Nach Genre filtern

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu

492 - Ni, Kwanini Wakatoliki tunapokea Mwili wa Kristo katika Umbo la Mkate tuu?
0:00 / 0:00
1x
  • 492 - Ni, Kwanini Wakatoliki tunapokea Mwili wa Kristo katika Umbo la Mkate tuu?

    Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Peter Mjwauzi, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kwanini sisi Wakatoliki tunapokea mwili wa Kristo katika umbo la Mkate tuu na wakati wa Sala ya Ekaristi Padre anasema twaeni mnywe wote?

    Mon, 29 Apr 2024 - 28min
  • 491 - Je, wafahamu mambo gani ya kufanya unapoingia Kanisani ?

    Karibu katika Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Frateri Elikana Nyagabona, anajibu swali lililoulizwa  naomba kujua ninapoingia Kanisani ni mambo gani natakiwa kufanya hadi inapoisha Misa Takatifu?

    Mon, 29 Apr 2024 - 27min
  • 490 - Je, Wafahamu Mashirika yanayotumia neno Bruda?

    Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Faxon Polycarp Mpili, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali linalojibiwa linasema neno Bruda lina maana gani? ni mashirika gani wanatumia neno bruda, na kazi zao ni zipi katika kanisa.

    Mon, 29 Apr 2024 - 19min
  • 489 - Je, Wafahamu vipindi vya Litrujia katika Kanisa Katoliki?

    Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateli Baltazar Bao, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Tunaomba kuelezwa kuhusu vipindi vya kilitrujia katika Kanisa Katoliki maana tumekuwa tukisikia wanasema sasa ni kipindi cha Krismas, mara Majilio mara Pasaka, kiukweli hatuelewi maana yake pia mpangilio […]

    Mon, 29 Apr 2024 - 26min
  • 488 - Je, Wafahamu Siri ya Miaka 28 ya Radio Maria Tanzania kwa Wanautume wake?

    Uinjilishaji  ni wajibu wa kila Mkristo Mbazitwa, Radio Maria Tanzania inarahisisha kazi hiyo ya  Uinjilishaji kupitia vipindi vyake Mbalimbali  Katika miaka 28 ya Radio Maria Tanzania, karibu  uwasikilize Wanautume wa Radio Maria Tanzania wakielezea  Utume huu Miaka 28 iliyopita  kupitia Makala hii iliyotayarishwa na Agatha Kisimba.

    Fri, 26 Apr 2024 - 54min
Weitere Folgen anzeigen