa uungwaji mkono wa Upinzani wa Mseto usiku wakuamkia.
Fri, 21 Aug 2026 - 12min - 3545 - Yaliyojiri Afrika:Askari pori watuhumiwa kwa mauaji ya raia Tanzania
Kituo cha sheria cha haki za binadamu Tanzania, kime eleza wasiwasi kuhusu madai ya watu kuuawa, kujeruhiwa au kupotea katika maeneo ya hifadhi nchini humo.
Tue, 18 Aug 2026 - 07min - 3544 - Taarifa ya Habari:Upinzani wa Mseto watishia kuzuia mabadiliko ya NDIS isipokuwa mwanya wa kodi ya mjane utakapofungwa
Upinzani wa Mseto unatishia kuzuia mabadiliko ya serikali kwa NDIS, isipokuwa serikali ya Labor iharakishe sheria ya kufunga kile kinachoitwa kodi ya mjane.
Tue, 18 Aug 2026 - 13min - 3543 - Makala Leo:Mageuzi ya NDIS yanatarajiwa kuwa sheria ila, wanaharakati wadai makato yata sababisha madhara
Mageuzi ya Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Watu Wenye Ulemavu yamejadiliwa katika Seneti, huku sheria ikitarajiwa kupitishwa wiki hii kwa msaada wa Upinzani wa Mseto.
Tue, 18 Aug 2026 - 16min - 3542 - Can you pick fruit from someone's garden? - Australia Yafafanuliwa:Je, unaweza chuma matunda kutoka bustani ya mtu?
Walking through an Australian suburb, you might spot everything from curry leaves and lemons to tomatoes and herbs growing in front gardens or on verges. But is it legal to pick it? This guide explains when it's legal to pick produce, why permission matters, and how community gardens offer another way to grow your own food. - Ukitembea katika kitongoji cha Australia, unaweza ona kila kitu kuanzia majani ya kari na limau hadi nyanya na mimea inayokua katika bustani za mbele au kwenye ukingo. Lakini je, ni halali kuvivuna? Mwongozo huu unaelezea wakati ni halali kuvuna mazao, kwa nini ruhusa ni muhimu, na jinsi bustani za jamii zinavyotoa njia nyingine ya kukuza chakula chako mwenyewe.
Tue, 18 Aug 2026 - 10min - 3541 - Taarifa ya Habari:Wafanyakazi wa kusambaza vyakula kuongezewa mshahara kuanzia leo
Takriban idadi yawa Australia 250,000 wanaosafirisha vyakula kutoka hotelini na dukani kwa ajili ya kujikimu, wanatarajiwa kupokea mshahara wa chini kisheria kwa mara ya kwanza.
Mon, 17 Aug 2026 - 05min - 3540 - Makala Leo:Serikali kuwekeza mamilioni katika nyumba za waathiriwa wa unyanyasaji wa majumbani; lakini je, inatosha?
Mgogoro wa makazi ukiendelea, vurugu za kifamilia na majumbani (DFSV) ndio sababu kuu ya wanawake na watoto kuondoka nyumbani kwao na kukosa makazi.
Sat, 15 Aug 2026 - 11min - 3539 - SBS Learn Eng Ep 117 Jinsi yakuzungumza kuhusu kukopa vitabuFri, 14 Aug 2026 - 15min
- 3538 - Taarifa ya Habari:Ripoti ya mwisho kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa na Serikali kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu itawasilishwa Bungeni
Ripoti ya mwisho kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa na Serikali kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu itawasilishwa Bungeni leo. Uchunguzi huo ulizinduliwa katika mwezi Mei ili kuchunguza mapendekezo ya Serikali, ya kuokoa karibu dola bilioni 38 kwa kipindi cha miaka minne.
Fri, 14 Aug 2026 - 15min - 3537 - Yaliyojiri Afrika: Uganda na Tanzania za zindua ushirikiano wa nishati
Bandari ya Tanga itakuwa kitovu muhimu cha nishati katika jumuiya ya Afrika Mashariki, chini ya ushirikiano mpya wa nishati uliozinduliwa kati ya serikali ya Uganda na Tanzania.
Fri, 14 Aug 2026 - 06min - 3536 - Makala Leo:Sensa imekwisha ila, bado hauja chelewa kama hauja jaza fomu yakoFri, 14 Aug 2026 - 06min
- 3535 - Taarifa ya Habari:Serikali yawahakikishia watu kwamba Sensa itakuwa salama
Serikali inawahakikishia watu kwamba Sensa itakuwa salama, kufuatia visa vya hivi karibuni vya roboti za AI kufanya ujambazi na uvunjaji wa data katika mashirika makubwa.
Tue, 11 Aug 2026 - 13min - 3534 - Yaliyojiri Afrika:Wanariadha wa Uganda watoweka Scotland
Mabondia wanne wa timu ya Uganda, wametoweka baada yakufeli kujitokeza kwa safari zao za ndege zakurejea nyumbani, baada ya kushiriki katika michezo ya jumuiya yamadola mjini Glasgow.
Tue, 11 Aug 2026 - 07min - 3533 - Makala Leo: Watetezi wa ulemavu waomba mlinzi nakuonya kuhusu 'athari kubwa' mageuzi yanapokaribia
Watetezi wa ulemavu wanaihimiza serikali kufikiria upya mabadiliko ya Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu unao julikana kama NDIS, kabla ya kura ya bunge inayokaribia kuhusu mageuzi yaliyopendekezwa.
Tue, 11 Aug 2026 - 09min - 3532 - Taarifa ya Habari:Wafanya biashara waomba ushirikiano na serikali kabla ifanye mabadiliko katika uhamiaji
Vikundi vya wafanyabiashara vinaihimiza serikali ya shirikisho kushirikiana nao, katika mashauriano kabla ya mabadiliko yoyote makubwa kutangazwa kuhusu sera ya uhamiaji.
Mon, 10 Aug 2026 - 06min - 3531 - Taarifa ya Habari:Ofisi ya takwimu ya Australia yahimiza wanao ishi katika nyumba zenye watu wengi wasiwe na hofu kushiriki katika sensa
Usiku wa sensa ukikaribia, maafisa wa Ofisi ya Takwimu ya Australia wanawahimiza watu wanao ishi katika makaazi yenye watu wengi sana, wasiwe na hofu yakushiriki kwa sababu hapatakuwa athari yoyote ya kisheria.
Fri, 07 Aug 2026 - 12min - 3530 - What are my rights if stopped by police in Australia? - Australia Yafafanuliwa:Haki zangu ni zipi kama nitasimamishwa na polisi nchini Australia?
Police officers have a range of operational powers they can exercise under legislation, including to ask questions, give ‘move on’ directions and conduct searches. Here’s what you need to know about your basic rights and obligations in a police interaction. - Maafisa wa jeshi la polisi wana mamlaka mbalimbali ya kiutendaji ambayo wanaweza kuyatumia chini ya sheria, ikiwa ni pamoja na kuuliza maswali, kutoa maelekezo ya 'kutoka ulipo' na kufanya upekuzi. Haya ndiyo unayohitaji kujua kuhusu haki na wajibu wako wa msingi katika mwingiliano wa polisi.
Fri, 07 Aug 2026 - 13min - 3529 - SBS Learn Eng Ep 116 Jinsi yakuzungumza kuhusu kumtembelea daktari wa wanyamaFri, 07 Aug 2026 - 15min
- 3528 - Taarifa ya Habari:Mfanyabiashara afariki mjini Melbourne baada ya tukio linalo shukiwa kutekelezwa na wezi
Mfanyabiashara mmoja wa duka mjini Melbourne amefariki baada ya kushambuliwa alipokuwa akijaribu kuzuia kundi la vijana walio kuwa waki iba dukani.
Fri, 07 Aug 2026 - 05min - 3527 - Yaliyojiri Afrika: DRC yaadhimisha GENOCOST
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi, ameongoza kumbukumbuku ya mauaji ya GENOCOST jijini Kinshasa, inayofanyika kila tarehe 2 mwezi Agosti.
Tue, 04 Aug 2026 - 07min - 3526 - Taarifa ya Habari:Mamia ya watu wakimbia mapigano Tigray na kuingia Sudan
Mamia yawa Ethiopia kutoka eneo la kaskazini mwa Tigray, wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Sudan katika siku mbili zilizopita, wakikimbia mapigano karibu na mpaka.
Tue, 04 Aug 2026 - 13min - 3525 - Makala Leo:Australia inakabiliwa na 'tsunami ya uharibifu' mkubwa kutokana na mlipuko wa virusi vya homa ya ndege H5
Jimbo la Kusini Australia huenda linakabiliwa na tukio la kwanza la vifo vingi vya wanyamapori nchini Australia linalohusishwa na homa ya ndege ya H5N1.
Tue, 04 Aug 2026 - 11min - 3524 - Makala Leo:Benki ya Hifadhi yasema wa Australia wengi hawa elewi jinsi viwango vya riba vinavyofanya kazi
Kiwango cha mfumuko wa bei nchini Australia kimepungua, lakini shinikizo la bei la msingi linabaki kuwa juu sana.
Tue, 04 Aug 2026 - 08min - 3523 - Taarifa ya Habari
Mdhibiti wa ushindani [[ACCC]] ameombwa na serikali ya shirikisho kufuatilia vituo vya mafuta kwa matukio yoyote ya kupunguzwa kwa bei - sasa kwa kuwa punguzo la muda la ushuru wa mafuta limeisha.
Visa 74 vya aina ya H-5 ya homa ya ndege vimethibitishwa nchini Australia.Hiyo inajumuisha uthibitisho wa tukio la kwanza la vifo vingi humu nchini kutokana na virusi hivyo Kusini mwa Australia.
Mji wa Ceuta mwishoni mwa juma haukuonekana tena kama jiji lililokuwa na wasiwasi, lakini wakazi bado walikuwa wameshtushwa na matukio ya wiki. Wengi wa wahamiaji 60,000 walioingia Ceuta wamerudi Morocco.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.Mon, 03 Aug 2026 - 05min - 3522 - Taarifa ya Habari:Kiongozi wa Victoria, ajiuzulu baada ya siku kadhaa za shinikizo dhidi ya uongozi wake
Jacinta Allan amejiuzulu kama Kiongozi wa Victoria, akisema ni uamuzi sahihi kwa Wa-Victoria. Tangazo hilo limekuja nusu saa tu baada ya changamoto inayotarajiwa ya uongozi katika mkutano uliopangwa wa chama cha wabunge, kuashiria kurudi kwa bunge la jimbo.
Tue, 28 Jul 2026 - 14min - 3521 - Australia Yafafanuliwa:Tamasha ya Garma ni nini, na kwa nini ni muhimu?
Kila mwaka, maelfu ya watu husafiri kwenda katika jamii ya kijijini kaskazini mashariki mwa Arnhem Land katika Eneo la Kaskazini.
Tue, 28 Jul 2026 - 10min - 3520 - Makala Leo: Jacinta Allan akataa kujiuzulu, pambano la uongozi wa chama cha Labor cha Victoria likiongezeka kasi
Kiongozi wa Jimbo la Victoria, Jacinta Allan, anasema atapambana na changamoto ya uongozi inayokuja baada ya viongozi wa mirengo tafuati ndani ya chama cha Labor, kukutana na kukubaliana kwamba amepoteza uungwaji mkono wa wengi katika mkutano wao.
Tue, 28 Jul 2026 - 11min - 3519 - Taarifa ya Habari: Kiongozi wa Victoria asisitiza hajiuzulu!
Kiongozi wa jimbo la Victoria, Jacinta Allan, anasema hatajiuzulu kutoka wadhifa wake, miezi minne kabla ya uchaguzi wa jimbo hilo.
Mon, 27 Jul 2026 - 05min - 3518 - Yaliyojiri Afrika:Kenya yapokea tani 4.5 zavifaa vya matibabu vya Ebola kutoka India
Kenya imepokea shehena ya kwanza ya tani 4.5 za vifaa vya matibabu kutoka kwa serikali ya India, ili kuimarisha uwezo wa nchi kujiandaa kukabiliana na uwezekano wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Sat, 25 Jul 2026 - 07min - 3517 - Taarifa ya Habari: Hatua ya Marekani kuongeza ushuru kwa mauzo ya nje ya Australia yazua ukosoaji
Utawala wa Trump umeongeza ushuru kwa mauzo ya nje ya Australia kutoka asilimia 10 hadi 12.5, huku kiwango kipya kikianza kutumika alasiri ya leo Ijumaa.
Fri, 24 Jul 2026 - 13min - 3516 - Makala Leo:Nini cha kutarajia kutoka kwa mfumo mpya wa tahadhari ya dharura wa Australia
Australia inajiandaa kuanzisha mfumo mpya wa kitaifa wa tahadhari ya dharura, ulioundwa kutoa tahadhari muhimu haraka na kwa uhakika zaidi wakati wa majanga.
Fri, 24 Jul 2026 - 15min - 3515 - Makala Leo:China yaambia Australia iache kuzungumzia Bahari ya Kusini mwa China wakati mvutano ukiongezeka katika Mkutano wa ASEAN
Mkutano wa Kikanda wa ASEAN unakamilika mjini Manila, ambapo Australia imeibua wasiwasi kuhusu hatua za kijeshi za China katika eneo hilo.
Fri, 24 Jul 2026 - 10min - 3514 - Taarifa ya Habari:Waziri Mkuu ataka chama cha Labor, kijitolee kupunguza shinikizo za gharama ya maisha
Waziri Mkuu Anthony Albanese, amesisitiza kujitolea kwa chama chake kupunguza shinikizo la gharama la maisha katika mkutano wa kitaifa wa chama tawala.
Thu, 23 Jul 2026 - 06min - 3513 - Yaliyojiri Afrika:Kituo chakujitenga cha Ebola nchini Kenya cha wapokea wamarekani 7 kutoka DRC
Wahudumu7 wamisaada kutoka wamarekani walikuowa wakisaida kupambana na Ebola DRC, wamewekwa katika kituo cha karantini nchini Kenya.
Thu, 23 Jul 2026 - 07min - 3512 - SBS Learn Eng Ep 115 Jinsi yakuzungumza kuhusu kufanya kazi ya ziadaTue, 21 Jul 2026 - 11min
- 3511 - Taarifa ya Habari:Waziri Wong aelekea katika kongamano lamawaziri wa mambo ya nje wa ASEAN kuimarisha uhusiano wa Australia na nchi wanachama
Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong anatarajiwa kwenda Ufilipino kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Asia Mashariki na Jukwaa la Kikanda la ASEAN.
Tume ya Dhamana na Uwekezaji ya Australia inasema imepata rekodi ya dola milioni 830 katika amri za adhabu za kiraia wakati wa Mwaka wa Fedha wa 2025-2026. Tume hiyo ilianzisha chunguzi zaidi ya 250, ambazo zilisababisha hatia 25 za jinai na watu 11 kuhukumiwa kifungo cha gerezani.
Karibu watu 930 wamefariki dunia kutokana na Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hii ikiwa ni kulingana na Wizara ya afya nchini humo. Vifo hivyo vimerekodiwa miongoni mwa visa 2,344 vya maambukizi vilivyothibitishwa hadi siku ya Jumamosi imesema wizara hiyo hii leo. Vifo vipya vilirekodiwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, idadi ya juu kabisa kuwahi kurekodiwa kwa siku moja.
Meli ya mafuta yenye bendera ya Tanzania imetekwa nyara na maharamia wanaoshukiwa kuwa wa Somalia katika pwani ya Yemen, vimebaini vyanzo vya usalama na maafisa wa eneo hilo kuhusu tukio hilo. Meli hiyo imehamishwa hadi majini katika eneo la Bari kaskazini mashariki mwa Somalia, kulingana na maafisa wa eneo hilo.Tue, 21 Jul 2026 - 13min - 3510 - Australia Yafafanuliwa:Kijana wangu anaweza anza kufanya kazi lini nchini Australia?
Kuanza kazi ya muda mfupi kunaweza kuwa uzoefu wenye maana kwa kijana, kuongeza kujithamini kwake, kumsaidia kujifunza ujuzi mpya na kupata pesa zake za kwanza.
Tue, 21 Jul 2026 - 12min - 3509 - Makala Leo:Mazoezi muhimu yakimataifa yajeshi yaanza katika Wilaya ya Kaskazini
Zoezi kubwa zaidi la kimataifa la Jeshi la Anga la Australia, linaendelea katika Eneo la Kaskazini na litafanyika kwa wiki tatu zijazo.
Tue, 21 Jul 2026 - 07min - 3508 - Taarifa ya Habari:Greens wataka makampuni ya mawasiliano nchini kutoa huduma yakuaminika kwa wateja
Chama cha Greens kinatoa wito wa mageuzi ambayo kisheria yatahitaji kampuni zama wasiliano kama Telstra, Optus na Vodafone kutoa huduma ya kuaminika kwa wateja.
Mon, 20 Jul 2026 - 04min - 3507 - Makala Leo: Mitandao ya teknolojia yaambiwa irekebishe pengo za ulaghai wakujamiana
Kamishna wa Usalama Mtandaoni wa Australia anatoa tahadhari kuhusu ulaghai wa kingono mtandaoni, baada ya kupokea malalamiko zaidi ya 2,000 katika miezi sita tu.
Fri, 17 Jul 2026 - 11min - 3506 - Taarifa ya Habari:Watoto wa Australia kuanza kuamua katika shule ya msingi kama watafuata taaluma za sayansi na teknolojia kwa msaada wa wazazi
Utafiti mpya unaonyesha kuwa watoto wa Australia wanaweza kuanza kuamua katika shule ya msingi kama watafuata taaluma za sayansi na teknolojia wanapokuwa wakubwa, huku wazazi wakiwa na ushawishi zaidi kuliko walimu katika maamuzi hayo.
Fri, 17 Jul 2026 - 14min - 3505 - Makala Leo: Argentina na Uhispania zaishi ndoto zakipekee za Kombe la Dunia
Argentina na Uhispania wanaishi ndoto ya kipekee ya Kombe la Dunia, baada yakutinga fainali ya kombe hilo. Mjini Buenos Aires na Madrid, mashabiki wanachangia jinsi walivyopitia tamthilia, hisia na sherehe.
Fri, 17 Jul 2026 - 05min - 3504 - Taarifa ya Habari:Ombi latolewa kuharamisha matamshi ya chuki dhidi yawa Aboriginal na wakaazi wa Torres Strait
Kuna wito wa kuharamisha matamshi ya chuki dhidi yawa Aboriginal na watu kutoka Visiwa vya Torres Strait, huku vikao vikiendelea katika uchunguzi wa ubaguzi wa rangi wa Serikali ya Shirikisho huko Darwin.
Thu, 16 Jul 2026 - 05min - 3503 - Makala Leo:Ufaransa na Uhispania tayari kwa pambano la nusu fainali
Nusu fainali za Kombe la Dunia zimewadia, Ufaransa na Uhispania zikijiandaa kufufua moja ya ushindani mkubwa wa soka la kimataifa. Tunaangalia kwa karibu habari za hivi punde za timu hizo na kusikia kutoka kwa kambi zote mbili kabla ya pambano kubwa la kesho.
Tue, 14 Jul 2026 - 05min - 3502 - Taarifa ya Habari:Vyuo vikuu kukabiliwa na faini kubwa vikishindwa kupambana na ubaguzi wa rangi
Serikali ya Shirikisho inasema vyuo vikuu vinaweza kukabiliwa na faini ikiwa vitashindwa kupambana na ubaguzi wa rangi chini ya viwango vipya vilivyoanzishwa Jumatatu 13 Julai 2026.
Tue, 14 Jul 2026 - 13min - 3501 - Makala Leo:Kusini Australia yatoa mpango wakupiga marufuku wahalifu wa vurugu kutoka programu zakuchumbiana
Jimbo la Kusini Australia limefichua mpango wa kwanza wa kupiga marufuku vurugu za majumbani na wahalifu wa kujamiana kutoka kwa programu za kuchumbiana.
Tue, 14 Jul 2026 - 10min - 3500 - Makala Leo:Mashambulizi mapya yashuhudiwa Iran na Marekani zikibishana kuhusu kufunguliwa kwa Hormuz
Marekani na Iran zimebadilishana wimbi jingine la mashambulizi, huku mapigano yakiongezeka kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz yakisukuma makubaliano ya kidiplomasia ya mwezi uliopita karibu kuvunjika.
Tue, 14 Jul 2026 - 10min - 3499 - Taarifa ya Habari:Daglo na maafisa wengine wa RSF wahukumiwa adhabu ya kifo
Mahakama ya Kupambana na Ugaidi na Makosa Dhidi ya Taifa iliyoko mjini Port Sudan nchini Sudan, , imemhukumu kifo kiongozi wa kundi la wanamgambo wa RSF, Mohamed Hamdan Daglo pamoja na maafisa wengine 15 wa RSF.
Mon, 13 Jul 2026 - 05min - 3498 - Yaliyojiri Afrika: Usalama waimarishwa katika mitaa ya Tanzania
Usalama unaendelea kuimarishwa katika miji mikubwa ya Tanzania, maafisa wa Polisi na Jeshi wenye silaha wakifanya doria.
Fri, 10 Jul 2026 - 07min - 3497 - Mbappé aiweka Ufaransa katika nusu fainali
Ufaransa imetinga nusu fainali ya Kombe la Dunia, baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Morocco. Kylian Mbappé amefunga mabao nane sawa na Lionel Messi, wakati Ousmane Dembélé akikamilisha ushindi huo.
Fri, 10 Jul 2026 - 04min - 3496 - Taarifa ya Habari:Polisi wachunguza kama kifo katika jimbo la Kusini Australia, kina husishwa na kupotea kwa huduma za Telstra Jumatano
Polisi wanachunguza kama kifo kinahusishwa na kupotezwa kwa huduma ya Telstra kote nchini Jumatano. Wapelelezi wa Kusini Australia wamethibitisha mtu mmoja alifariki katika hospitali ya kanda Jumatano, lakini polisi hawakuwa wamearifiwa kuhusu kifo hicho.
Fri, 10 Jul 2026 - 14min - 3495 - Australia Yafafanuliwa: Sensa ya 2026: Unacho stahili jua kuhakikisha una hesabiwa
Sensa ya 2026 itafanyika Jumanne tarehe 11 Agosti na kila mtu nchini Australia usiku huu lazima ahesabiwe.
Fri, 10 Jul 2026 - 12min - 3494 - Makala Leo: Waziri Mkuu Albanese aendeleza msukumo wake wakidiplomasia katika Pasifiki
Waziri Mkuu Anthony Albanese ameweka ratiba kabambe ya mkataba mpya kamili na Visiwa vya Solomon, akisema angependa kuuona ukikamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Fri, 10 Jul 2026 - 11min - 3493 - Taarifa ya Habari:Unyanyasaji wa kingono unaendelea kutumiwa kama silaha ya kivita DRC
Mamlaka katika jimbo la Kusini Australia, zimethibitisha kisa cha pili cha homa ya ndege aina ya H5 katika jimbo hilo.
Thu, 09 Jul 2026 - 06min - 3492 - Chiry"wasichana wenzangu njooni tuboreshe afya zetu kupitia mpira"
Jamii ya wakenya wanao ishi mjini Sydney, NSW walishuhudia historia ikiandikwa jioni ya Jumapili 28 Juni 2026 timu mpya ya mpira wa miguu ya kina dada ilipo cheza mechi yao ya kwanza katika uwanja wa Rydalmere.
Wed, 08 Jul 2026 - 09min - 3491 - Uhispania na Ubelgiji za tinga robo fainali wakati Ronaldo aaga Kombe la Dunia
Uhispania na Ubelgiji zimefuzu kwa robo fainali, wakati ndoto za Kombe la Dunia za wenyeji Marekani na Ureno ya Cristiano Ronaldo ziki gonga miamba.
Tue, 07 Jul 2026 - 04min - 3490 - Taarifa ya Habari:Ofisi ya Takwimu ya Australia yazindua kampeni ya tamaduni mbalimbali kabla ya Sensa ya mwezi ujao
Ofisi ya Takwimu ya Australia imezindua kampeni ya tamaduni mbalimbali kabla ya Sensa ya mwezi ujao, ikijumuisha matangazo katika lugha 28 tofauti.
Tue, 07 Jul 2026 - 14min - 3489 - Makala Leo: Wiki ya NAIDOC ni nini, na nini kimejificha nyuma ya kauli mbiu ya mwaka huu?
Maadhimisho ya Wiki ya NAIDOC ya Kitaifa yanafanyika kote nchini Australia wiki hii, kwa ajili ya kusherehekea na kutambua historia, utamaduni na mafanikio ya watu wa Asili na wakaazi wa Visiwa vya Torres Strait.
Tue, 07 Jul 2026 - 11min - 3488 - Makala Leo: Makampuni makubwa ya mtandao wakijamii yatetea sera zao mbele ya Tume ya Kifalme
Kampuni kubwa ya mtandao ya kijamii, Meta, ilifika mbele ya Tume ya Kifalme kuhusu Unyanyasaji wa Wayahudi na Uwiano wa Kijamii jana Julai 6, ikitetea rekodi yake ya kukomesha matumizi mabaya mtandaoni.
Tue, 07 Jul 2026 - 08min
Podcasts similaires à SBS Swahili - SBS Swahili
El Partidazo de COPE COPE
Herrera en COPE COPE
La Linterna COPE
Dante Gebel Live Dante Gebel
Es la Mañana de Federico esRadio
La noche de Cuesta esRadio
La Trinchera de Llamas esRadio
Hondelatte Raconte Europe 1
Affaires sensibles France Inter
LEGEND Guillaume Pley
El colegio invisible OndaCero
La Rosa de los Vientos OndaCero
Les grands dossiers de l'Histoire par Franck Ferrand Radio Classique
Espacio en blanco Radio Nacional
Enquêtes criminelles RTL
Entrez dans l'Histoire RTL
Le grand récit RTL
Les Grosses Têtes RTL
L'Heure Du Crime RTL
Parlons-nous RTL
El Larguero SER Podcast
SER Historia SER Podcast
Todo Concostrina SER Podcast
Un Libro Una Hora SER Podcast
Autres podcasts de Société et Culture
Conversations ABC Australia
Casefile True Crime Casefile Presents
Forensic Files HLN
The Diary Of A CEO with Steven Bartlett DOAC
Ukraine: The Latest The Telegraph
Unravel ABC Australia
Forbidden History Like A Shot Entertainment
Unexplained iHeartPodcasts
Stuff You Should Know iHeartPodcasts
Barangay Love Stories Barangay LS 97.1 Manila | GMA Network Inc.
Late Night Live — Full program podcast ABC Australia
Australia All Over ABC Australia
The Megyn Kelly Show SiriusXM
Life Uncut LiSTNR
The Poisoned Wife The Australian
The Michael Berry Show KTRH (KTRH-AM)
Mamamia Out Loud Mamamia Podcasts
Papa Dudut Stories Papa Dudut | TAGM Marketing Solutions Inc.
2 Worlds Collide Podcast Sam Bamford
Legends of the Old West Black Barrel Media
