Filtrar por género
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
- 165 - Safari ya Sudan Kusini kuelekea uchaguzi wake mkuu wa kwanzaSat, 26 Sep 2026
- 164 - EAC: Kesi za kisiasa au utawala wa kisheria
Katika kipindi cha miaka ya karibuni, viongozi wa upinzani katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki wameendelea kujikuta mahakamani wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo uhaini.
katika Makala ya Afrika Mashariki, tunaangazia mwenendo wa kesi zinazowakabili viongozi wa upinzani katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, je, ni ishara ya kuimarika kwa utawala wa sheria au kuna maswali yanayoendelea kuulizwa kuhusu ushindani wa kisiasa?
Fri, 11 Sep 2026 - 163 - Kenya yaanza safari ya kutafuta dira mpya, ruwaza ya 2030 ikielekea kufika ukomo
Kenya imeanza safari ya kutafuta dira mpya ya maendeleo baada ya Ruwaza ya Taifa ya Maendeleo 2030 kuelekea kufikia ukomo wake.
Safari hii inakuja wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, ikiwa na dira yake ya pamoja ya mwaka 2050, inayolenga kujenga ukanda wenye uchumi shindani, miundombinu iliyounganishwa, viwanda, biashara, ajira na maendeleo ya watu.
Fri, 21 Aug 2026 - 162 - Tanzania: Nanenane imebaki maonesho ya kilimo au imegeuka soko la biashara?Wed, 12 Aug 2026
- 161 - Safari ya Tohara ya kitabibu kutoka mila hadi afya ya ummaSat, 01 Aug 2026
- 160 - Mazungumzo ya kitaifa yanaweza kuponya majeraha ya DRC?Fri, 24 Jul 2026
- 159 - CCM na ACT-Wazalendo vimesaini makubaliano mapya ya maridhiano.
Baada ya mvutano wa kisiasa uliojitokeza mara baada ya uchaguzi mkuu uliopita huko Zanzibar, sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo vimesaini makubaliano mapya ya maridhiano.
Lakini je, makubaliano hayo yatafungua ukurasa mpya wa demokrasia, au ni hatua ya kujenga utulivu kuelekea uchaguzi ujao?
Makubaliano hayo yaliyosainiwa Julai 9, 2026 yanajumuisha mapitio ya Katiba, mageuzi ya uchaguzi, maboresho ya mfumo wa sheria, kuimarisha uwajibikaji katika utumishi wa umma, kuundwa kwa chombo cha kisheria cha kusimamia utekelezaji wa makubaliano pamoja na kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Hafla ya utiaji saini imefanyika Ikulu Zanzibar mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na viongozi wa dini, serikali na wadau mbalimbali.
Karibu katika Makala ya Afrika Mashariki hii leo tunaangazia makubaliano ya kisiasa kati ya CCM na ACT-Wazalendo Zanzibar, matarajio yake, changamoto zake na athari zake kwa mustakabali wa demokrasia visiwani karibu tuwe pamoja hadi tamati.
Wed, 15 Jul 2026 - 158 - Hali ya Ziwa Victoria na changamoto zinazolikabili
Tunaangazia hali ya Ziwa Victoria, changamoto zinazolikabili pamoja na juhudi za kikanda zinazofanyika kulinusuru ziwa hilo ambalo ni mhimili wa uchumi na maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki.
Ziwa Victoria, ambalo ni tegemeo la mamilioni ya wananchi wa Afrika Mashariki, linaendelea kukumbwa na changamoto kubwa za mazingira, uvuvi haramu na uchafuzi wa maji.
Ripoti mpya ya mwaka 2025 imeonya kuwa bila hatua za haraka, uchumi, afya na maisha ya wananchi wa ukanda huo yako hatarini.
Jumuiya ya Afrika Mashariki imezindua ripoti ya mwaka 2025 kuhusu hali ya Bonde la Ziwa Victoria, ikieleza changamoto zinazoendelea kulikabili ziwa hilo ikiwemo uvuvi haramu, uchafuzi wa mazingira na kupungua kwa samaki muhimu wa biashara.
Ripoti hiyo yenye sura tisa imechambua kwa kina hali ya ikolojia, mazingira, viwanda, mipango miji, ajira, utalii pamoja na maendeleo ya miundombinu katika ukanda wa Ziwa Victoria.
Sat, 30 May 2026 - 157 - Tanzania: Ripoti ya Tume ya uchunguzi kuhusu vurugu za uchaguzi mkuu wa OktobaSat, 02 May 2026
- 156 - Kumbukizi ya miaka 32 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994
April 7, 1994 ni siku ya ambayo historia ya Rwanda ilianadikwa kwa wino mwekundu kumaanisha hatari, kifo cha Rais zamani wa Taifa hilo Juvenal Habyarimana aliuawa akitokea nchini Tanzania katika mchakato wa kusaka amani nchini Rwanda, baada ya waasi wa kundi la RPF wakati huo, ambalo kwa sasa ni chama kilichopo madarakani, kuanzisha vita dhidi ya serikali ya Juvenal Habyarimana, wakimtuhumu kuwatenga raia wa Rwanda kutoka jamii ya watutsi.
Hapo ndipo ghasia zikazuka kote nchini humo kwa jamii ya Wahutu na Watutsi kushambuliana vikali kutoka mijini hadi katika vijiji.
Sat, 11 Apr 2026 - 155 - Kasi na mapokeo ya ueneaji wa akili mnemba barani Afrika
Karibu katika ya Afrika mashariki hii leo macho na masikio ya Makala haya yanatazama kasi na mapokeo ya ueneaji wa akili mnemba barani Afrika tukienega katika Mkutano wa Kimataifa wa AI kuhusu Afrika 2025, unaofanyika Kigali nchini Rwanda Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe soote hadi tamati
Fri, 11 Apr 2025 - 154 - Je una ufahamu juu ya ulinzi wa taarifa binafsi ?
Kasi ya ugunduzi na uvumbuzi katika maswala ya sayansi na teknolojia na ujio wa Internet sanjali na matumzi ya mitandao ya kijamii yanafanya wajamii kuwa katika hatari kumbwa kupoteza usiri wa taarifa zao.
Baada ya mabadiliko makubwa ya teknolojia yamesababisha taarifa za watu kuwa ni moja ya mtaji mkubwa kwa watu wengine na makampuni makubwa
Tanzania kama yalivyo mataifa mengine ya Afrika mashariki imekutunga sheria rasmi ya kulinda haki kulindiwa taarifa binafsi
Lakini sio kulinda tu taarifa binafsi lakini pia kuhakikisha taarifa hizo zinamfaidisha moja Kwa moja mlengwa wa taarifa endapo zinatakiwa kutumiwa Kwa matumizi fulani.
Msikilizaji wa RFI Kiswahili karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwama kuangaza na kumulika kwa namna gani wakazi wa Afrika mashariki wanauelewa juu ya ulinzi wa taarifa binafsi sanjali na juhudi za mataifa katika kulinda maswala hayo Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe hadi tamati
Sat, 05 Apr 2025 - 153 - Tatizo la kifua kikuu (TB) katika mataifa ya Afrika Mashariki
Maambukizi ya kifua kikuu yanaweza kuenezwa kwa urahisi katika miji mikubwa na maeneo ya umma ambapo kuna mkusanyiko mkubwa wa watu, kama vile vituo vya mabasi, masoko, na hata sehemu za kazi kama waendesha bodaboda wanavyojihusisha.
Msikilizaji wa RFI Kiswahili karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwana kuangaza namna waendesha bodaboda wanaweza kuchukua tahadhari ya kupambana na maambukizi ya kifua kikuu Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe sote hadi tamati.
Sat, 29 Mar 2025 - 152 - Tanzania: Namna wakaazi wa vijijini wanafikiwa na huduma za majiSat, 15 Mar 2025
- 151 - Athari za mgogoro wa DRC katika mataifa ya Afrika
Mgogoro wa Mashariki ya DRC umeendelea kwa miongo kadhaa, na bado ni moja ya changamoto kubwa za kiusalama na kisiasa Barani Afrika.
Katika Mashariki ya DRC, kuna makundi ya waasi kama vile M23, ADF, Twirwaneho, ambayo yameongeza umwagaji damu na kusababisha maelfu ya watu kuhama kutoka maeneo yao.
Siasa za kikanda, ushindani wa madaraka kati ya mataifa kama Rwanda yana iweka DRC njia panda kila uchao
Karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii tunangaza mgogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe sote hadi tamati
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu, hasa katika majimbo ya mashariki ya Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Tanganyika, kutokana na migogoro ya silaha na mapigano baina ya jamii. Mnamo Septemba 2024, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)
Sat, 08 Mar 2025 - 150 - Umuhimu wa kutunza lugha mama katika jamii za Afrika
Karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tukiangaza safari ya miaka 25 ya UNESCO kuenzi lugha mama na nafasi ya lugha mama katika kukuza maendeleo ya jamii Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe sote hadi tamati ya Makala haya.
Lugha ni muhimu kwa elimu na maendeleo endelevu, zikitumika kama njia kuu ambayo maarifa hupitishwa na tamaduni kuhifadhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyo chapishwa katika tovuti ya Umoja wa mataifa inaeleza kukiwa na takriban lugha 8,324 duniani leo, nyingi ziko hatarini kutoweka kutokana na utandawazi na mabadiliko ya jamii.
Kuhakikisha kwamba mifumo ya elimu inaunga mkono haki ya mtu ya kujifunza katika lugha-mama ni muhimu sana katika kuboresha matokeo ya kujifunza, kwani wanafunzi wanaofundishwa kwa lugha wanayoelewa kikamilifu huonyesha ufahamu bora, ushirikishwaji, na ustadi wa kufikiri kwa kina.
Sat, 01 Mar 2025 - 149 - Namna wakazi wanaoishi karibu na migodi wanaweza kufaidika na shughuli hizo
Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwama na kuangazia kwa namna gani wakazi wanaozunguka migodi ya madini kupitia uwajibikaji kwa jamii.
Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umekua, na kukua huku ni kutokana na ongezeko la asilimia 7.3 kwa mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 9.
Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hii serikali ya Tanzania imechukua hatua muhimu ya kuhakikisha kwamba wawekezaji wakubwa na wadogo kwenye Sekta ya Madini wanaendesha shughuli zao kwa tija kwa kuwezesha mazingira wezeshi ya uwekezaji na upatikanaji teknolojia unaimarika, hii ni pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ambayo serikali imeamua kuimarisha kwa lengo la kuvutia uwekezaji na kuwezesha uwekezaji huo kuleta faida kwa kila mwekezaji.
Sat, 01 Feb 2025 - 148 - Tanzania: Changamoto wanazokabiliwa nazo watu wenye Albinism mjini Mwanza
Watu wenye ualbino Afrika Mashariki, na hasa nchini Tanzania, wanakutana na changamoto kubwa za kijamii, kisiasa na kiuchumi. Vilevile, wanakumbana na unyanyapaa, ubaguzi, na vitendo vya kikatili vinavyoweza kupelekea madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na mauaji na uharibifu wa miili yao.
Ingawa jamii ya watu wenye ualbino imekuwa na umakini wa kimataifa, bado wanakumbana na hatari na shida kubwa, hasa katika maeneo ya vijijini. Katika hali hii, sanaa ya uimbaji imekuwa chombo muhimu cha kuelimisha jamii na kubadili mitazamo potofu kuhusu ualbino, ikichochea mabadiliko katika matendo na hisia za jamii kuhusu watu hawa.
Wed, 22 Jan 2025 - 147 - Safari ya miaka 61 ya Mapinduzi ya ZanzibarSat, 18 Jan 2025
- 146 - Tanzania: Kuongezeka kwa visa vya ugonjwa wa usugu wa vimelea dhidi ya dawaSat, 16 Nov 2024
- 145 - Uwekezaji katika sekta ya kilimo mkoani Arusha Kaskazini mwa Tanzania
Sekta ya Kilimo inaongoza kuwa na fursa nyingi za uwekezaji kwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kwa mfano uzalishaji wa Ngano, mafuta ya kupikia, matunda na mboga mboga, mbolea, Viatilifu, mbegu bora, vifungashio, kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno na eneo la kilimo cha umwagiliaji.
Fri, 08 Nov 2024 - 144 - Tanzania: Kumbukizi ya miaka 119 tangu kuibuka kwa vita vya majimaji
Karibu katika Makala ya Afrika mashariki, hii leo tunatuwama nchini Tanzania katika Mkoa Lindi uliopo kusini mwa Tanzania mahali ilipo ibuka vita vya majimaji mara hii ikiwa ni kumbukizi ya miaka 119 tangu kuibuka kwa vita vya Majimaji.
Vita vya Majimaji vilipata mizizi yake katika eneo la Nandete Kipatimu, ambapo jamii za Matumbi zilijitokeza kwa ujasiri dhidi ya ukandamizaji wa kikoloni.
Roho hii ya upinzani ilichochea moto ulioenea hadi katika eneo la Ruvuma, ambapo watu wa huko, wakichochewa na ujasiri wa majirani zao, walianza kuungana katika mapambano yao wenyewe.
Wao pia waliharibu barabara walizolazimishwa kujenga, wakigeuza mandhari ya ukandamizaji kuwa uwanja wa vita kwa ajili ya uhuru.
Uasi huu wa pamoja ulionyesha azma inayokua miongoni mwa jamii za kupambana na ukweli mgumu wa utawala wa Kijerumani na kudai heshima yao.
Thu, 24 Oct 2024 - 143 - Wiki ya vijana ilivyoaadhimishwa mjini Mwanza nchini TanzaniaThu, 17 Oct 2024
- 142 - Tanzania: Mradi wa Jenga Kesho Bora ulivyoanza kutoa mazao kwa wafugaji wa samakiFri, 04 Oct 2024
Podcasts similares a Afrika Ya Mashariki
El Partidazo de COPE COPE
Herrera en COPE COPE
La Linterna COPE
Dante Gebel Live Dante Gebel
Es la Mañana de Federico esRadio
La noche de Cuesta esRadio
La Trinchera de Llamas esRadio
Hondelatte Raconte Europe 1
Affaires sensibles France Inter
LEGEND Guillaume Pley
El colegio invisible OndaCero
La Rosa de los Vientos OndaCero
Les grands dossiers de l'Histoire par Franck Ferrand Radio Classique
Espacio en blanco Radio Nacional
Enquêtes criminelles RTL
Entrez dans l'Histoire RTL
Le grand récit RTL
Les Grosses Têtes RTL
L'Heure Du Crime RTL
Parlons-nous RTL
El Larguero SER Podcast
SER Historia SER Podcast
Todo Concostrina SER Podcast
Un Libro Una Hora SER Podcast
